Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia kwenye bajeti hii ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, suala la pango limeongelewa sana labda sitalirudia rudia sana, lakini niseme tu kwamba hata ripoti ya CAG tangu nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati hii mwaka wa sita sasa imezungumzia sana fedha nyingi inayopotea kwenye kulipia fedha za pango kwenye Balozi zetu mbalimbali. Ni wazi kwamba fedha zile zingekuwa tumejenga ofisi zetu, kwanza mpaka sasa hivi tungekuwe tumeshamaliza na ofisi zile zingepangishwa.

Mheshimiwa Spika, lakini niseme pia kwamba pamoja na hayo, ukiangalia kwa mfano Ubalozi wetu wa Washington, Mheshimiwa Liberata Mulamula - Waziri wewe nakufahamu sana na cv yako ni nzito hebu tembelea Ubalozi wetu tena uangalie. Inasikitisha na ni aibu, yaani jengo limechakaa, ni aibu furniture ni za zamani, labda ziwe zimewekwa mwaka jana ambapo sijakwenda. Lakini hata ukifika pale layout yake inatisha, yaani unatoka Ubalozi wa Kenya, uone wenzetu walivyopanga ofisi zao za kibalozi, ingia yetu ya Tanzania, utafikiri tupo ofisi ya Kariakoo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nakuomba sana tukaangalie hizi balozi zetu jinsi ambavyo zipo katika hali mbaya na ya aibu. Hiyo itatuwezesha kuona umuhimu wa kujenga majengo ya kisasa ambayo ni mazuri na kuweka furniture ambayo inayoendana na nchi yetu ambayo tumesema tunaingia katika uchumi wa kati.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo maadili ya staff, nimekwenda kwenye balozi nyingi nyingi kitu ambacho nime-observe bado sisi sio staff wote, lakini pale unapokutana nao kwenye mambo ya visa kuna rafiki zangu wanasema hebu tukusindikize kwenye ubalozi wenu tukapate visa, utapata aibu. Sitawataja hapa maana si vizuri, lakini unakuta watu wameweka maandazi, wameweka vitumbua, wamekaa wanakula, ukifika wanakuchekea, karibuni karibuni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu amekuja yupo serious katoka labda state ya mbali, anataka ahudumiwe haraka haraka, lakini anakutana na watu wanacheka cheka, wameweka maandazi yao hapo, wanakula, hawana hata aibu. Sasa unasema hivi kweli ile shule yetu ya Diplomasia si inafundisha watu ethics, enheee kwamba mnajiwekaje, mkiwa kwenye ubalozi mna-behave vipi, lakini hilo kwa Watanzania sisemi ni wote, wala sisemi ni Balozi zote, lakini sijui kama Europe na Marekani kuna Balozi za wenzetu ambazo sijaingia. Kwa hiyo tuna tatizo hilo kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia nizungumzie watanzania wengine tunaokwenda kwenye delegation za nje. Hili halipo kwenye ripoti sijaliangalia, lakini zamani tulikuwa delegation ikitakiwa kwenda nje, Chuo chetu cha Diplomasia wanakaa nao wanawaeleza, sasa hivi ni wengi, lakini tuwe na mikakati ya kueleza watu wetu. Unakuta mmekwenda na delegation kikazi karibu three quoters wamekwenda shopping, mmekaa watu wawili/watatu pale. Tunaaibisha kwamba kweli tumekwenda kufanya shopping hatukwenda kwa ajili ya yale yaliyotupeleka kama mikutano, ni aibu kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia table manners ni kitu muhimu sana, ni kitu hatukiongelei lakini nataka tukiongelee. Unakuta mmepangiwa buffet, mtu anajaza lisahani mpaka chakula kinamwagika, enhee! Yaani wakati tungefundishwa huku kwetu tumezoea kujaza maana utakula mara moja basi, lakini kule wenzetu buffet urudi hata mara tatu/mara nne. (Makofi/Kicheko)

Nimgeomba sana tuwe na njia ya kutengeneza semina ambazo zinahamasisha au zinaeleza ethics za kwenda kula kule nje. Niliona moja niliaibika sana, mtu kaenda kachukua supu na mkate kaweka, kaenda kajaza chakula, alivyomaliza alisema sasa nishushie na supu sasa, yaani ile supu ya starter yeye ndio kafanya ndio ya kushushia. Sasa wanatuangalia kwamba hawa watu gani hawa, wametoka wapi! (Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa hao ni Wanyamwezi, Wasukuma. (Makofi/Kicheko)

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, unaogopa kusema tumetoka Tanzania.

Kwa hiyo naomba sana yaani tuangalie hivi vitu vya kidiplomasia, it matters a lot kwamba tuna-portray picha gani tunapokenda nchi za nje.

Mheshimiwa Spika, lakini pia tuangalie hii Sera ya Diplomasia ya Uchumi. Nimefurahi mlivyoonesha kwamba mnaifanyia kazi na mnaikamilisha. Mimi ningeomba tu, kwenye sera ile sijaisoma, kwa hiyo, siijui. Lakini nadhani tuwe na priority ya kuonesha kwamba mabalozi wetu tuna-identify, kwa mfano, Balozi aliyepo Uchina au Japan au New York au wapi tunakupa kwamba ututafutie wawekezaji kwenye maeneo hayo, tuwe specific ili mtu asiamue tu yeye huyu anakuja kutengeneza tu wine hapa na nini, kumbe tuna vitu vingi ambavyo vinge-create employment, viwanda kama vya pamba, tuchakate pamba, tutengeneze nguo, tu-add value kwenye products zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, which means Wizara ya Mambo ya Nje wakikaa na Wizara ya Viwanda na Kilimo wanaweza ku-prioritize zile areas ili wawape mabalozi kwamba hizi ndio areas ambazo tunaona mzipe kipaumbele wafanya mikakati ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzetu utakuta Wachina walikuwa nyuma sana, ni miaka kumi tu walitutangulia, lakini sasa hivi wanasaidia karibu Afrika nzima. Kwa nini, wao walilenga mwekezaji anayekuja wanampa conditions sisi tunataka uwekeze hapa, kama huwekezi hapa basi kwaheri. Halafu sasa sisi wewe unampa mtu, anaweka kakitu kadogo amechukua ardhi kubwa halafu returns zake hatuzioni.

Mheshimiwa Spika, area nyingine nakata kuzungumzia, sasa hivi tunataka ku-promote Kiswahili kuwa lugha ya Taifa na nchi nyingi za nje zimekubali zitumie lugha ya Kiswahili, lakini nakumbuka kuna chuo kimoja tu nafikiri ni Michigan, Mnigeria ndio anafundisha Kiswahili kule, wakati nafikiri tungekuwa na mipango mikakati kwamba ni sehemu zipi au vyuo vipi vinahitaji vya huko nje kufundishwa Kiswahili, tukaomba jinsi nchi yetu inavyoweza kutupia wale walimu wakapelekwa kule. Lakini hapo hapo na sisi kwa vile tunakwenda kwenye Kiswahili, unakuta lugha ya kingereza itatutupa nje. Sasa hivi lugha ya Kiingereza bado ni tata, je, tutakapoingia moja kwa moja Kiswahili itakuwaje.

Mheshimiwa Spika, zamani kulikuwa na wale volunteers from nchi kama za Marekeni, Uingereza na nakumbuka…

(Hapa kengele ililia)

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Nafikiri kengele ya kwanza hiyo.

Nakumbuka Waingereza walikuwa na retired officers ambao ni walimu na walikuwa tayari wapelekwe nchi za nje kama Tanzania waje wasaidie kufundisha Kiingereza ambacho mahitaji yao wao walitakiwa nyumba tu wala sio malipo. Hebu tuwape mabalozi wetu kazi za kuweza ku-identify hizi areas kuona kwamba je, hatuwezi kupata walimu wa kutufundisha Kiingereza propery. Maana ukiangalia sasa hivi hata mtu akitoa speech hakuna wale wenzetu makabila watanisamehe ambao “r” anasema “lailway” hasa nitasema “lailway” ni kitu gani ni “railway” hiyo. Sasa unakuta mtoto wa kwanza anafundishwa kingereza na mtu ambaye kwao hakuna “r” au Kiingereza chenyewe huyo anayekifundisha naye ni mbabaishaji, watoto wetu watajifunza lugha gani.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo unakuta kwamba tunakuwa tuna-specialization kwamba sasa Kiingereza iwe tuna-specialize kwa hiyo tunakijengea mikakati au Kifaransa au Kichina tupate walimu wazuri wa kufundisha vizuri ambao watafundisha ile lugha kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, sisi nchi yetu bado tuna nafasi sana ya ku-liaise na mabalozi wetu tukapata volunteers kama hatutaweza kuajiri walimu hao ambao wakatusaidia na pia hata kupeleka walimu wetu nje wapate exposure. Unakuta mwalimu anafundisha Kiingereza hajawahi kumsikia muingereza mwenyewe akiongea, kwa hiyo unakuta hata anavyofundisha inakuwa ni aibu.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Nje ni kioo chetu kwa nchi za nje, kwa hiyo ningeiomba Wizara mtusaidie sana kuonesha kwamba Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa sana, lakini tumekwenda zaidi katika ombaomba, tuna-feel proud tukiona nchi fulani inatusaidia, inatukopesha. Tutoke huko, tuangalie kwamba namna gani tuangalie kanchi kadogo kama Indonesia. Indonesia hawana resources kabisa, natural resources lakini wamewekeza kwenye skills za watu wao kiasi kwamba wameweza kukuza uchumi wao kwa hali ya juu sana kuliko kutegemea mikopo au misaada. Misaada inatudumaza, misaada inatufanya kwamba kila tukikaa unasema wawekezaji au wahisani hawajatupa fedha, sasa matokeo yake nchi ambayo tuna utajiri mkubwa kama sisi Tanzania kwa nini tu-rely kwa donors kila wakati tunakuwa ombaomba. Ahsante sana. (Makofi)