Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

MHE. OTHUMAN HIJA JUMA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukuwa fursa hii kutoa shukurani zangu kwako kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. Hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimae kuiwasilisha katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo. Kwanza ni kuhusu sekta ndogo ya umeme na hali ya upatikanaji wa umeme nchini. Napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyofanya jitihada kubwa ya kutafuta vyanzo vya umeme vya kila aina. Vyanzo vyote ni muhimu sana na vitasaidia katika upatikanaji wa umeme.

Mheshimiwa Spika, uchunguzi unaonesha kuwa umeme wa gesi ni rahisi sana ukilinganisha na vyanzo vingine. Hivyo, ushauri wangu kwa Serikali katika suala hili ni kuharakisha matumizi ya chanzo hiki ili kuwarahisishia maisha wananchi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, lingine ni mradi wa kuzalisha umeme wa Ruhudji. Mradi huu ni mkubwa sana ambao unazalisha MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji. Mradi utajengewa laini yenye urefu wa kilometa 170 yenye mkondo wa 400kv. Urefu wa kilometa 170 ni mrefu ambao bila ya shaka laini itapita kwenye vijiji kadha katika maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba wapitie shirika letu la TANESCO na kuweka vituo vya kupoza umeme (substations) katika maeneo yatakayopitiwa na line hii ili wananchi wa maeneo hayo yaweze kufaidika na umeme huo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.