Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama yetu kipenzi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuchochea maendeleo katika nchi yetu ya Tanzania. Nimesimama hapa nikiwa kama Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria nami napaswa kuzungumza yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kazi ambazo zilifanywa kwa mwaka mzima, napenda zaidi kuzungumzia taasisi ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inahusiana na masuala ya majanga ya usalama mahali pa kazi (OSHA) wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana. Pia Kamati ilibaini kwamba OSHA wana kila sababu ya kuongezewa watumishi kwa sababu watumishi walionao kwa sasa ni wachache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaangalia pia kwenye suala zima la taasisi ambazo zinashughulika na majanga mbalimbali ikiwemo Zimamoto. Kamati imebaini kuwa wenzetu hawa wa Zimamoto bado kimsingi hawajajipanga vizuri, kwa sababu hawana vitendea kazi, lakini pia maeneo mbalimbali ambayo majanga yanatokea wanashindwa kufika kwa wakati. Basi tumeona ni vizuri sana sasa tuishauri Serikali, iweze kuwezesha maeneo hayo ili mwisho wa siku haya majanga ambayo yanatokea na yamekuwa yakiwa yanaathiri sana uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla; basi yaweze kusimamiwa vizuri na kuweza kuondokana na hiyo hali ambayo kimsingi huwa inaleta hasara kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa na umeme mpaka vijijini kule, umeme wa REA umekwenda mpaka vijijini tunaishukuru sana Serikali kwa kufanya kazi nzuri namna hiyo, lakini sasa umeme huu umekwenda vijijini. Kuhusiana na masuala ya majanga mbalimbali wananchi je, wamepewa mafunzo maalum kuhusiana na masuala ya umeme? Faida zake na hasara zake incase kama hawatautumia vizuri umeme, nani ametoa maelekezo haya? Basi tumeona ni vizuri kuishauri Serikali kwamba, iweke kipaumbele kwenye kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala zima la umeme ambao umekwenda mpaka kule vijijini chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la taasisi nyingine ambayo iko ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, PSSSF. PSSSF wamefanya kazi nzuri sana, tulikwenda pale Moshi kukagua Kiwanda cha Viatu ambacho PSSSF wana asilimia 86 na Magereza wana asilimia 14 kwa maana ya ubia. Kazi wanayoifanya ni nzuri sana lakini bado kuna changamoto kubwa sana kwenye vile viatu wanavyovitengeneza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viatu wanavyovitengeneza ngozi yake ni ngumu sana. Kwa mfano kama unamnunulia mtoto kiatu, basi unaweza kukuta katika viatu pea nne ulizonunua ukanunua na hicho ambacho kinatengenezwa na kiwanda kile, ukakuta mtoto anapenda kuvaa viatu vingine lakini kile anakiacha kwa sababu kile kiatu ni kizito. Pia bei zake is not affordable kwa wananchi wa kawaida. Kwa hiyo watakaonunua vile viatu ina maana ni wale watu ambao wana uwezo. Kwa hiyo sasa tumeshauri kwamba wenzetu hawa wajipange vizuri waweze kutengeneza viatu kuendana na hali ya sasa ili waweze kupata masoko ya watu wa kada tofauti tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato ya ndani ya halmashari ni asilimia 10. Nimemsikia Mheshimiwa Mbunge mmoja amezungumza sikusudii kurudia lakini nadhani nikazie hapo hapo. Haya mapato ya ndani nia ilikuwa ni kuwasaidia makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi, lakini kwa sasa hivi tunapata mashaka huenda fedha hizi zinatumika vibaya. Kwa mfano; tumesikia maeneo mbalimbali na juzi nimeona kwenye mtandao, mdogo wangu Jokate Mwegelo pale Temeke ameingiliwa na watu ambao kimsingi katika halmashauri ile unakuta Diwani mmoja ameweza kujiwezesha mpaka milioni 300 ya mapato ya ndani ya halmashauri. Maana yake amekwenda ameunda vikundi vikundi hatimaye amekwenda kujiwezesha yeye mwenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahusiano ya vikundi vile ambavyo vimepewa fedha yaani havina mahusiano ya ukaribu na halmashauri. Vikundi vingine vipo mbali, ni nje ya halmashauri husika. Kwa hiyo, niombe CAG aende akakague katika halmashauri zote ili aweze kujiridhisha kuhusiana na hii fedha ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani. Nia ni kumwezesha mwananchi ili aweze kujikwamua kiuchumi, lakini sasa inakuwa tofauti watu wanataka kujinufaisha wao wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie suala la Madiwani. Madiwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana kwenye maeneo husika, sisi tupo hapa Bungeni muda wote wako kule na wananchi. Kwa misingi hiyo, wanatakiwa kwa hali na mali tuwatetee ndani ya Bunge hili ili waweze kuongezewa posho kwa sababu kazi wanazifanya lakini pia hawana usafiri wa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine hasa wale Madiwani wa vijijini ambao kimsingi wanakuwa wanatoka kijiji fulani kwenda kijiji kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno haya machache, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. (Makofi)