Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hoja hii. Ningependa kuchangia hoja ya Kamati ya Miundombinu, nitachangia na hoja ya Kamati ya Kilimo.
Mheshimiwa Spika, ningeomba kuzungumzia na kuchangia kwenye zoezi la uhakiki wa line za simu, sasa hivi ulimwengu ni simu, simu ni kitu kidogo lakini simu sasa hivi ni kitu kipana sana. Hizi line za simu ni watu wa aina zote tunazo hizi simu, matapeli wana hizi simu, wezi wana hizi simu, wendawazimu wana hizi simu, wasomi wana hizi simu. Kwa hiyo, simu hii Serikali isipofanya uhakiki ikafahamu kweli line zake ziko na kina nani ni hasara sana katika nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, line ambazo zimesajiliwa na Serikali mpaka sasa ni zaidi ya line milioni 60 lakini mpaka tarehe 19, Januari zilizohakikiwa, Serikali ikafahamu haswa owners wa hizo line ni 58,432,669 ambayo ni sawa na 96.2% siyo mbaya. Lakini line ambazo hazijahakikiwa mpaka leo ni line 2,307,121 sawa na 3.8%, ni vyema na ni lazima kila mtu aliye na line ya simu kama kweli ni mtu ambaye ana ile line ya simu kwa upande ambao ni wa chanya ni lazima ahakikiwe. Sasa sisi kama Kamati ya Miundombinu tuliongea sana na Wizara tukaiomba iongeze muda wa hizi line kuhakikiwa na kweli niseme ukweli Wizara kila wakati tukiongea nao wamekuwa wanaitikia kweli. Sasa Serikali imeongeza mpaka tarehe 13 Februari, 2023. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba nione tofauti kwamba mtu ambaye mpaka tarehe 13 Februari, 2023, line yake haijahakikiwa atakuwa yeye mwenyewe ana sababu zake binafsi kwa hiyo naunga mkono kwamba TCRA izime. Kwa sababu Wizara kila wakati imekuwa inaongeza muda na wamekuwa wasikivu sana Wizara ya Mheshimiwa Nnauye. Wamekuwa wasikivu sana ndani ya kamati. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa mwisho kabisa hii tarehe 13 Februari, 2023 mtu kama atakuwa hajahakiki line yake niseme kwamba yeye hiyo line yake alikuwa anaitumia labda kwa utapeli. Kwa hivyo, naunga mkono kwamba sasa tarehe 13 Februari, 2023, line zote tutasema, tutakubali kwamba zimehakikiwa, ambazo hazikuhakikiwa ni za wale ambao walikuwa wanatutapeli sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme ukweli line zimekuwa zinatumika vibaya mno mwenyewe niliyesimama hapa nikizungumza nimetapeliwa mara nyingi na akishakutapeli tu unastuka, ukimpigia humpati tena. Kwa hiyo, line hizi zilizokuwa zinatutapeli kiasi hiki sasa ni vyema zijue zimefika mwisho na baada ya taerehe 13, Serikali inasimama hao tunajua ni wale waliokuwa wanatutapeli ndiyo hawakuhakikiwa. Ninaunga mkono hoja kwamba Serikali ina haki ya kufunga baada ya tarehe 13. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja suala la Kamati ya Kilimo, suala la mbolea, naomba nizungumzie mbolea ya ruzuku. Hii mbolea ya ruzuku iliyotolewa kipindi hiki na Serikali, ambayo Serikali imelipa 50% ya ile mbolea, yaani kama mfuko wa mbolea ya urea ilikuwa ni shilingi 140,000, mwananchi anaununua ule mfuko kwa shilingi 70,000. Suala hili liliwafurahisha sana wananchi wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nikiri kwamba kitu chochote, suala lolote linapokuwa kwenye introduction stage(mwanzo) kunakuwa na changamoto nyingi sana. Kipindi hiki hii mbolea ya ruzuku imekuwa na changamoto nyingi lakini nina uhakika Wizara imejifunza itakapofika kwenye stage ya growth, stage nyingine inayokuja mwaka huu tukifika wakati, nafikiri mwaka huu huko baadae, hawa watakuwa wamejifunza sana. Nikiri kwangu kuanzia Desemba 21 mpaka Januari 21, nilipata tani 212, tulipokea tani 212, nashukuru sana Serikali. Suala lililokera ambalo ni gumu na inabidi mabadiliko yatokee, vituo vya kupokelea ile mbolea. Kwangu mfano kwenye Jimbo langu ilikuwa ni makao makuu ya Jimbo tu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kabla ya yote naishukuru Serikali kwa sababu mbolea ilifika makao makuu ya jimbo lakini wananchi wanaoishi maeneo ya milimani, wananchi wanaoishi tarafa zingine ambazo siyo Tarafa ya Ndungu ilikuwa ni kazi lakini nilikuwa nawasihi wananchi kwamba kwa sababu Serikali ndipo inapoanza sasa kutoa ruzuku kubwa kiasi hiki, ninaomba mjikusanye mje kuchukua mbolea, nilikuwa kule kule. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba tukiri kwamba hii ruzuku ni nzuri lakini ni lazima Serikali itafute njia ya kuwafanya wananchi wote kwenye maeneo mbolea ile ifike. Kwa sababu center zikiwa ziko mbali sana inakuwa kidogo ni tabu. Naomba niseme ninaunga mkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi)