Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kwa mambo mazuri makubwa ambayo imeweza kutekeleza katika kipindi kifupi. Wametujengea madarasa 15,000 na kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tumeweza kujenga madarasa mengi kiasi hicho na wanafunzi wote wameingia kwa mkupuo wote walioshinda kuingia kidato cha kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii vile vile imepunguza pressure kwa wazazi ambapo kwa kipindi hiki huwa wanahangaika kutafuta michango. Sasa hivi Serikali imepanga wanaenda kujenga shule 1,000 za Sekondari ili kuhakikisha kwamba kila Kata ambayo haikuwa na shule ya sekondari itakuwa imejengewa shule ya sekondari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia mama ametoa shilingi bilioni 30, wanaenda kujenga shule za wasichana katika Mikoa 10. Kwa hiyo, sisi akina mama mnaotuona hapa, ambao ni wasichana wa zamani, tulisoma kwenye shule za wasichana za bweni, tukalelewa, tukalindwa, tukaepukana na mimba na ndoa za utotoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita. Pamoja na kwamba tumejenga mashule mengi, lakini kwa sasa hivi tuna upungufu mkubwa sana wa walimu na hasa katika Mkoa wa Kagera tuna upungufu mkubwa. Bila mwalimu huwezi kutoa elimu bora, mwalimu ni central katika kutoa elimu bora. Bila walimu wa hisabati na walimu wa sayansi, huwezi kuwa na watalaam ambao wanaweza kuleta hiyo tecknolojia tunayohitaji kwa ajili ya uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza kwa Serikali kwamba watoe vibali walimu waajiriwe. Ila pale ambapo Serikali itakuwa haijatoa vibali, tunao walimu wengi waliohitimu wako mitaani, tunaomba vibali vitolewe kwa Halmashauri. Wawaajiri hawa walimu kwa kutumia own source kama part time teachers, watoto wetu wakasomeshwe. Itakapotokea kwamba vibali vya ajira vimetoka, hawa watimu wapewe kipaumbele cha kupewa ajira, lakini waendelee kufundisha watoto wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu magonjwa yasiyoambukiza (noncommunicable disease) ni matatizo makubwa sana. Huko nyuma tulifikiri kwamba ni magonjwa ya matajiri, ni ya wazee, lakini sasa hivi wataalam wanatuambia, mtu yeyote yule anaweza kuugua. Hata watoto nao wameanza kuugua magonjwa kama kisukari, kansa, pumu, magonjwa ya akili, selimundu na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sasa hivi haya magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaua Watanzania kuliko hata magonjwa kama Malaria, Corona na Kipindupindu. Hata hivyo, haya yanasababishwa na mtindo wa maisha. Tumeacha kutembea, tunakaa kwenye viti kwa muda mrefu, hatufanyi mazoezi, ulaji usiofaa; tunakula chumvi zaidi, tunakula mafuta zaidi; tunakula sukari zaidi, tunakunywa pombe kuzidi, tunavuta tumbaku, tunatumia madawa ya kulevya, tuna misongo ya mawazo na vile vile hatupati usingizi wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi huko kwenye Majimbo, huyu anaanguka na pressure, huyu anakufa na kisukari, na kadhalika. Ndugu zangu, haya magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kuzuilika. Kwa hiyo, ni jukumu la kila mmoja kudhibiti haya magonjwa. Therefore, tunahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali, tuyape umuhimu. Ndiyo maana sisi kama Wabunge, baada ya kuona kwamba kuna umuhimu wa kila mtu kushiriki katika kudhibiti haya magonjwa, tumeanzisha mtandao wa Wabunge katika kudhibiti haya magonjwa yasiyoambukiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Serikali ipange bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya ili waweze kutekeleza afua mbalimbali za kudhibiti haya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile hata kwenye Wizara ya Michezo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)