Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Augustine Vuma Holle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kushukuru kwa kupata fursa hii ya kuchangia na kushauri machache kwenye Wizara hii ya Maliasili na Utalii. Kwanza nipende kumshukuru na kumpongeza kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro kwa ushirikiano ambao anaendelea kutupa sisi wananchi wa Kasulu, hususani Kasulu vijijini baada ya mvurugano mkubwa na TFS. Busara za Mheshimiwa Waziri zimetusaidia sana, tunamshukuru sana, sana, asiyeshukuru ni kafiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu miaka mitatu iliyopita kama sikosei miwili, kulitokea mlipuko huu wa ugonjwa wa corona yaani Covid 19. Ugonjwa ambao umefunga dunia kabisa na uliathiri sana, sana, mwenendo wa utalii duniani hata kwetu sekta ya utalii ilisinyaa sana. Sasa wakati huu ambapo tunajifunza kuishi na ugonjwa huu, nipende kwa dhati kabisa kumpongeza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi na hatua anazochukuwa kuhakikisha kwamba anafungua Taifa letu ili kuhakikisha kwamba Taifa letu wageni wanakuwa na confidence ya kuja hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu tunajua sekta ya utalii key players ni foreigner hao ndio wakubwa. Sasa kama hawana confidence na nchi yetu, sasa kama hana confidence na njia ambazo tunazitumia kuhakikisha kwamba tunafungua nchi yetu au kufanya nchi kuwa salama, hapa utalii wetu utaendelea kusinyaa, ni lazima tukubali. Dunia imekubali kwamba namna ya kuweza kufungua dunia tena na shughuli mbalimbali za utalii ziendele ni namna ya kuwapatia watu chanjo, watu wapate chanjo ili wawe na confidence ya kusafiri kwenda sehemu mbalimbali, mtalii ajija hapa akipokelewa na mtu ambaye amepewa chanjo, naamini atakuwa na confidence kubwa zaidi kuliko kupokelewa na mtu ambaye hajapewa chanjo. Sasa katika hili kule mtaani tunasema, mama anaupiga mwingi sana katika upande huu wa kushughulikia suala la Covid-19.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina machache ya kumshauri Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro hasa kwenye utalii wa uwindaji. Kule kwangu Kasulu tuna kitalu cha uwindaji, sasa wakati wa Covid 19, utalii wa uwindaji umesinyaa sana, lakini wako wawekezaji wachache pamoja na kwamba utalii wa uwindaji ulisinyaa lakini wameendelea kuwa na sisi, vitalu vingi viko wazi kwa sababu ya Covid-19, lakini wako wachache ambao waliendelea kuwa na sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande huu, ningependa kushauri yafuatayo ili kuhakikisha kwamba utalii wa uwindaji unaendelea kuwa na nguvu na unaendelea kutuletea mchango kwenye sekta ya utalii. Moja, ningependa tuwatie moyo wale ambao wamesimama na sisi wakati wa Covid 19. Kwa sababu ni ukweli usiopingika wengi wao wametengeneza hasara, wamelipa kodi, wamelipa kila kitu lakini watalii hawakuwa wengi kama ambavyo walivyotegemea, sasa lazima tuwape moja tuwatie joto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ningependa kwenye mnada unaokuja hawa watu tuwape holiday wasishiriki mnada, waendelee kuwa na maeneo yale yale ambayo wamekuwa nayo, ili kuhakikisha kwamba wanaweza kurudisha zile gharama ambazo wameingia hasara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa sana kwa wakati huu ambapo tunapambana na ugonjwa hili, tujitahidi sana kuwaruhusu watu walipe kwa instalment. Kama mtu umemwambia kitalu unachomuuzia ni dola 80,000, basi ufanye alipe kwa instalment ili kwamba aweze kupata nafasi pamoja na mazingira magumu ya kiuchumi ya kuweza kulipia Serikali ipate mapato.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kengele imeshagonga.

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba dakika moja tu, lipo la msingi.

NAIBU SPIKA: Kila mtu akiomba moja sitaweza, sekunde 30.

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, moja muda wa watu wa kufanya mnada urefushwe. Haya mambo ya kumpa mtu mwaka mmoja halafu utegemee aendeleze kitalu kwa kuendelea kufanya uwekezaji haiwezekani, lazima tuongeze muda wa kufanya mnada. Ukimpa mtu umpe miaka mitano, miaka angalau kumi aweze kufanya uwekezaji, aendeleze kitalu vizuri. Kwa kufanya hivyo..

NAIBU SPIKA: Muda wako sasa umekwisha.

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)