Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Wizara hii ni miongoni mwa Wizara muhimu katika kuendesha uchumi wa nchi yetu.

Pili, natoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwasilisha katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia maeneo yafuatayo; kwanza ni kuhusu mazingira ya kibiashara katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali kwa juhudi kubwa inayochukua katika azma yake ya kuelekea kwenye suala la biashara. Ni azma nzuri ambayo itatuvusha katika kuinua uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lolote linahitaji matayarisho ya kufanikisha jambo hili. Matayarisho hayo ni kuliwezesha jambo hilo kufanikiwa. Bado katika nchi yetu hatujaweza kufanikisha kutayarisha mazingira bora ya kibiashara. Wafanyabiashara wengi hasa wawekezaji wanapata usumbufu namna ya kupata hudumu hasa ya usajili wa biashara zao. Bado kuna mzunguko wa kupata ruhusa ya kufanya au kuwekeza biashara zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ni kuendelea kwa kasi kubwa kutengeneza mazingira yatakayowavutia wawekezaji wa nje na ndani.

Pili ni kuhusu uhusiano kati ya biashara na kilimo; ni jambo muhimu na ni lazima katika kuleta maendeleo ya kiuchumi katika nchi. Viwanda vyovyote haviwezi kutekeleza malengo yake bila ya kilimo. Kilimo ndio kitakachotoa malighafi ya kuendeleza kiwanda.

Ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kutengeneza mazingira ya kupunguza bei za pembejeo za kilimo ili wakulima waweze kuzalisha mazao ambayo yatapelekwa viwandani kuweza kuendesha viwanda kwa kuzalisha mali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mono hoja.