Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikali kwa kazi kubwa. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais mama yetu mpendwa kwa kusikia kilio cha wananchi. Nampongeza pia Waziri wa Fedha na wasaidizi wake kwa kutuletea bajeti nzuri inayokidhi mahitaji ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia natoa pongezi kwa Serikali kusikia kilio cha bodaboda, Madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji. Ushauri wangu kwanza Serikali ipange maeneo ya kutosha ya kilimo na kupunguza au kuondoa migogoro kati ya wakulima na watumiaji wengine wa ardhi (matumizi bora ya ardhi) ili kupunguza migogoro kati ya wafugaji na wakulima ambayo pia imekuwa kikwazo kati ya wafugaji na wakulima katika ustawi wa maendeleo ya sekta ya kilimo na mifugo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi tumeona makundi haya mawili kuwa na uhasama mkubwa. Mipango ya matumizi bora ya ardhi yaainishwe kwa mpango wa ramani ili kila mmoja ajue mipaka yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, masoko endelevu ya mazao; wakati tunapitisha bajeti ya Wizara ya Kilimom, Waziri alisema tunataka Bunge hili la Kumi na Mbili liwe la mapinduzi, naishauri Serikali ihakikishe inatafuta masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima wetu. Wakulima waruhusiwe kuuza nje ya nchi na masoko mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, bajeti ya Wizara ya Kilimo ya shilingi bilioni 294.1 ni ndogo sana, Serikali ijipange kwa bajeti zijazo kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo angalau ifike asilimia tano ya bajeti yote kwani kutokana na ufinyu maeneo haya huathiriwa na upungufu wa wataalum, zana za kilimo /vyombo vya usafiri na OC na kutokuwepo kwa mashamba ya kuzalisha mbegu ndani ya nchi hali ambayo pia itafanya mkulima kupata pembejeo za kilimo hususan mbegu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.