Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Jang'ombe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante awali ya yote kwanza nishukuru kwa kupata hii nafasi nimshukuru mwenyezi mungu na pia niishukuru Serikali hii inavyokwenda vizuri hasa katika mambo ya nje kwa hiyo ni jambo la kupongezwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nataka kuzungumzia mambo matatu katika East Africa na nitaanza kwa msemo unaosema ndege wenye bwawa za rangi moja na mlio mmoja siku zote huwa wanaruka pamoja. Na katika nchi zetu hizi za Afrika Mashariki ni sawa na kusema ni ndege wenye bwana za rangi moja na mlio mmoja basi pia kuna stahiki tuwe tunaruka pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, inapotokea kwamba mruko wa pamoja hatuupati, basi ujue hapo kuna ndege ameshabadilika mbawa, mlio na ndege huyo wakati mwingine anaweza tukasema anaweza anastahili kutengwa. Sasa jambo la kwanza ambalo linalozungumza kwanza nipongeze Serikali kwa mahusiano haya mazuri tunayoyaendeleza maana sisi Tanzania ni kinara katika kuendeleza masuala haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru Serikali ya kuendeleza masuala haya tunaishukuru Serikali pale Rais alipotoka kwenda Kenya, tukakubaliana masuala ya biashara, tunaishukuru tena Serikali Rais alipokwenda Uganda, tukakubaliana mambo ya biashara, tunaishukuru tena Serikali Rais aliyepita naye pia alipatana sana na Burundi na tukapanga mipango yetu ya maendeleo katika nchi zetu hizi za East Africa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mawaziri nao wa sekta nao tumewaona kwamba nao wamekwenda wameshirikiana na wenzao na hili ndilo jambo linalotakiwa. Sasa kuna kitu ambacho kinaweza kikaondosha mazingira haya ya biashara. Katika protocal yetu ya East Africa kuna ibara ya 24 ambayo katika article hiyo ya 24 inahitaji kuwa na Kamati ya Biashara; kamati hii ya biashara hata panapotokea matatizo inatakiwa watu wakae na waweze ku-solve disputes zote zinazotokea.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mpaka hivi sasa mwaka wa 16 hii Ibara haijatekelezwa hakuna kamati iliyoundwa ya biashara na ndio maana leo Tanzania utasema fungia mahindi yasiende Kenya, kesho mahindi yanapelekwa Kenya, Kenya wanasema rudisha, leo tumekaa hatuna mapatano mengine ambayo yaliyokuwa sio ya kikodi kwa sababu hii article haijatekelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niiombe Serikali ili hii article iweze kutekelezwa na kwa mujibu wa ile sheria tokea imetungwa wakati nchi hizi za East Africa zipo tatu peke yake. Ilikuwa kuna Uganda Kenya na Tanzania na ndio maana katika hiyo article kilichozungumzwa humo ni wajumbe tisa, watatu kutoka kila nchi. Sasa hilo ndipo tunaiomba Serikali ikae Waziri wetu wa Mambo ya Nje, Mama yetu unayependeza sana na unapendwa na watu pamoja na kijana wako hapo mwende mkaunde hii kamati, hayo matatizo yote ya biashara kwa sababu hii kamati haipo na huku haya yaliyopangwa mengine ya biashara yakija kuvurugika tunakaa kikao gani cha kuyapanga, maana wameenda kukua Marais, hawa wajumbe wengine walikuwa awaendi na walikuwa hawapo kwa hiyo hilo ni moja..
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili ambalo nataka nizungumzie kuhusiana na hao ndege wenye mbawa moja; katika ukurasa 51 paragraph ya 100 ya hotuba ya Waziri ameongea hapa kuhusiana na kwamba nchi hizi wananchama zilikutana na wakasema kwamba mwanachama anaweza kuendelea na mkataba wa ubia wa uchumi wa EPA. Kwa hiyo nchi zinazotaka ziruhusiwe lakini hilo jambo limefanyika Februari, 2021 Kenya alikwisha jiunga mapema, huyu sijui kama ndege ambaye ana rangi za kwetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa sababu nchi zote tulikuwa tunaogopa kuja kuondoa protocol yetu hii ya customs union, yeye atakapokuwa anapata bidhaa na anafanya biashara na nchi za Jumuiya ya Ulaya ina maana kwamba tayari kuna mambo yetu ambayo tumekubaliana humu ndani yatakuwa hayaendi sambamba.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa mujibu wa Ibara ya 37.4 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha hapa tunatakiwa wote tuwe kitu kimoja na yeyote anayetaka kujiunga huku basi kwanza atizame yale makubaliano yetu kwamba hayawezi kuharibika. Lakini hapa kuna wenzetu wameshajiunga sisi tunasema kwamba tumekubaliana waruhusiwe kumbe tayari wameshajiunga na ndio maana nilianza na msemo ule msemo wa ndege wenye rangi moja huruka pamoja, lakini sasa inaelekea tuna rangi tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja suala lingine ambalo alilizungumza Mheshimiwa Taska kwamba tunawatuma Wabunge wa Afrika Mashariki, lakini hawawajui wanaenda kufanya kitu gani. Mimi ninachoshauri tuwe na sera sisi Tanzania yakuiendea Afrika Mashariki kama hatuna sera ni kweli wale hatukuwa instrument tutakuja kuwauliza nini, tuliwaambia wakafanye nini, sasa inawezekana wakaja wakaunga kipaumbele cha nchi nyingine kwa sababu sisi wenyewe hatuna sera. (Makofi)
Mheshimiwa Naibi Spika, sera tungekuwa na mkakati, mkakati tungekuwa na malengo ambayo tumejiwekea na vipaumbele vyetu. Kwa hiyo, mimi nashauri tuwe na sera yetu ambao vipaumbele vyetu, vitakuwemo kwenye hii sera na hapa ndipo tutakapokwenda vizuri na tutawajua hawa Wabunge kwa sababu watakuwa tayari wana instrument, watakapokuja kuomba kura aliyekuwa ameenda kinyume na sera na lile ambalo tunalolitaka sisi kama Tanzania basi tuna uwezo wa kumlaumu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hapa hatuwezi kuwalaumu kwa sababu hakuna hiyo sera ya Tanzania kuendea East Africa kwa hiyo, naliomba hili nimeomba mambo matatu tukafuate kanuni ya 37(4) haidhuru tunasema kwamba mtu anaweza akaruhusiwa, lakini tuangalie athari zitakazokuja kutokezea kiuchumi na kibiashara, kwa sababu tuna makubaliano ya kibiashara na nchi za East Africa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naliomba hili nimeomba mambo matatu tukafuate kanuni ya 37(4) haidhuru tunasema kwamba mtu anaweza akaruhusiwa lakini tuangalie athari zitakazokuja kutokezea kiuchumii na kibiashara kwa sababu tunamakubaliano na biashara na nchi za East Africa. Na lingine nimeomba kuwepo na sera Waziri atakaposimama hapa kwa nini kwanza hii sera haipo, lakini atuambie lini hii sera itakuwepo.
Mheshimiwa Naibu Spika, na lingine tunazungumzia kamati ya biashara ya East Africa iwepo, haya yote tunayoenda kukubaliana ikatokezea mizozo hatuna mahali pakwenda tukakaa tuka-solve huo mzozo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri niombe jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine wamenituma wananchi tena hawa ni wa Jang’ombe, wameondoka wameenda Uganda juzi, wamepimwa vipimo vya corona vingi sana, kwa hiyo, mimi kama Mbunge wao nilisikitika sana na kwa sababu hatuaminiani katika Jumuiya hii ya Afrika Mashariki…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Nashukuru kupata nafasi naunga mkono hoja. (Makofi)