Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Madini

Hon. Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Madini

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia mada iliyopo mbele yetu. Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema kufikia jioni hii ya leo. Lakini pia nianze kumpongeza Waziri wa Madini Mheshimiwa Doto Biteko pamoja na Katibu wake Prof. Shukrani Manya na watendaji wote wa wizara. Lakini pia naipongeza hotuba na naiunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nianze kuipongeza wizara kwa hotuba yake nzuri kwa kuelezea wingi wa leseni ambazo zimeshatolewa kwa wachimbaji wadogo nchini; ikiwemo wachimbaji wadogo wa Jimbo langu la Nyang’hwale. Kwa kweli leseni zimeshatoka PML zaidi ya PML 50 kwa hiyo, wachimbaji wadogo wa Nyang’hwale wanaipongeza sana wizara, Waziri pamoja na Naibu Waziri. Lakini pia ukweli usiopingika, madini yanaliingizia Taifa fedha nyingi, lakini pia tukumbuke madini kote yanakochimbwa kuna athari kubwa ya kimazingira. Nitatoa mfano kwenye jimbo langu la Nyang’hwale kulikuwa na msitu unaitwa Iyenze, kwasababu msitu ule umezungukwa na wachimbaji msitu huo miti yote imekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaangalia namna gani tunavuna sasa hivi, lakini kizazi kijacho fedha hii ambayo tunaipata sasa hivi itarudi tena kwenda kuandaa mazingira. Nilikuwa nataka nitoe ushauri kwamba wizara iweke mpango mzuri wa kuweza kuwakopesha wachimbaji wetu wadogo ili waweze kupata zana za kisasa. Miti ile imekwisha kwenye ile misitu kwa ajili wanaitwa matimba; uchimbaji wowote wa dhahabu unahitaji matimba ni zile ngazi za kuingilia shimoni. Ukiangalia ule msitu wa Iyenze umekwisha na kuna msitu ambao ukitoka Geita unakwenda Katoro na wenyewe unakwenda kuisha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ushauri wangu naomba sana wizara ijaribu kuangalia namna gani ya kuwasaidia wachimbaji hao wadogo waweze kupata zana hizi za matimba ama zana nyingine za uchimbaji ili kupunguza uhalibifu wa mazingira. Lakini ushauri wangu mwingine ni kwamba Wizara ya Madini ishirikiane na Serikali za Vijiji. Nimezungumzia uharibifu wa mazingira leo unakuta maeneo ya wachimbaji ama kwenye vijiji ambako kuna wachimbaji unakuta kila mchimbaji anatengeneza kitu kinaitwa mwalo Kijiji kizima unakuta kuna miyalo miyalo, na ile miyalo inatumika Zebaki ambayo ni sumu, sumu hiyo itakuja kuleta madhara makubwa kwenye kizazi kijacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaiomba Serikali, naiomba sana wizara ishirikiane na Serikali za Vijiji kuangalia angalau maeneo maalum watakayofanyia hizo kazi zao hao wachimbaji kama ni kuharibika eneo liharibike eneo fulani tu. Sio sasa hivi kila mchimbaji, ukikuta kijiji kina wachimba 200 kila mmoja unamkuta ana mwalo kwake anatumia sumu hii ni hatari sana kwa maisha ya wachimbaji wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa waziri nimekupongeza sana, ni mmoja wao wa uanzilishaji wa masoko ya dhahabu. Kama unakumbuka kulikuwa na Kamati ya Naibu Waziri Stanslaus Nyongo mimi nikiwa makamu, tulianzisha na leo kila anayesimama anasema wilayani kwangu kuna duka la dhahabu. Ninakupongeza tulianza vizuri na tunaenda vizuri, tuendelee vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema haya Mheshimiwa, naunga mkono hoja. Ahsante kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)