Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia kwenye Wizara hii muhimu na nyeti kwa nchi yetu. Awali ya yote, naomba niunge mkono hoja.
Nimesimama hapa ili niweze kuzungumzia mradi mkubwa wa kihistoria ambao nchi yetu inaendelea nao wa SGR. Nilisamama hapa mara ya mwisho nikauzungumzia, lakini leo nataka nizungumzie na niishauri Serikali namna bora ya ku-finance mradi huu wa SGR.
Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu mkubwa na mzuri kwa nchi yetu kama hatukujipanga vizuri na namna ya kuu- finance vilio vitakuwa vikubwa sana huku kuhusu barabara na mambo mengine ya miundombinu mingine. Hii ni kwa sababu fedha nyingi tunayoipata itakuwa inakwenda hapa, halafu tunashindwa kupeleka maendeleo kwenye maeneo mengine ya miradi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipo kitu kinaitwa credit rating, nimesimama hapa niishauri Serikali kufanya mchakato wa kufanya credit rating ya nchi yetu. Zipo kampuni duniani zinazofanya mchakato huu wa kui-rate nchi na faida ya kui- rate nchi ni kwamba utakuwa na uwezo, ukishakuwa rated una uwezo wa kwenda kwenye masoko ya mikopo makubwa na ukapata fedha kwa kiwango kikubwa na cha uhakika zaidi kuliko ambavyo sasa tuna-finance mradi huu kwa kutumia concessional loans.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza concessional loans zenyewe zilivyo zina masharti mengi na ambayo zinafanya sekta zetu binafsi zisiweze kushiriki kwenye maendeleo. Unapokuwa umechangua finance kwa kutumia concessional, yule anayekupa fedha ndiye anayechangua kampuni ya kusimamia, ndiye anayechagua kampuni ya kujenga pia. Tungekuwa tumejielekeza kwenye kufanya credit rating ili tuweze ku-issue infrastructure bonds, ingetuwezesha sisi kuamua nani tumpe kazi gani kwenye mradi upi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyozungumza nitatolea mfano Standard Charted Bank kwa kushirikiana na Export Credit Agencies walitupa sisi kama nchi mkopo wa bilioni 1.46. Mkopo huu ambao tumepewa kwa ajili ya kujenga hii SGR ni gharama kubwa ku-service mkopo huu kwa sababu gani, kwa sababu ukitumia njia hii ya kupata mkopo ni kwamba unaruhusu madalali katikati Standart Charted hana hela ya…
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kwagilwa kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Getere.
T A A R I F A
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nampa taarifa mdogo wangu Kwagilwa kwamba tunapozungumza habari ya miradi ya kimkakati ya kimaendeleo katika nchi za kiafrika, bora uchague moja, upewe mkopo kutoka nje wenye masharti ya kwamba mradi ukiisha ukishindwa kulipa wauchukue au utafute mkopo wa bei nafuu kwenye nchi yako mradi uendelee kuwa wako. Kwa hiyo ndio mambo tunayopewa kuchagua hayo.
NAIBU SPIKA: Kabla sijakuuliza Mheshimiwa Kagilwa, Mheshimiwa Getere na Waheshimiwa Wabunge wote niwakumbushe humu ndani tumekuwa na mazoea si mabaya tukiitana nje lakini humu ndani ni Waheshimiwa, kuna wakati huwa inaleta changamoto kidogo mtu akiitwa mdogo wa mtu, kaka wa mtu, shemeji wa mtu na mambo kama hayo au mke wa mtu kwa maana hiyo hiyo.
Mheshimiwa Kwagilwa unaipokea taarifa hiyo.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge aliyezungumza inaelekea hajui hiki ninachokiongea, kwa hiyo taarifa hiyo siipokei. Nazungumzia infrastructure bonds, ni mkopo kama ulivyo mkopo mwingine na mkopo huu hauna sharti lolote la kwamba ukishindwa kulipa mradi huu unachukuliwa haiko hivyo. Uki-issue infrastructure bonds kunakuwa na watu wanao-subscribe wengi kutoka nje wenye fedha wanakupa. Hiki ndicho ninachokizungumzia.
Mheshimiwa Naibuu Spika, nilikuwa natolea mfano kwamba tulipata ile 1.6 kutoka Standard Charted, yupo Standard Charted pale, maana yake tumemlipa fedha wako Export Credit Agencies maana yake tumewalipa fedha na yote hii inaenda ina amount kwenye deni letu la Taifa, ungekuwa ume-issue bond ungekuwa umechukuwa tu fedha moja kwa moja kutoka kwa yule anayekukopesha bila kupita kwa mtu mwingine. Hiki ndicho ninachokizungumzia.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukifanya hivyo tutaweza kujenga barabara zetu za ndani kwa makusanyo yetu sasa, haya tunayokusanya kupitia TRA. Kwa mfano, Barabara ya Handeni – Kiteto – Kibirashi – Kondoa - Singida itaweza kujengwa, lakini ilivyo hivi sasa tumefanya bajeti allocation ya bilioni nne, hapo hapo kuna miradi mingine ya barabara kwa fedha hizo, tutakamalisha lini ujenzi wa barabara hizi ambazo ni za muhimu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nashauri kama tutaweza tufanye credit rating kwa kutumia Kampuni ya Standard and Poor, kama tukiweza tufanya credit rating kwa kutumia moody kama tukiweza tufanye credit rating kwa kutumia fitch.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaweza kufanya kwa kutumia kampuni mbili au tukiona ni gharama tufanye kwa kutumia kampuni moja. Tafsiri ya credit rating ni kwamba mnakuwa declared kama nchi ambayo ina uwezo wa kuhimili deni na kulipa pale inapogoma. Hiki ndio tunachokishauri na ndicho ninachokishauri kifanyike na Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunapozungumza kwenye huu mradi huu wa SGR mpaka sasa loti Na.3 haina fedha na haina mkandarasi. Mpaka sasa loti Na.4 Tabora - Isaka haina fedha na haina mkandarasi, hata hii unayoongelea loti Na.5 ya Isaka - Mwanza wamekuja Wachina hapa wameahidi kutupa 1.32 bilioni, hiyo ni concessional loans, sharti la kwanza kampuni zao mbili ndio zijenge. Ndugu zangu hatutaweza kulinda hata ubora wa mradi wenyewe, yaani mtu anapokupa, ajenge yeye, asimamie yeye, sasa wewe ushiriki wako ni upi kwenye hii? Tukiangalia kwenye sekta ya ujenzi ndio sekta ambayo imekuwa mfululuzo kwenye miaka hii ya karibuni lakini watanzania wanashiriki vipi kwenye sekta hii ya ujenzi, hawawezi kushiriki kama tunaendelea kuchagua financing za namna hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nimeongea kwa wakati, nikushukuru sana kwa nafasi na naunga mkono hoja. (Makofi)