Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

Hon Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kuchangia hizi hoja za Kamati tatu zilizoko mbele yetu. Nimshukuru pia Mheshimiwa Rais kwa kuiwezesha vizuri sana sekta yetu inayosimamia usalama wa raia. Ni matarajio yetu kwamba kwa uimarishaji huu basi vyombo vyetu pia vitimize wajibu wao kwa kuzingatia matarajio ya Watanzania kama yalivyoelezwa na Waheshimiwa Wabunge wengi waliochangia hoja hizi. Nikushukuru wewe binafsi kwa namna unavyoongoza mjadala huu na uvyotu-guide vizuri ili tuweze kuwawakilisha vizuri wananchi waliotuleta hapa. Mwisho nizishukuru Kamati zote tatu kwa michango mizuri zilizotoa kwenye sekta tunayoisimamia, na zaidi Wabunge waliochangia kwa kiango kikubwa kwenye maeneo ya uhamiaji na eneo la Polisi, hasa eneo la tozo lililotolewa azimio na Kamati yetu ya PAC. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu haya yaliyojitokeza Uhamiaji, hizo concerns za Kamati, za CAG na za Wabunge ni very valid, ni za msingi kabisa. Hakuna mtu ambaye anatarajia chombo kilichoaminiwa kije kifanye mambo ambayo yanakiuka kabisa maadili. Na kwa kweli hata Mheshimiwa Rais mwenyewe wakati akifunga mafunzo ya askari wetu wanaoingia Immigration alisema bayana kwamba yapo mambo ambayo lazima Wizara na Immigration tuyafanyie kazi, hasa yale yanayohusika na ubadhirifu kwenye sekta hiyo ya visa na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sisi kama Wizara tunaungana na wote kusisitiza haja ya uadilifu, uaminifu, uzingatiaji wa sheria, uepukaji wa wizi na ubadhirifu kwenye maeneo yote yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mheshimiwa Spika, Wizara (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara ya Uhamiaji) tunazingatia ipasavyo maelekezo ambayo mara kwa mara yamekuwa yakitolewa na CAG wakati wa ukaguzi na Kamati zetu hizi ambazo zinatusimamia. Mimi niwahakikishie kwamba wakati wote Wizara itashirikiana na CAG na Kamati za Bunge na Wabunge kuchukua hatua stahiki pale ambapo haja ya kufanya hivyo ipo.

Mheshimiwa Spika, sasa baada ya maelezo haya, naomba nigusie maeneo yaliyojitokeza kwa hisia kali miongoni mwa wasemaji na kwenye Ripoti ya Kamati. Nikumbushe tu kwamba hii ni Ripoti ya 2020/2021, kwa hiyo tunayoyaongea hapa sisi kwenye sekta huku kuna hatua zimeshachukuliwa.

Mheshimiwa Spika, moja ambalo nimeliona likijitokeza hasa kwenye michango ya Wabunge, inakuwa kama vile pengine kuna kutilia shaka uwezo wa Wizara na pengine taasisi yetu ya Immigration kuchukua hatua. Niwaondoe shaka Waheshimiwa Wabunge, wote tuko pamoja.

Mheshimiwa Spika, jambo moja juu ya hii habari ya visa zilizotakatishwa hizi. Baada ya uchunguzi ule Serikali ilichukua hatua, kwa sababu kulikuwa kunaonekana kuna jinai, DCI alilichunguza jambo lile kwa undani sana. Lakini uchunguzi ule haukumuwezesha kuwa na ushahidi ambao ukipelekwa mahakamani wale watuhumiwa wangeweza kutiwa hatiani.

Mheshimiwa Spika, kama alivyoshauri CAG kwenye ripoti yake, DCI pia alishauri kwamba mamlaka husika za kinidhamu zichukue hatua. Naomba nilitaarifu Bunge lako kwamba Immigration imechukua hatua dhidi ya watumishi wote 32 waliotuhumiwa kuhusika na matendo yale na hatua za kinidhamu mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, lakini kubwa, wale waliokuwa na uongozi wametolewa na wengine tumewapa siyo chini ya miaka miwili hawawezi kufikiriwa kwa uongozi wowote ule. Tumewaweka kwenye matazamio wasifanye matendo kama hayo. Hata hivyo, Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu ili yeyote atakayejitokeza kufanya mambo hayo yenye mwelekeo wa kijinai wanapelekwa mahakamani.

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la tuzo na tozo, tumesikiliza maoni ya Wajumbe na maoni ya Kamati. Ushauri wote uliotolewa tunaukubali na maazimio yale hatuna shida nayo kabisa. Isipokuwa nina mambo machache ambayo nadhani tuyatolee ufafanuzi ambayo baadhi ya Wabunge walisema kama vile sasa ule mfuko hauna usimamizi kabisa. Nilimuona Mheshimiwa Sangu akiongea kwa uchungu sana juu ya jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, niwaeleze kwa kifupi. Mfuko huu upo kwa mujibu wa Kifungu cha 66 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Nchini, Sura ya 322. Sheria ile imebainisha vyanzo vya mapato, lakini hata kwenye PGO Na. 135 aya ya pili na PGO 135 aya ya 2(b) yameainishwa mule maeneo gani yanaweza yakawa vyanzo vya mapato na mamlaka ya matumizi.

Mheshimiwa Spika, na vyanzo vya mapato kama vinavyofahamika kwa mujibu wa sheria ni adhabu za makato ya mishahara kwa watumishi wanaofanya makosa ya kinidhamu, asilimia 50 ya mauzo ya mali za kuokotwa zinazokuwa polisi, makusanyo kutoka benki, taasisi, viwanda na migodi inayopata huduma za ulinzi toka Jeshi la Polisi. Na kwa sasa tuna jumla ya vyanzo 55.

Mheshimiwa Spika, akaunti hii iko BOT, maana yake Benki Kuu, na utaratibu wa matumizi umeainishwa vizuri sana. IGP kabla ya kuanza kutumia, huandaa mpango unaouwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara, naye ana- share na Waziri. Tukishajiridhisha ngazi ya Wizara, ndiyo anapelekewa Paymaster General kwa ajili ya kuruhusu fedha zitoke zikagharamie mpango ule ambao uliridhiwa kabla. Haamki tu akapanga hizi ziende zikatumike huku. Fedha hizi zinapofika kwa matumizi, huhamishiwa kwenye akaunti ya Miscellaneous Deposit Account iliyoko chini ya Wizara ya Fedha, akaunti ambayo huwa inakaguliwa.

Mheshimiwa Spika, tunakiri kwamba kutokuwepo kwa kanuni ni udhaifu ambao tumeanza kuufanyia kazi kama Wizara na kabla ya audit ijayo tutakuwa tayari tunazo kanuni za kusimamia mfuko huu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naona muda wangu umeisha, lakini nimalizie tu kwa kusema, kulikuwa na hoja ya kutumia fedha hizi kama msingi wa kujenga kwa haraka vituo na nyumba za wafanyakazi. Hilo tumeanza kulifanyia kazi kwa kuwasiliana na Banks ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi halafu mfuko ule utumike kurejesha.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda, nashukuru kwa hayo, lakini tuko pamoja na haya yaliyoshauriwa nashukuru sana. (Makofi)