Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia machache kwenye Mapendekezo ya Mpango wetu wa Maendeleo, ambao utaenda kutafsiri mpango wetu wa bajeti wa mwaka wa fedha 2023/2024. Kutokana na ufinyu wa muda, naomba niende haraka haraka. Kwanza, nataka kupendekeza, Mpango huu, ukiuangalia na ukiusoma ni kama academic paper. Ni mpango ambao unatengeneza matarajio na tamaa tuliyokuwa nayo. Tumetohoa kutoka kwenye Mpango Mkuu ule wa Miaka Mitano ambao ni mpango wa mwisho kabisa katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya mwaka 2000 - 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba Dira ya Maendeleo inaisha 2025 na huu Mpango wetu una-overlap kwenda 2026. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na mipango ambayo tutakuwa tunajitathmini kila wakati katika kutengeneza ule mpango wa mwisho kabisa. Sasa nimesema kwamba kwa jinsi ambavyo unaonekana ni kama vile tumeorodhesha tu tunachotamani kiwepo, lakini kimsingi hauoni ule mpango ndani ya Mpango huu. Sasa napenda kupendekeza yafuatayo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kuweza kutengeneza malengo mapana zaidi, hapa malengo yapo matano tu na ukiangalia yote ni macro-economic objectives. Kwa hiyo, tumefinya mpango huu kwenye kutaka ku-achieve only macro-economic objectives na wakati mpango mpana ule tumesema tupate competitive and industrial economy for human development. Kwa hiyo tuna mambo matatu pale, tuna competitiveness, industrial growth, lakini pia kuna human development.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitegemea kwenye malengo makuu yajigawe katika maeneo yote matatu lakini ukiangalia pia imejifinya kabisa, ni maeneo matano tu ya ukuaji wa uchumi, Pato la Taifa, tax effort, tax to GDP ratio, imejifunga kwenye maeneo matano tu. Kwa hiyo, naomba tupanue twende kwenye maeneo mengine ambayo yanagusa wananchi. Kwa mfano, tunafahamu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imekuwa referred humu kama moja ya reference documents. Inasema ni lazima tutoe ajira kwa vijana kufikia milioni nane mwaka 2025, lakini kwenye mpango huu huoni mwaka huu kwamba tutatengeneza ajira ngapi? Sasa hivi itatuonyesha tu jinsi ambavyo Serikali kuu itaajiri, sijui vibali vya ajira 32,000, sijui na nini, lakini haifanyi mirroring kwenye Mpango Mkuu wa Miaka Mitano, tukijikita kwenye maeneo yale ambayo tumejiwekea sisi kama Taifa kama malengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo napenda kabisa kwenye Mpango huu tuonyeshe waziwazi, kwa mwaka huu tutatengeneza ajira ngapi za vijana wetu? Mwakani tukifika, ajira ngapi? Kufika 2025 twende tumesema kwamba okay, hizi indicators ni measurable, tumeweza kuzi-achieve na kwa kweli tumetekeleza wajibu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, tumesema tunataka tutanue wigo wa kodi, lakini ukisoma document huoni kwamba tutatoka kwenye tax GDP ratio ya 11.7 kwenda 12 kwa kutumia njia zipi? Je, kutakuwa na mfumo mpya wa kodi? Pili, tutatengeneza compliance mpya ya kikodi? Tatu, tutatengeneza mazingira rahisi zaidi ya kikodi? Nne, existing taxpayers watatengenezewa utaratibu wa kulipa vizuri zaidi, tutaenda kwenye TRAB na TRAT kule kwenda ku - resolve zile disputes nje ya mahakama au tutaenda kutengeneza taxpayers wapya ambayo ni walipakodi binafsi kama personal income taxpayers au corporates, tunaenda kuzalisha walipa kodi wapya kwa kutumia njia ipi, hatuoneshi moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango mpana unasema tutakuza eneo la utaalam wa watumishi wetu. Sasa hatuonyeshwi hapa ule utaalam wa watumishi wetu ambao tunalazimika kutoa vibali vya kazi kwa wafanyakazi kutoka nje ya nchi, tunaziba vipi ile gap? Tumeambiwa kwenye Mpango Mkuu hata kwenye ile preface ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, anasema kabisa pale, tutakwenda kutengeneza wataalam kwenye maeneo mbalimbali ambayo yanahitajika ku-respond to the market demand, lakini ukiangalia hapa huoni kwamba mitaala yetu itaendelea kubaki vile vile au itabadilishwa na kama itabadilishwa, itabadilishwa nini? kwa sababu mpango lazima useme, tunaenda kubadilisha nini ili sector ministry iwajibike kupitia Mpango huu. Huu Mpango ni Mpango Mama, lakini huioni hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa natamani kuona kilichoandikwa kwenye Mpango Mkuu kinatafsiriwa moja kwa moja huku. Kwa mfano, tumesema reli ya kutoka Mtwara kupitia Masasi kwenda Songea na Mbamba Bay pale Ziwa Nyasa na kuwa na branch spur kwenda pale Liganga na Mchuchuma pale Ludewa, ambayo baadaye tumesema tuta-connect pia kwenda Makambako kuingia kwenye TAZARA. Huo mpango tumeandika kwenye Mpango wa Miaka Mitano kwamba utatekelezwa under PPP program, lakini kwenye mwaka huu haijaoneshwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake ni kwamba tunasubiri miaka mitatu iliyobakia labda huko ndio tutaonyesha kama mpango. Kwa hiyo, naomba wenzetu wa Wizara ya Fedha waionyeshe hiyo kama ni mpango ambao tunaanza nao mwaka huu, tuta-attract expression of interests waweze kuja, kama tunavyofanya kwenye hizo EPC+F kwenye maeneo ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitarajia pia sekta za uzalishaji, of course, sifurahii sana kuona kwamba kwenye mchango wa Taifa wa GDP, sekta ambazo zinaongoza ni sekta ambazo, Sanaa na Utamaduni, sijui Habari, Sekta za Uzalishaji za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda zipo chini kabisa. Kwa hiyo, nafikiri mpango huu ungeweza kusema. Tuna Viwanda kwa mfano 11 vya Ubanguaji wa Korosho, vikiwemo vya pale Masasi ambavyo ni vikubwa kuliko viwanda vyote pale. Hivi viwanda havifanyi kazi na korosho sasa hivi tumesikia hata bei ya korosho ni chaos kule kwetu, bei sasa hivi imetoka shilingi 4,000 kwenda shilingi 1,400 mpaka shilingi 1,800.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mpango gani kwenye mwaka huu tuhakikishe kwamba viwanda vyote vya korosho, vya pamba, vya alizeti, vya nini, vitafanya kazi, tuna mpango upi ambao tutaonyesha humu? Ni vizuri tuonyeshe ili ikifika mwakani tunajipima kwamba kweli intervention yetu imefanya kazi. Kwa hiyo, tunakuwa na indicators ambazo kweli zinaonyesha sisi tunawajibika. La si hivyo tutajikuta tunakuwa na natural growth ambayo ilizungumzwa na Mheshimiwa Magessa asubuhi. Ule ukuaji mdogo mdogo wa asilimia 0.2 ile ni natural growth ni ukuaji wa asili. Whether umefanya kazi au hujafanya, umepanga hujapanga, utakua tu, kwa sababu watu lazima wazalishe, lazima wale lazima wanywe. Kwa hiyo, kuepuka hiyo ili tuonekane na sisi tumefanya kazi yetu vizuri, tutengeneze a planned growth ambayo tutakuwa na growth kama za wenzetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natamani sana, eneo ambalo tumeligusa na humu limezungumzwa kuboresha huduma za watumishi wa umma kwenye jamii. Tunaboreshaje? Haisemi! Nina mawazo na nikuombe kweli, hili Bunge letu lazima tufikirie, umefika wakati na hata ukiangalia ripoti za CAG, ile ya PAC na LAAC lakini pia PIC ambayo tumejadili wiki iliyopita. Tumeona kuna laxity kubwa kwenye Public Service Management. Watumishi wa umma wame-relax kabisa kwa sababu tu wana security ya kazi zao. Kumfukuza mtumishi wa umma ni shughuli kweli kweli, natamani kweli kwa sasa hivi tumefikia wakati wa teknolojia, tuwe na utaratibu wa mikataba...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, kengele ya pili hiyo.

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE:…kwa watumishi wa umma ili anayefanya vizuri tumpandishe, anayefanya vibaya aondoke, apishe nafasi kwa watu wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda kuunga mkono hoja. (Makofi)