Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

Hon. Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, Ahsante kwa kunipa nafasi hii kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kupata nafasi ya kusimama hapa nami kutoa mchango wangu. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu wake na watendaji wake jinsi mnavyofanya kazi.

Mheshimiwa Spika, nilianzia kazi maji miaka ya1987 ukilinganisha na leo kweli Serikali imefanya kazi kwenye maji haikuwa hivi. Lakini kwasababu watu wengi wameshaongelea maji, matatizo ya maji na kila kitu mimi naomba nijikite kwenye miundombinu na mapato ya mamlaka zetu za maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajua kuna nyumba za Serikali nyingi, Tanzania nzima nyumba hizi kwenye bill za maji huwa hazilipwi kule kwenye nyumba za Serikali kwenye bill zile. Sasa tuanze kuzifungia prepaid nyumba hizi kuokoa mapato ya Mamalaka za Maji yanayopotea kumekuwa na uzoefu baadhi ya watumishi wa Serikali au baadhi ya viongozi wanahama wanaacha bill kwenye nyumba zile bila bill zile kulipwa sasa hii inakuwa ni hasara kwa Mamlalaka za Maji, wakati mwingine inakuwa ni hasara kwa mtu anayeingia kwenye nyumba ile kuambiwa alipe zile bill ambazo ziliachwa kule.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapitisha bajeti ya kila taasisi hapa ikiwa na gharama za ulipaji umeme na maji, lakini nadhani kwasababu ni Serikali yenyewe kwa wenyewe Wizara ya Maji mnaona aibu kwenda kukata maji kule kwenye zile Taasisi na hawachukuli umuhimu wa kulipa bill za maji. Sasa niwashauri nishauri Wizara ya Maji anzeni kufunga prepaid mita kwenye taasisi za Serikali ili kuokoa yale mapato, tukishafunga hizo prepaid watalipa kama inavyotakiwa na ukiangalia hata kwenye ripoti ya CAG mapato mengine ya maji yanapotea pale taasisi za Serikali azilipi ipasavyo bill za maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hebu twende tukafunge prepaid kwenye hizo taasisi za Serikali walipe kwasababu bajeti ipo, Mheshimiwa Spika unaipitisha hapa na Wabunge tunapitisha ulipaji wa gharama zozote za uendeshaji wa Ofisi za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nijikite tena kwenye miundombinu, Wizara ya Maji au Mamlaka za Maji wanapokuwa wanafunga yale mabomba ya maji watayapitisha kwenye barabara, ujenzi wa barabara ni gharama kubwa nayo kwa Serikali. Sasa niombe tu Wizara hizi mbili wakati mnapoanza ujenzi wa miundombinu mkae pamoja mshauriane kwamba ni wapi miundombinu itapita ili tupunguze gharama za utengenezaji wa barabara zinazobomolewa wakati wa kupitisha mabomba ya maji. (Makofi)


Mheshimiwa Spika, kuna miundombinu ya haya mabomba kuchakaa na kumwaga maji hasa kwa jiji la Dar es Salaam hiyo ndiyo ilikuwa kubwa sana maji yanamwangika hovyo. Niombe tu Wizara ya Maji, tumesema chuo cha Maji sasa havi kinatowa wale vijana hawajapata kuzunguka na kuangalia yale mabomba ambapo maji yanapotea wakafanye kazi ya kuwa wanatoa taarifa mabomba yale yanafanyiwa matengenezo ili maji yasipotee na watumiaji wa maji wasipate bill kubwa.

Mheshimiwa Spika, ninachojua Wizara ya Maji Mamlaka zenu za Maji ni maji salama na safi na maji taka, sasa mnapokua kutengeneza ufungaji wa maji basi fanyeni na ufungaji wa mabomba ya maji taka viende pamoja ili kuweza kufanya hivi vyote vitu viwe pamoja kupunguza gharama na kuweka na kuweka sehemu za miji kuwa salama zaidi.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo niongeze tu kama mtumishi wa wafanyakazi kuna wakurugenzi wengi sasa hivi wanakaimu, mnawatumishi wengi wanakaimu, kukaimu nafasi huwa kunapunguza ushujaa au confidence ya kufanya kazi, basi niombe wale ambao mnaona wamefanya vizuri tunajua sheria inasema akaimu miezi sita, kama unaona ajatosheleza basi mtowe weka mwingine, kama unaona amestahili na amefanya vizuri basi watumishi hawa ambao ni ma-engineers wapeni hizo confirmation ili wawe na uhakika wa kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga hoja mkono ahsanteni sana.