Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii lakini pia nikupongeze kutokana na kazi kubwa na nzuri ambayo unaifanya katika Bunge hili pamoja na wasaidizi wako wote.
Mheshimiwa Spika, lakini pili nichukue nafasi hii kwa mara nyingine tena kumshukuru sana Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwa na imani na mimi lakini pamoja na kuweza kutuongoza vizuri na kutusimamia vyema katika kutekeleza majukumu yetu pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pia nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Waziri wangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa kweli ananisaidia sana katika kutekeleza majukumu yangu. Mimi na yeye tofauti yetu ni moja ndogo ya kishabiki, lakini ni mtu ambaye tunafanya naye kazi vizuri toka Mambo ya Ndani na sasa tunaendelea vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pia nishukuru sana watendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipango nikianzia na Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Makamishna wakurugenzi na wakuu wa Taasisi mbalimbali zilizopo katika Wizara ya Fedha na Mipango.
Mheshimiwa Spika, baada ya shukrani hizo naomba sasa niende moja kwa moja kwenye hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge walizungumza. Hoja ya kwanza niliomba nichangie inahusu mfuko wa pamoja wa fedha ambao Kamati ya Bunge pamoja na baadhi ya waheshimiwa Wabunge walizungumza kuonyesha concern yao ni kwamba sasa imekuwa muda mrefu sana, mfuko huu haujaanzishwa.
Mheshimiwa Spika, nataka nichukue fursa hii kupitia kwako kuwaeleza Waheshimiwa Wabunge pamoja na Kamati kwamba kimsingi suala la mfuko la pamoja wa fedha ni matakwa ya Kikatiba, na kama matakwa ya kikatiba basi utekelezaji wake ni jambo ambalo linapaswa liendelee kuzingatia misingi hiyo ya kikatiba na mpaka sasa hivi kuna hatua kadhaa ambazo zilizofanyika. Kwa sababu tayari mfuko wa pamoja wa fedha kwa maana ya Joint Finance on Committee imeshaundwa na kupiata Joint Finance on Committee kuna hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa za kuanzisha mfuko huo pamoja na fedha.
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa hatua hizo ni kwanza kwa sababu jambo lenyewe ni kubwa sana lilihitaji kufanya utafiti wa kina kuona ni jinsi gani ambapo mfuko huu utaweza kusimamiwa vizuri na uweze kuleta tija na kuwa endelevu mpaka sasa stand nyingi zimefanyika na zimekamilika, lakini pia hali kadhalika hatua ambayo imefikiwa mpaka sasa hivi iko katika hatua ya maamuzi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni hakikishe Waheshimiwa Wabunge kwamba sisi tutahakikisha tunasimamia katika hatua za mwisho zinazobakia ikiwemo kuandaa waraka kwa ajili ya kupeleka kwenye mamlaka za juu kwa ajili ya kufanya maamuzi. Mahamuzi hayo yatakapokuwa yamefikiwa basi ni imani yangu kwamba mfuko huu utaweza kuanza kufanya kazi ni jambo ambalo ni la msingi nakubaliana na Waheshimiwa Wabunge pamoja na Kamati lakini ni jambo ambalo vile vile tunalichukua kwa uzito unaostahili.
Mheshimiwa Spika, lakini katika hili baadhi ya wachangiaji walizungumzia kuhusiana na hoja ya changamoto ya VAT, nadhani Mheshimiwa Mbunge Ali King alizungumza kuhusiana na changamoto hiyo. Nataka nimhakikishie kwamba kwanza ni kweli mfuko huu ni muhimu lakini si kweli mfuko huu unaweza ukazitatua changamoto hiyo ya VAT ambayo ni mezungumzwa.
Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya mujibu wa Katiba yetu kuna kodi ambazo zimezungumzwa kuwa ni kodi za Muungano, ikiwemo Kodi ya Mapato ambayo inalipwa na watu binafsi, mashirika, pamoja na ushuru wa forodha, pamoja na ushuru wa bidhaa. VAT moja kati ya kodi za Muungano.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, nataka niwahakikishie kwamba changamoto hii na yenyewe tumeifanyia kazi kwa sababu Mheshimiwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hivi karibuni pamoja na timu yake walikuja tukafanya nao mazungumzo na kuna mambo ambayo tumekubaliana lakini kwa sababu bado bajeti haijaiwasilisha Mheshimiwa Waziri namuomba Mheshimiwa Mbunge avute subira ninauhakika Mheshimiwa Waziri, wakati ambapo atakuja kuwasilisha bajeti yake atakuja kulizungumzia na kulitoalea ufafanuzi suala hili kwa kina kabisa.
Mheshimiwa Spika, lakini jambo jingine ambalo nilitaka kulichangia ambao Waheshimiwa Wabunge wengi wamelizungumza ni juu ya hofu yao kubwa ambayo ni ya msingi kabisa walioyokuwa nayo ya juu ya riba kubwa kwenye mabanki yetu ambayo imeathiri sana uwekezaji katika nchi hii. Ni Dhahiri kabisa riba kubwa katika mabenki ya biashara inachangia sana kuzorotesha kasi ya uzalishaji katika viwanda, lakini vile vile inasababishwa kupunguza dhamira ya Serikali ya kuweza kuona ina ajiri watu wengi Zaidi kupitia katika uwekezaji mbalimbali ikiwa kwenye viwanda, ikiwa kwenye biashara na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, lakini pia inachangiwa vile vile kupunguza fursa za Serikali za kukusanya kodi. Kwa hiyo, ni hoja ambayo ni ya msingi kwa hiyo ni hatua nyingi ambazo banki ya Tanzania imechukua ambazo zimesaidia ama ziko zinalenga kuhakikisha kwamba banki zetu za biashara zinatoa riba nafuu kwa wananchi wake. Miongoni mwa hatua hizo kupitia sera yetu ya fedha imeweza kuhakikisha kwamba inaongeza ukwasi katika mabenki haya.
Mheshimiwa Spika, lakini jingine ambalo BoT imechukua hatua kuhakikisha kwamba inapunguza riba za BoT kwenda katika mabanki mengine kutoka asilimia 12 mpaka asilimia tano. Lakini hali kadhalika hatua nyingine ambazo nimezichukua kuhakikisha kwamba inapunguza viwango vya amana kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 6.
Mheshimiwa Spika, lakini kwamba hiyo haitoshi hali kadhalika BoT imeendelea kuboresha mfumo wa taarifa za wakopaji ili kuhakikisha kwamba mabenki yetu yanatambua wale ambao wakopaji ambao wako katika kiwango cha high risk. Lakini mambo mengine ambayo umechukua kama hatua za kuhakikisha kwamba kodi riba inapungua katika mabenki ili mabenki haya yaweze kukopesha kwa riba ya chini.
Mheshimiwa Spika, lakini hata hivyo bado kuna masuala ya kujiuliza juu ya jitihada zote ambazo benki yetu ya Tanzania imechukua lakini bado riba ziko juu haziridhishi. Nataka nikubaliane na Waheshimiwa Wabunge kwamba hoja hii ni hoja ya msingi na vile vile haikubaliki kwa sababu kuna mambo ambayo mabenki ya biashara yatakuwa lazima yatueleze kwamba mbali ya jitihada hizi ambazo benki ya Tanzania imechukua wenyewe wamefanya jitihada gani kuhakikishwa wanakabiliana na changamoto hii kubwa riba. Kwa sababu madhara ni makubwa yanapunguza na kudhorotesha kasi ya maendeleo katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, malengo ya Serikali ni kuhakikisha kwamba riba hizi zinashuka. Sasa hili riba nyingi katika mabanki zinatoka katika asilimia 12 kwenda juu, tunachokitaka ziwe chini ya asilimia 10. Kwa hiyo, nataka niseme kwamba katika hili lazima tukubaliane na Waheshimiwa Wabunge kwamba tutahakikisha kwamba tunafanya jitihada za ziada ili tuchukue hatua za ziada kuzisimamia hizi benki hizi za biashara ziweze kupunguza riba. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na moja katika mambo ambayo tunayachukua tutayaelekeza BoT kuhakikisha mara baada ya kikao hiki cha bajeti kuweza kukaa na wadau wote ikiwemo mabenki ya biashara ili kuzungumza nao wadau hawa kuwasikiliza waweze kujua ni jambo gani ambalo linapelekea kufanya wao washindwa kushusha riba hizi chini ya kiwango cha angalau asilimia 9 kushuka chini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge kwa kufikiria jambo hilo lakini niwahakikishie kwamba tumechukua mawazo yenu na tunaanza kuyafanyia kazi kwa mkakati huo ambao nimeueleza. Naamini kabisa tukisimamia vizuri na tukiwasikiliza tunaweza kufika hatua nzuri na malengo ya Serikali ya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata mikopo kwa riba za kiwango chenye kuridhisha yanafikiwa.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo imezungumzwa na baadhi ya Wabunge kama mapendekezo ni kupunguza rate za hati fungani kutoka asilimia 15 kuja chini ya asilimia 15. Kwanza, niseme kwamba mpangilio wa rate za hati fungani uliopo sasa hivi unategemea na miaka, ziko hati fungani ambazo rate yake inafika mpaka asilimia 7.2 zile ambazo zinachukua miaka miwili, hii asilimia 15 ni ya miaka 25.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo wazo la Waheshimiwa Wabunge tumelichukua ingawa wazo hili linahitaji kuangaliwa kwa umakini sana, kwa sababu kupunguza hati fungani ziwe za kiwango cha chini zaidi kunaweza kuathiri uchumi na kufanya hati fungani zile zikakosa soko. Kwa hiyo, kuna mambo mengi ambayo inabidi tuyaangalie kabla ya kuizingatia hoja hii ambayo Waheshimiwa Wabunge wametoa. Naamini kwamba ni wazo zuri tumelipokea na tutalifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka kuchangia ni suala la ukusanyaji wa mapato. Waheshimiwa Wabunge wengi wameshauri jinsi ya kufanya ili tuweze kukusanya mapato vizuri Zaidi. Nichukue fursa hii kuipongeza sana Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kazi nzuri ambayo imefanya mpaka sasa hivi toka Serikali ya Awamu ya Sita imeingia madarakani.
Mheshimiwa Spika, kuna takwimu ambazo zipo zinaonyesha kuwa tumepiga hatua ya kuridhisha. Kutokana na mabadiliko makubwa ambayo tumeyafanya kwa kipindi kifupi tungetarajia pengine tungetetereka katika ukusanyaji wa mapato lakini hali haikuwa hivyo. Kwa mfano, katika takwimu ambazo tumezipokea za Machi mpaka Mei hii malengo ya ukusanyaji wa mapato yameongeza kulinganisha na kipindi cha miezi ya nyuma. Kwa hiyo, hizi ni jitihada kubwa sana ambazo zimefanyika na zinahitaji kupongezwa.
Mheshimiwa Spika, haya yamefanyika kwa sababu kuna mambo ambayo TRA wamefanya. Moja, imehakikisha kwamba inaongeza weledi katika ukusanyaji wa mapato. Pili, kujenga mazingira mazuri ya biashara. Haya ndiyo malengo ambayo sisi tumeyapanga katika Serikali na mimi nawapongeza TRA kwa kuanza kuyasimamia vema mapema kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala lingine ni kuhakikisha kwamba weledi huo unapotumika unahakikisha unajenga mazingira mazuri ya walipa kodi kulipa kodi kwa hiyari badala ya kutumia ubabe. Kwa hiyo, ndiyo mambo ambayo kimsingi yamesaidia kufanya mapato yetu kukua. Nina takwimu hapa lakini kutokana na muda nisingependa kuzisoma, lakini takwimu hizi zipo wazi kupitia TRA zinapatikana kila mtu anaweza akaona jinsi ambavyo tumepiga hatua katika miezi hii mitatu toka Serikali ya Awamu ya Sita imeingia madarakani mbali ya kufanya reform za aina nyingi ambazo nimezieleza na nyingine ambazo sijazieleza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna mambo hapa Waheshimiwa Wabunge wameshauri na mimi nasema ni ya msingi. Moja, wanazungumzia kuhusu eneo hili la mifumo; ni kweli tuna changamoto ya mifumo, ni dhahiri mifumo hii inachangia katika kupunguza kasi hii ya ukusanyaji wa mapato. Kwa mfano, sasa hivi tunategemea kodi kubwa katika maeneo makubwa matatu; ushuru wa forodha kupitia bandari, walipaji wa kodi wakubwa lakini kuna eneo kubwa sana la kodi za ndani ambalo hatujafanya vizuri sana.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, eneo hili na mengine tunaweza kufanya vizuri zaidi ikiwa tutayazingatia maoni ya Waheshimiwa Wabunge ambayo kimsingi tumeshaanza kuyafanyia kazi. Moja, ni eneo la mifumo kuhakikisha inakuwa harmonized na inasomana. Nataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba tupo katika hatua za kuhakikisha kwamba tunaboresha na kuimarisha mifumo yetu pale TRA ili tuweze tuwe na mifumo ambayo itakuwa inafanya kazi vizuri ya kuweza kusimamia mapato. Hii itasaidia vilevile kupunguza rushwa kwani itasaidia kupunguza makutano baina ya walipakodi pamoja na wasimamizi wa kodi.
Mheshimiwa Spika, lingine ambalo Waheshimiwa Wabunge wamelizungumza na ni la msingi hasa inapokuja hoja ile ya block management ambayo inahitaji rasilimali watu. Kwa hiyo, niwahakikishie kwamba tuna dhamira hiyo na tunashirikiana na Idara ya Utumishi ili kupata kibali cha kuajiri watumishi wa TRA wa kutosha. Sasa hivi tuna watumishi ambao hawazidi 5,000 lakini tukipata watumishi angalau 1,000 basi tunaweza tukapiga hatua nzuri zaidi. Niwahakikishie kwamba kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali tutafanya kila linalowezekana hali itakaporuhusu tuweze kuongeza idadi ya watumishi TRA pamoja na kuimarisha mifumo yetu ili haya mafanikio ambayo tunayazungumza yaweze kuzidi mara dufu au zaidi ya mara dufu ya tunayojivunia leo hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini lingine ambalo napenda kulizungumza ni hoja hii ya PPP. Tumezungumza hapa wakati wa Mpango kwamba moja ya vipaumbele vya Serikali hii ni kuhakikisha kwamba nafasi ya private sector inachukuwa umuhimu mkubwa kushiriki kwenye uchumi wa nchi hii. Hili litafanyika kupitia utaratibu wa foreign directly investiment ama kupitia kwa utaratibu wa wawekezaji wetu wa ndani ama kupitia utaratibu wa ubia katika sekta ya umma na sekta binafsi.
Mheshimiwa Spika, kuna hatua kadhaa ambazo zimeshachukuliwa; tuna sheria nzuri lakini kuna jambo ambalo lazima tukubaliane kwamba tunatakiwa tulifanye kwa haraka, tunahitajika kuhakikisha tunaanzisha PPP center kwa haraka. Hili Waheshimiwa Wabunge tunaahidi kwamba tutalikamilisha muda si mrefu. Imani yetu tukianzisha taasisi hii itasaidia sana kuharakisha na kuwa kiunganishi muhimu kati ya wawekezaji pamoja na taasisi za umma lengo ni kuona nafasi ya miradi ya PPP inakuwa kwa haraka na inaimarishwa. Katika hili niwahakikishieni kwamba tutakwenda nalo vizuri.
Mheshimiwa Spika, lakini lingine ambalo wamelizungumza wamesema kwamba kuna haja ya kupunguza mitaji kutoka dola za Marekani milioni 20 mpaka kuwa Dola milioni 5 mpaka 10.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante, malizia tu hilo.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii, naunga mkono hoja. (Makofi)