Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, mchango wangu utajielekeza katika eneo la uwezeshaji wananchi kiuchumi, kwanza niipongeze Serikali kwa kuendelea kuratibu programu ya kuongeza ujuzi kitaifa kwa vijana ambayo imekuwa na tija kwa vijana wengi na wananufaika na fursa hizo.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa tuliyonayo ni vijana hawa wakishahitimu masomo yao, kujiajiri au kuajiriwa; natambua juhudi za Serikali kwamba baadhi ya wahitimu wamekuwa wakitafutiwa na kuunganishwa na waajiri wao lakini bado kuna vijana wengi hawajaweza kupata ajira au kuajiriwa kutokana na changamoto ya mtaji.

Mheshimiwa Spika, katika mkutano wa vijana Mwanza na Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alituarifu kuwa wataunda benki ya vijana wajasiriamali hapa nchini ili kutatua tatizo la mtaji kwa vijana, na ningeomba kuishauri Serikali; benki hiyo tunaomba izingatie vigezo na masharti vya nafasi ya vijana ambao wengi hawana dhamana ya kukopa, tunaiomba sana Serikali izingatie nafasi ya uchumi wa vijana wengi ambao hawana kazi rasmi na iweze kuwasaidia kupitia mawazo yao ya biashara, matamanio ya vijana wengi ni kuona benki hii inakuwa suluhisho la mtaji kwa vijana wengi.

Mheshimiwa Spika, sasa ningependa mtoa hoja wakati anahitimisha hoja yake atueleze mchakato wa kuunda benki ya vijana wajasiriamali umefikia wapi.