Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

Hon. Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia nkatika hoja zilizowasilishwa. Kwanza ningependa kuunga mkono hoja ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo ni kamati ninaihudumu kwa kipindi hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tuliiomba na tunaendelea kuomba kama kamati kuona namna bora ya kuweza kuongeza fedha katika mashirika ambayo yanahudumiwa na Wizara hii ya Maliasili ikiwepo Shirika la TANAPA lakini pia TAWA. Kumekuwa na uongezaji wa hifadhi lakini pia kumekuwa na uongezaji wa mapori. Yote haya yanahitaji kuhudumiwa, kwa mfano leo tunavyozungumza TAWA wameongezewa mapori matano zaidi kutoka mapori 22 yamekwenda kuwa mapori 27. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapowapa mapori mengine zaidi kwa bajeti ile ile hawa watu wanakwenda kufanya kazi namna gani? Tunaona jinsi ambavyo kuna changamoto, wanyama wakali wanakwenda kuvamia watu, kuvamia mashamba ya watu, hawa watu hawana manpower ya kutosha, hawana fedha za kutosha, tunategemea hawa watu wafanye kazi kwenye mazingira gani? Niiombe sana Serikali iweze kutenga fedha ya kutosha ili hawa watu waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tunaiangalia TANAPA. Tukiangalia pia kwenye suala zima la utalii, hawa watu wanakusanya mapato, TFS halikadhalika wanakusanya mapato. Mapato yale yanapokusanywa sasa hivi yanakwenda moja kwa moja kwenye mfuko mkuu. Kutoka kwenye mfuko mkuu kurudi huku imekuwa changamoto. Niiombe Serikali itambue kwamba ukitaka kula sharti uliwe. Toa fedha upate fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapotaka kupata fedha bila kutoa fedha utapata wapi? Toeni fedha watu wafanye kazi fedha ziingie. Mheshimiwa Waziri wa Fedha tunaliomba sana hili jambo ili mfuko wako uweze kutuna zaidi wape watu fedha wanaoingiza fedha. TANAPA wanaingiza mapato, TFS wanaingiza mapato, TAWA wanaingiza mapato lakini yale yanapoingia hayarudi hawa watu waende wakafanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hapa tunapozungumza Royal Tour imelipa, wageni wanakuja chungu nzima, hawa watu wanaumiza vichwa hawa wageni watakaokuja kwenye hii high season safari hii wataenda kulala wapi? Watakwenda kulala wapi kwa sababu hawana fedha ya kuweza kuendeleza mipango mingine ya kuhakikisha wanaendelea kupokea wageni. Mpaka kuna wakati kamati tulishauri labda pengine tuliwahi sana kutangaza hii Royal Tour wakati bado Serikali hamjajiandaa. Hebu tuwe serious na haya mambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli tunataka utalii uweze kuongeza mapato katika nchi hii ni lazima tufike mahali tukubali kupoteza fedha ili tupate fedha kwa sababu tunahitaji fedha. Vinginevyo tutapiga mark time tutalaumu watendaji, tutalaumu Waziri, tutabadilisha mawaziri lakini mwisho wa siku bila fedha hii Wizara haiwezi kufanya kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niiombe Serikali, nimuombe Waziri wa Fedha aiangalie hii Wizara kwa jicho la tatu, aiangalie kwa umakini mkubwa, ahakikishe kwenye haya mashirika wanaongezewa fedha ama wanarudishiwa hata ile incentive angalau kwa 20% ili hawa watu waweze kufanya kazi. Wame-stuck, wamekwama. OC zenyewe sasa hivi zinachelewa, hawa watu wanafanyaje kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sana kwa upande wa maliasili niombe sana kwenye bajeti waongezewe bajeti. TAWA mpaka leo tangu mwaka 2018/2019/2020 wanapewa shilingi bilioni 45 pekeyake, niambie na bado mnaendelea kuwaongezea mapori. Hawa watu wanafanyaje kazi? Lazima fedha ziongezwe ili watu waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili mambo yaweze kwenda vizuri kama tunataka kutangaza utalii wetu na kufanya utalii ndiyo uwe unaongoza katika pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kwenye upande wa ardhi. Ardhi ni changamoto sana nchini kwetu, siyo siri kama utakumbuka bajeti iliyopita watu walizungumza sana kuhusiana na masuala mazima ya ardhi lakini pia waliiomba Serikali kuona namna bora ya kuongezea tume ya matumizi bora ya ardhi fedha ili waweze kupanga matumizi ya ardhi kwa sababu kupanga ndiyo kila kitu katika ardhi ya Tanzania. Tukishapanga ardhi hii tukapima vijiji vyetu sawasawa, matatizo na changamoto za ardhi zitakuwa ni story. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema na ninarudia tena labda kama matatizo ya ardhi kwenye Serikali imekuwa ni mtaji, pengine labda itakuwa ni hivyo lakini kama tunahitaji mwarobaini, ni lazima tukubali kuweka fedha katika tume ili tume hii iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliomba fedha hapa bajeti iliyopita, tuliomba shilingi bilioni 10 wakakosa wakaongezewa shilingi bilioni nne katika shilingi bilioni moja waliyokuwa wamepewa. Hiyo shilingi bilioni nne hata kwenye bajeti ya safari hii nusu mwaka haijaonekana kabisa lakini ukiuliza unaambiwa Wizara ya Fedha hawajatoa, yaani wanafanya kurushiana mpira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuelewi tatizo ni nini, tatizo ni nani, tatizo ni Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi watatuambia hapa kwamba tujue kwamba matatizo na changamoto za ardhi ni mitaji kwao, watuambie hapa kwamba sisi matatizo ya ardhi ndiyo mitaji yetu kwa hiyo mtuache ili tuendelee na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kamati tulitegemea Wizara ya Ardhi imepata mkopo nadhani mtaiona humo kwenye taarifa yetu ya kamati. Mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 345. Tukategemea katika mkopo huo japokuwa kamati tulikuwa hatujui habari ya mkopo huo wala tulikuwa hatujui nini kinaenda kufanyika, walipotuletea tukagundua katika shilingi bilioni 345, shilingi bilioni 345, vijiji vinavyokwenda kupangwa ni vijiji 250 pekeyake katika vijiji zaidi ya 9000 ambavyo vinatakiwa vipangwe, vipimwe na viwekwe katika mpango mzima wa matumizi bora ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bilioni 300, wakati tume ya upangaji wa ardhi waliomba shilingi bilioni 10 waende wakapime vijiji 600 kwa mwaka lakini leo tumepata fedha za mkopo ambazo Watanzania watakwenda kuzilipa hizi fedha, leo ndani ya miaka mitano Wizara inakwenda kupima vijiji 250 bila aibu halafu fedha nyingine zote zinapelekwa kwenye seminar wamejitengea five bilion, bilioni tano imetengwa kwa ajili ya seminar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamejitengea uratibu, yaani kwenda kuratibu kwenye hayo maeneo wanayokwenda, wametenga zaidi ya shilingi bilioni 40, zitakwenda kutumika kwa ajili ya kazi hiyo, kuna uboreshaji wa ofisi za Wizara, kuna ujenzi wa ofisi kwenye kila mkoa, mikoa 25 wameweka fedha hizi. Kuna matengenezo ya magari wameweka fedha hizi, kama Mbunge niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu mkopo huu tuombe tuupitie kwanza. Huu mkopo ndugu zangu mikopo ina maneno mengi huko nje, Mheshimiwa Rais anatembea kila kukicha asubuhi, saa sita na jioni kutafuta fedha, hizi fedha kama hazina tija kwa Watanzania, hazina tija kwa wananchi, huu mkopo utatu- cost. (Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hawa kuna taarifa ya Mheshimiwa Waziri.

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, atajibu si Waziri? (Kicheko)

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa Angelina.

T A A R I F A

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nataka kumpa taarifa tu msemaji na bahati nzuri ni mjumbe wa kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapochukua mkopo au unapoingia mkataba wowote unakuwa una lengo lake. Lengo la mkopo huu uliochukuliwa, lengo kuu ilikuwa ni kuweka miundombinu ya kujenga mifumo, kujenga uwezo wa wataalam, kununua vitendea kazi ili kazi ya upangaji na upimaji iweze kukamilika vizuri na iwe endelevu, ndiyo lengo la mkopo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hawa taarifa hiyo.

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mabula ni Mbunge wa CCM, ilani ya chama chao inasemaje ndani ya miaka mitano kupima vijiji vingapi? Lazima tunapochukua fedha tuchukue fedha kwa malengo na mipango ya nchi na Taifa kwa ujumla lakini pia fuata ilani ya chama. Inakwambia nini? Ufanye nini ndani ya miaka yako mitano? Haiwezekani hata kama mna malengo mchukue shilingi bilioni tano muende mkafanye seminar na watu wanaokwenda kuseminishwa ni hao hao wafanyakazi wa ofisini kwao ambao tayari wanajua mambo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nchi hii haina tatizo la mfumo. Leo Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya mfumo wa ILMIS. Umefanya kazi Dodoma na Dar es Salaam, niambie mpaka leo nenda pale Dodoma, ni shida na changamoto kubwa. Mfumo umeshindwa kufanya kazi. Mfumo unafanya kazi.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa, Mheshimiwa Ole Sendeka karibu.

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani mnanitoa kwenye stimu.

T A A R I F A

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge anayeongea. Nimepata habari kwamba yeye ni mjumbe wa kamati hiyo na kwa maelezo ambayo ameyasema na maelezo ambayo Mheshimiwa Waziri ameyatoa. Kama hali iko hivyo ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameeleza na fedha hizo zinakwenda katika mazingira ya aina hiyo ya kusema kujenga uwezo na posho hizo zinakwenda katika mazingira hayo, Serikali nashauri itoe maelezo kwa sababu naunga mkono hoja anayoizungumza Mheshimiwa Mbunge. Hatuwezi kuwa na matatizo ya upimaji wa maeneo halafu fedha zote zinakwenda kwenye Wizara. Maelezo yatolewe kwenye Bunge hili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hawa unaipokea hiyo taarifa?

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea taarifa yake kwa mikono miwili. Kwa sababu kama Waheshimiwa Wabunge, tutakubali huu mkopo uende ukafanye kazi ya haya ambayo wameyaandika kwenye taarifa, naomba msome taarifa ya kamati. Haya yamo na wamechanganua naomba msome taarifa ya kamati. Kama tunakwenda kukubali haya, hali ilivyo huko nje watu wanavyopiga kelele na mikopo, leo tunakwenda kukopa fedha, tunakwenda kupima vijiji 250 katika vijiji 9,000 ambavyo vimebaki havijapimwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu uhuru nchi hii imepima vijiji 2,600 peke yake. Katika vijiji 12,000 na ushee tumepima vijiji 2,600 peke yake. Halafu vipaumbele vyetu ni nini kwenye suala zima la ardhi? Vipaumbele vyetu ni kujenga ofisi za Wizara? Vipaumbele vyetu ni kulipana posho? Kutengeneza magari? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani, huu mkopo uangaliwe upya, upitiwe upya ili wakati tunakwenda mwaka 2025, vijiji vyote 9,000 vilivyobaki vipimwe, hii fedha ni nyingi itolewe shilingi bilioni 145 vijiji vipimwe, wakati Mheshimiwa Rais anakwenda kumnadi, hili nalo liwe ni sehemu ya kampeni zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)