Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Juma Hamad Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ole

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nichukue fursa hii kukupongeza sana wewe kwa kuchaguliwa kwako kuwa Naibu Spika na kumpongeza Mheshimiwa Job Ndugai kuchaguliwa kwake kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano. Nawapongeza kwa sababu Mheshimiwa Spika, Job Ndugai ali-participate sana katika kuandaa kanuni ambazo zina mawanda mapana; zinatufanya tufanye kazi zetu katika Bunge hili ndani na nje kwa urahisi zaidi. Na wewe ninakupongeza kwa sababu umekuwa dictionary wa kutekeleza kanuni hizi. Lakini baada ya hayo, najua itifaki inazingatiwa, nataka niende kumpongeza Rais wetu wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Ninampongeza kwa sababu ameingia katika record ya dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa nini, sasa hivi katika viongozi wa dunia wanawake heads of states tunao 26 na sita katika hao wanatoka Bara la Europe, watano wanatoka Afrika na mama Samia akiwa mmojawapo. Nchi ambazo zilikuwa zina viongozi wanawake katika Afrika kama ninavyosema ni watano. Tunaye kiongozi wa Namibia, Saara Kuugongelwa, tunaye kiongozi wa Ethiopia Sahle-Work Zewde, tunaye kiongozi wa Togo, Victoire Tomegah Dogbe Dogbe na tuna Garbon kiongozi wake anaitwa Rose Francine Rogombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini baada ya kutoa pongezi hizo kwa Mheshimiwa Rais sasa nataka nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Bajeti kwa hivyo, sina sababu ya kutounga mkono hoja hii. Nakupongeza sana, umeleta bajeti ambayo nataka niseme wazi, katika maisha yangu ya kuwa Bungeni, sijapata kuona bajeti ambayo imeleta mapinduzi makubwa kama bajeti ya mara hii. Nimekuwa hapa vipindi vinne, kipindi cha Mzee Mwinyi nikiwa Waziri wake na kipindi cha Mheshimiwa Magufuli na sasa hivi Mheshimiwa Samia. Lakini nataka nikuhakikishie bajeti yako ni ya aina yake. Nasema ni ya aina yake kwanini, nitakuja nitaeleza vizuri. Lakini, ili hii nchi ipate maendeleo na ihitajike kuna mambo matatu makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nchi lazima iwe na Prudent Physically and Monetary Policy, la pili nchi iwe na Budgetary Policy ambayo ni imara. Yote hayo yawe katika backet/katika kapu ambalo ni la good governance, tunayo. Tumemchagua Rais wetu juzi, kwa kishindo kikubwa tu. Kwa hiyo, tunayo good governance, kama vile hii transition ya madaraka kutoka Hayati Mheshimiwa Magufuli mpaka kuja Samia, ilikuwa ni ya salama kwa hivyo, tunayo good governance. Sasa sitazungumzia Physically Monetary Policy sasa hivi, lakini zaidi kwa sababu muda wenyewe hautoshi nitajikita kwenye Budgetary Policy. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kufanya kazi zake bila la kodi, Kodi ndiyo inayoendesha Serikali. Marekani ni nchi ambayo imeendelea lakini haiwezi kwenda bila kukusanya kodi. Katika City of New York kuna road tolls pale, kuna road toll station inatozwa kodi ya barabara na kadhalika. Kwa hivyo kodi ni muhimu na siri moja ya kukusanya kodi ni kukusanya kodi with minimum inconvenience to taxpayer. Huyu taxpayer ikusanywe kodi yake bila ya kusumbuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hizi indirect taxes zinazopita kwenye mafuta, zinazopita kwenye simu hazinipi matatizo, hizi haziumizi hata kidogo na bajeti yetu kwa kiasi kikubwa imejikuta na indirect taxes. Katika bajeti ya Mheshimiwa Waziri mara zote, mara zote, nasema tena au mara nyingi amekuwa akipunguza kodi katika Sekta ya Kilimo, Sekta ya Uvuvi, Sekta ya Madini na Sekta ya Mifugo. Hayo ni mambo yanayogusa wananchi, maana asilimia 65 ya wananchi wa nchi hii ni hao. Kwa hivyo nasema ni mkombozi mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niweze ku-refer maneno mazuri sana ya Mama yetu Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwanza twendeni Ukurasa wa, kama sikosei, Ukurasa wa 127. Ukurasa wa 127, Kifungu cha 105. Mheshimiwa Mwigulu anasema:

“Amekuwa wazi kuwa Rais wetu hataki kodi ya dhuluma. Hataki kodi ya dhuluma. Hataki kuendesha Serikali kwa Mapato ya dhuluma. Ameweka wazi kusimama imara kwenye masuala ya mapato na matumizi ya Serikali. Ameweka wazi kuwa atakuwa imara kwenye vita dhidi ya rushwa.”

Hayo ni maneno ya Mama Samia Suluhu Hassan tunataka Rais wa namna gani kama si Mama Samia?

WABUNGE FULANI: Mama Samia.

MHE. JUMA HAMAD OMARI: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tukienda ukurasa wa 136, Mheshimiwa Mwigulu ana- windup kwa kusema:

“Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais amenituma, niwahakikishie Watanzania kupitia hotuba hii kuwa, tutaendelea kujenga nchi. Ije mvua, lije jua tutaendelea kujenga nchi. Uwe usiku na mchana tutaendelea kujenga nchi. Kazi inaendelea.”

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka maneno gani ya busara kama hayo? Kwa hiyo nadhani tuna kila hali ya kumpongeza Rais wetu mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa hiyo naomba nijikite zaidi kwenye mambo haya ya budgetary policy. Nchi hii naifananisha na Nchi ya Malaysia, Malaysia ilipopata uhuru kutoka Uingereza mwaka 1957 ilikuwa ni nchi ya low income, basically nchi ile ilikuwa ya kilimo, walikuwa wanauza haya mazao ya kilimo ndipo ulikuwa uchumi wao. Akaja Mwanamapinduzi mmoja Mohamad Mahathir akaifanya Malaysia ikatoka kwenye low income ikaja kwenye middle income jambo ambalo kuwa na sisi Tanzania tumefanya hivyo. Tumetoka kwenye low income tumekuja kwenye middle income kiwango cha chini. Nani kafanya hayo? Ni Mama Samia na akishirikiana na Mheshimiwa Hayati marehemu Magufuli. Kwa hivyo tumetoka kwenye low income tumekuja kwenye middle income kipato cha chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa vigezo vya Benki ya Dunia ili u-qualify kuwa uchumi wa kati kigezo cha chini unatakiwa uwe per capital income ya dola 1,036, sisi tunakwenda zaidi. Malaysia sasa hivi hawapo tena kwenye low income, kigezo cha chini, wao wapo hawapo kwenye middle income kigezo cha juu ambao wameshafika uchumi wao per capital income ya dola 4,045. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, inachukua muda mrefu sana kutoka middle income ngazi ya chini kwenda kwenye middle income ngazi ya juu. Kwenye high income itachukua muda mrefu zaidi kwa sababu you’re talking per capital high income of 12,000 dollars ambayo hiyo siyo rahisi kufika kwa muda wa karibuni. Kwa hivyo, tutakuwa hapa kwa muda mrefu najua, lakini kwa jitihada hizi, ambazo Serikali yetu inafanya, nina hakika hatuna muda tutakwenda uchumi wa kati kigezo cha juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ninavyosema hii mimi ni bajeti yangu ya kipindi cha nne; sijapata kuona bajeti nzuri kama hii. Kwa mfano, bajeti inakwenda inapunguza kodi kwenye horticulture, wenzetu wa Kenya horticulture peke yake per annum wanapata kama two billion dollars. Sasa sisi foreign exchange yetu imeongezeka sasa hivi tunakwenda kwenye 5,000 dollars. Kwa hivyo ni dhahiri kwamba kwa sababu kuna upunguzaji wa kodi kwa vifaa vya horticulture kama vile majokofu ambayo yatajengwa Airport, nina hakika inawezekana kabisa tunaweza kuvuka dola 5,000 kwa muda mdogo sana. katika kipindi kinachokuja kidogo tu sisi tutavuka zaidi ya hiyo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa kengele ya pili imeshagonga.

MHE. JUMA HAMAD OMARI: Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kusema, tuna mengi sana lakini kwa sababu muda mdogo, namalizia kwa kusema tu, naiunga mkono bajeti hii na nawaomba Waheshimiwa Wabunge wenzangu hatuna sababu ya kutounga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)