Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi nichangie na mimi katika Wizara ya Michezo na nitachangia kwenye upande wa maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
Mheshimiwa Spika, tukizungumza michezo kwenye Taifa sio tu ni sehemu ya kujenga afya ya mwili, lakini michezo pia ni sehemu ya kutangaza nchi, lakini pia michezo ni sehemu ya kuimarisha umoja na mshikamano wa nchi; lakini pia michezo ni ajira hasa hasa kwa vijana kwa sababu tunajua hata wanamichezo wapo ambao wamekuwa wakipunguza muda wao ili waonekane kama ni vijana kwa sababu inaonekana michezo pia ni kwa ajili ya vijana, hasa football na mingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pia kwa nchi yetu TFF ndio wamekuwa wasimamizi kwenye upande wa mchezo wa mpira wa miguu Tanzania. Kwa hiyo, haitakuwa busara kama hatutazungumza yaliyopo kwenye TFF.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2017 Tanzania ilikuwa mwenyeji kwenye mashindano ya vijana Barani Afrika - AFCON ambako Mheshimiwa Rais, Hayati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliatoa shilingi bilioni moja na mashirika mengine na taasisi walichanga kwa ajili ya kusaidia kufanikisha mashindano ya AFCON 2017. Lakini pia baada ya wageni kuja kulifanyika vitu vingi sana ambavyo kimsingi vilileta taharuki kwa TFF kiasi kwamba TAKUKURU waliingilia kati kwa ajili ya kwenda kuchunguza ubadhirifu wa fedha ambazo zilichangwa pamoja na fedha iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kipindi kile. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, TAKUKURU walichunguza mpaka leo hatujajua nini kinaendelea, hatujapata feedback kujua nini kilionekana huko kwamba walikutwa na hatia au hawakukutwa na hatia. Naomba Waziri atakapokuja kuhitimisha aeleze nini kilitokana na uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU kwa TFF ili kujua matumizi ya zile fedha, kwa sababu mpaka sasa hivi Hoteli ya Holiday Inn ambayo wachezaji walikwenda kufikia pale baadhi waliotoka nje inadai shilingi milioni 80. Kwa hiyo, nitapenda Waziri atuletee feedback nini kiliendelea ili Watanzania wajue, kwa sababu TFF kiukweli inalalamikiwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini mwezi Julai, TFF inakwenda kwenye uchaguzi; sasa hivi wamebadilisha Katiba yao, kinyume na Katiba ya nchi, kinyume cha FIFA, kinyume na CAF wameweka kigezo cha elimu cha juu kuliko inavyotakiwa. (Makofi)
Sasa tunapata dukuduku kidogo kuona kwamba kwa nini wanakaribia uchaguzi halafu wanabadilisha badilisha katiba bila ya kufuata utaratibu. Na Wizara hatujaisikia ikisema chochote kwenye hilo yaani TFF imekuwa kama ni dude kubwa hivi ambalo ni ligumu kulifikia, ni kama wanalindwa fulani nisiende huko sana, lakini tunataka tusikie Wizara inazungumza nini kuhusiana na TFF kubadilisha Katiba yake kwenye suala la elimu, wameweka kiwangu tofauti kabisa hata na utaratibu wa nchi.
Mheshimiwa Spika, lakini TFF imeonekana ikiwaonea baadhi ya viongozi wa michezo kwenye nchi. Nitatoa mfano wa Mwakalebela aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga. Ukionekana unakosoa TFF unakuwa labeled kama mtu ambaye uko against TFF na wanakushughulikia vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa TFF nitapenda Wizara wakati inafanya hitimisho itoe majibu kwenye hayo kwa kweli ni sehemu ambayo inaleta mtanziko mkubwa kwa watu ambao ni wapenda michezo.
Mheshimiwa Spika, lakini pia nitazungumza kuhusiana na kukuza vipaji vya wanamichezo wetu kwenye nchi. Tumezungumzwa kuhusiana na sports academy. Mimi nina fikra tofauti kidogo kwa sababu mimi ni muumini wa Tanzania, ninapenda michezo lakini pia ni muumini wa timu ya Taifa ya Tanzania.
Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba timu ya Taifa inakuwa constituted na vilabu yaani na vilabu, kwa sababu ni miaka mingi tumezungumza tumesema kwamba tutengeneze sports academy kwenye nchi, lakini haifanikiwi, ninachojaribu ni kutoa solution ya tunaweza kufanya nini kutokana na experience ya nchi nyigine. Nigeria inaonekana inafanya vizuri sana kwenye michezo, lakini Nigeria hata zile private sector wana football academy nyingi na zinafanya vizuri na ndio Serikali inategemea huko. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri badala ya kuimba kila siku tutaweka football academy ya Taifa Stars na haifanikiwi, nafikiri kuna haja ya kuwezesha hizi sports academy za club kama Namungo, Ruvu JKT huko kwa sababu tunategemea wanamichezo wetu watoke kwenye hizo klabu. Ni kweli kwamba tunategemea pia nchi zingine kutuletea wanamichezo kwetu, lakini pia mimi nafikiri tutengeneze ndani zaidi kwa sababu ndio tunaowategemea na tuna-feel proud kama tutapata kina Samatta wengi zaidi maana yake ni faida pia kwa Taifa, kwanza anatangaza Taifa, lakini pia inaleta hamasa kwa vijana wengine ambao wanafanya michezo Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nafikiri sasa Serikali kuna sports academy Tanzania nitazitaja na najua Waziri either anazifahamu au kama hazifahamu aangalie namna ambavyo unaweza kuzisaidia. Kwa upande wa shule, shule ya Fountain Gate Academy, sports academy wanafanya vizuri sasa hivi wameingiza timu ya wasichana under 17. Wanafanya vizuri sana na mnajua kuna football academy Morogoro na hapa ya Fountain Gate, they doing very great na hapa kwa kweli kwenye hili nawapongeza pia Simba Queens chini ya uongozi wa Fatma Dewji kwa kweli wanafanya vizuri pamoja na kwamba mimi mwenyewe Simba tunawapongeza Simba wale. Lakini Simba Queens kwa sababu wanafanya vizuri sana this time tunawapongeza pia na nafikiri wanahitaji kupewa support kwa namna moja ama nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kuna sports academy kama Roho Sports Academy, Gymnastic Sports Academy, Dar es Salaam International Academy, A Future Stars Academy, Football Academy Arusha, Street Children Sports Academy, Faome Highway and…
T A A R I F A
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Nusrat.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, nilitaka nimpe taarifa Mbunge anayeongea sasa kwa kuwa amesema kwamba timu ya Simba Queens Sports Club inafanya vizuri sana na kwa misingi hiyo mimi nilikuwa nataka niseme kwamba angeendelea kuongelea kwamba hii timu walau sisi Wabunge tungewachangia ili kuwatia motisha waendelee kufanya vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na kwa msingi huo nimuombe Mheshimiwa Nusrat atoe hoja ili sisi tuiunge mkono na hawa vijana wetu, mabinti zetu waweze kupata motisha ili waweze kufanya vizuri zaidi. Ahsante. (Makofi)
SPIKA: Unapokea hiyo hoja Mheshimiwa Nusrat. (Kicheko)
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, naipokea na kimsingi hili ni suala tunaweza pia kusema ni la Kibunge zima, kwa hiyo, Yanga pia watulie ikifika na wao hatua yao, kwa kweli hili kama itabidi tuweke utaratibu mzuri ili watu waichangie Simba Queens, kwa hiyo naipokea. Nafikiri niendelee kuchangia.
WABUNGE FULANI: Endelea.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, kwenye sehemu ya kukuza vipaji kwenye Taifa kwa masikitiko makubwa sana…
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Taarifa.
T A A R I F A
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi naomba nimpe taarifa Mbunge anayechangia kwamba anapoipongeza Simba kufanya vizuri ajue kwamba kuna mwanamke lazima ampongeze pia Barbara kwamba wanawake sasa hivi hata Yanga wakimuweka mwanamke wanaweza wakafanya vizuri zaidi. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Nusrat unapokea taarifa hiyo kwamba wanawake mnaweza?
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, naipokea na nilimtaja Fatma Dewji kwa sababu ndio anasimamia Simba Queens, lakini Barbara ndio top in charge mwenyewe kwa hiyo tunampongeza. Yanga tulieni! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, upande huo huo wa kukuza vipaji, nasikitika sana kuna dada anaitwa Hadhara Charles Mjeje alishinda mashindano ya football free style ya danadana mnamfahamu, alishinda na anatoka Tanzania mpaka Rais Donald Trump alim-post, alifanya video call na Messi, walimpongeza sana na kuna baadhi ya makampuni walijitolea kuingia naye kwenye contract kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao za michezo kwa sababu she is really good.
Mheshimiwa Spika, lakini nasikitika sana alikuwa amepata deal ya ten years akafanye na kampuni moja ya kutangaza bidhaa za michezo South Africa, lakini inaonekana Serikali iliomba ile kampuni ibadilishe muda isimuwekee ten years mpaka tunapozungumza yupo mtaani na juzi alikuwa anahojiwa, ana maisha magumu mno.
Mheshimiwa Spika, ina-demoralised, inashusha morali na ari ya vijana na wote watu wa Tanzania ambao wanajituma sana na wanavipaji ambavyo wamebarikiwa. (Makofi)
Sasa kuna siku moja ulizungumza kuhusu less government kwenye intervention, Serikali ni sehemu moja wapo ya kuweka link kati ya wananchi na yenyewe Serikali kwa maana ya utaratibu, lakini isiwe kikwazo cha kusaidia vijana wetu na wana michezo wetu kufanya vizuri kwenye Taifa. Kwa hiyo, nafikiri huyu sasa kwa sababu pia umri pengine umekwenda na nini, lakini ikitokea vijana wengine wana uwezo wa kufanya vizuri, tunahitaji sana kuwasaidia. Tunategemea Wizara iwe sehemu ya kuwa-link na kuwasidia kwa sababu wanatangaza nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi uki-google unaandika Mtanzania aliyepostiwa na Donald Trump, unaweza kusema ni kitu kidogo, lakini Tanzania imeshaingia kwenye hiyo statement Tanzania imeshaingia, lakini pia is our very own, ni wa kwetu, kwa hiyo vitu vya kwetu lazima viwe protected sasa in the same spirit tunaomba Diamond Platinum asaidiwe kuhakikisha kwamba anashinda tuzo anayogombea kwa sababu in the name of the country, ukiachana na hivi vitu vyote, kwanza ukweli usiopingika anafanya vizuri, huo ndio ukweli anafanya vizuri, very good. Kwa hiyo tuna sababu pia kila sababu ya kumsaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pia nimalizie kwenye upande wa wasanii wetu, namna gani tunaweza tukalinda kazi za wasanii wetu na kwa kweli pamoja na mambo yote Serikali imekuwa ina mkono mzito sana kwenye kuwabana wakifanya vibaya. Lakini kwenye kuwasaidia imekuwa ni changamoto kubwa sana. Nashauri kuundwe chombo maalum ambacho kitakuwa kina waratibu wasanii wao, najua kuna vyombo vingi huko, lakini kuna mgawanyiko na ninyi mnajua kuna madudu mengi sana yanaendelea huko, wana mambo yao wenyewe ndani wanajua kina Mwana FA.
Mheshimiwa Spika, lakini nafikiri pia kuna namna ambavyo hata kupiga kazi zao. Nashauri Serikali itoe mwongozo asilimia 80, yaani asilimia 100 ya kupiga nyimbo za wanamuziki duniani basi asilimia 80 zipigwe za Watanzania, zipigwe za kwetu. Hilo suala mnaliweza, ni suala tu la kutoa mwongozo.
Mheshimiwa Spika, tunahitaji vijana wetu wanaofanya muziki wapate coverage kubwa na wajisikie fahari kufanya sanaa Tanzania. Ukweli ni kwamba Afrika Mashariki nchi ambayo inafanya sanaa nzuri ya uimbaji ni Tanzania. Wakenya wapo wanapiga tu kazi zetu kwenye club zao, redio zao na television zao kwa sababu tunafanya muziki mzuri. Kwa hiyo, ikawe pia ilete tija. Kamati imeshauri kuhusu aggregation na mimi nashauri na naongezea hapo hapo kwamba ili wapate kipato, wekeni utaratibu mzuri kuwasiliana na Wizara ya TEHAMA kuona namna gani wasanii wetu wanaweza wakapata faida kutokana na kazi zao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana kwa kunipa nafasi. Nategemea majibu ya maswali niliyowauliza Wizara kwenye masuala ya TFF, kwa kweli ni very important, tunahitaji kusikia mnazungumzaje kuhusu TFF. Ahsante. (Makofi)