Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba ya Wizara hii. Hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu. Wizara inawahusu wananchi wote wa nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; nikianza na mafunzo kwa watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Wizara hii kwa mipango yake madhubuti ya kuiongoza Wizara hii. Kwa kweli wanaendeleza na kuiongoza Wizara hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, dunia sasa hivi inaendelea kwa kasi sana kwa nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kitekhnolojia. Hivyo basi ili kuenda sambamba na kasi hiyo hatuna budi kuwapa fursa za masomo watendaji wetu. Lazima tuwasomeshe ili waweze kufanya kazi zao kiutaalam na kisasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2020 Wizara hii iliahidi kutoa mafunzo kwa watendaji 700. Lakini mpaka hotuba hii inasomwa leo ni asilimia 19.5 tu ya ahadi hiyo ndio ilioweza kutekelezwa; yaani ni watendaji 137 ndio waliopata mafunzo; hii ni idadi ndogo sana. Pamoja na kwamba Wizara haikusema sababu ya kutokifika lengo hilo lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hii ni idadi ndogo kabisa.Ushauri wangu kwenye jambo hili kwa Serikali kuweka kipaumbele cha hali ya juu kutoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara hii ili kuenda sambamba na kasi ya ukuaji wa kiitaalam duniani.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ni kuhusu utawala na raislimali watu. Rasilimali watu ni kitendea kazi katika Wizara. Ni lazima suala hili lifikiriwe kwa nguvu zote. Upungufu wa wafabyakazi 3,114 katika nchi ambayo kila mwaka inatoa wahitimu wengi, ni kitu ambacho hakipendezi. Ushauri wangu kwa suala hili kwa Serikali ni kutoa fursa za ajira kwa vijana ambao wapo wengi sana katika nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.