Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukurani zangu za dhati kwako kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. Hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu kwa uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwakilisha katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza kwa dhati Serikali yetu kwa namna inavyochukua jitihada kubwa ya kuboresha miundombinu katika sehemu za kitalii. Uboreshaji huu utavutia kuja kwa watalii jambo ambalo litaongezea Taifa letu kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utalii umegawanyika katika sehemu mbili; utalii wa ndani na utalii wa nje. Naipongeza Serikali kwa kuboresha utalii wa nje lakini bado utalii wa ndani haujakaa vizuri. Bado bei za kuingilia katika vituo vyetu vya kitalii ni kubwa kwa watalii na wananchi wetu. Wengi wanashindwa kutumia fursa hii ya kuona rasilimali yetu. Ushauri wangu katika suala hili kwa Serikali ni kuweka bei rafiki kwa watalii wetu wa ndani ili nao waweze kufaidi rasilimali za nchi yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyochukuwa jitihada ya upandaji wa miti. Bado juhudi hii haijafika katika kiwango cha kuridhisha. Idadi ya ongezeko la mashamba bado ni dogo. Ongezeko kutoka mashamba 23 mpaka 25 ni dogo mno. Ushauri wangu kwa Serikali ni kuongezwa kwa jitihada za makusudi ya kupanda miti ili kuboresha utalii katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.