Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango mfupi wa mdomo, napenda nisisitize juu ya uwekezaji kwenye ardhi. Inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2050 dunia itakuwa na watu wapatao bilioni 9.7. Watu wote hawa watahitaji kula, hivyo watahitaji ardhi kwa ajili ya kilimo. Nchi yetu haina umakini wa kutosha namna tunavyowapa wageni ardhi. Wawekezaji wengi wanakuja tunawauzia ardhi kwa maana kuitumia kwa shughuli za kilimo kwa miaka 33, 66 au 99.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania kihistoria haina ardhi tupu. Aidha, itakuwa inamilikiwa na familia, koo fulani au Serikali za vijiji. Mara nyingi wakija hawa wawekezaji tunazichua ardhi hizi kutoka kwa watu wanaohodhi na kuwapa wawekezaji kwa bei ndogo sana na kwa kuwa maeneo ya uwekezaji kwenye ardhi yanazidi kupungua, tusipozingatia tutakuja kujikuta ardhi imekwisha na kundi kubwa vijijini litabaki bila ardhi na hii inaweza kuwa hatari kwa usalama na usitawi wa watu na Taifa lao.
Napendekeza itungwe sheria au miongozo ya kusaidia Watanzania wabaki na ardhi yao ila itambuliwe mahali ilipo, inamilikiwa na nani na kiasi gani na inafaa kwa kilimo cha mazao gani. Mwekezaji akija tumwambie ardhi ya uwekezaji ipo mfano Kalenga ni eka kadhaa inamilikiwa na kijiji au watu binafsi. Unakaribishwa kuwekeza ila ardhi sio yako ingawa unaruhusiwa kuwekeza mfano kwa miaka 40 lakini tutamiliki kwa hisa ardhi hiyo wewe mgeni chukua asilimia 80 kwa kuwa unaleta pesa na ujuzi na kijiji au mtu binafsi wachukue asilimia 20 ya mazao au faida inayotokana na mazao hayo. Jambo hili niliona muhimu sana, litavijengea uwezo vijiji vyetu na watu wetu, itaimarisha uchumi wa vijiji na watu wake. Nimeangalia muundo wa Dubai (Dubai Land for Equity). Alichotakiwa kuwa nacho Mdubai ni ardhi tu iliyopimwa. Wawekezaji walikwenda kutoka Ulaya, Marekani na kwingineko. Iwe hivyo kwenye ardhi yetu kwa faida ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.