Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niendelee kuchangia kwenye hoja ya Kamati hizi mbili, Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na Kamati ya USEMI. Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii, kwa hiyo mimi ni sehemu ya mapendekezo yaliyowekwa kule.
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nipende kushukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa ujenzi mkubwa sana wa miundo mbinu katika elimu na afya. Wote tumeshuhudia ujenzi mkubwa wa madarasa, zahanati, vituo vya afya hata hospitali. Tunasema Mama ahsante sana kwa sababu wewe unawajali Watanzania. Tatizo lililobaki ambalo ni kubwa sana ni tatizo la uhaba wa watumishi ambalo sasa linaanza kufunika na kufifisha kazi nzuri iliyofanywa na Serikali. Serikali imejenga majengo yake pale lakini kama hakuna watumishi inaonekana kwamba hatujapata thamani ya pesa iliyotumika.
Mheshimiwa Spika, daktari leo akifanya makosa wakati anatekeleza kazi zake athari utaziona pale pale Mgongwa ataugua zaidi au atafariki; lakini kwenye mfumo wa elimu kosa likitokea leo athari utakuja kuziona miaka kadhaa baadaye. Kwa hiyo ndugu zangu tunachokiona leo cha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kidato cha nne ni kwa sababu, haya matokeo yanatokana na uchache wa walimu uliokuwepo kwa miaka mingi kadhaa. Pale ambapo kuna walimu wa kutosha ufaulu uko juu na pale ambapo kuna walimu wachache ufaulu uko chini. Kwa mfano, ukiangalia taarifa za ufaulu katika kidato cha nne mwaka 2022 kwenye masomo ya Historia, Geografia, Kiswahili ambapo unakuta upungufu wa walimu ni asilimia 5, 8, 24 hata ufaulu uko juu, kwa sababu unakuta kwenye Kiswahili wameshindwa asilimia nne kwenye historia wameshindwa kama asilimia 46. Hata hivyo, lakini ukienda kwenye masomo ya sayansi na hisabati huko ndio kuna kasheshe wanafunzi wengi wanashindwa.
Mheshimiwa Spika,Physics tuna upungufu wa walimu asilimia 77 na wanafunzi wameshindwa kwa 82, mathematics wameshindwa kwa asilimia 83 kwa sababu tuna upungufu wa walimu zaidi ya asilimia 71. Lakini ndugu zangu, hebu angalia sasa hivi kwenye shule zetu za kata tumeanza kupata division one, tunapata division two, tunapata division three. Ukiona shule ambazo zimeanza kutoa matokeo mazuri kama hayo ujue kwamba kuna walimu wazuri kwenye shule hizo lakini kule ambapo hakuna walimu hali ni mbaya.
Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa najiuliza hali hii ikiendelea kwa miaka kumi na tano ijayo watoto wakaendelea ku-fail mathematics, waka-fail physics, waka-fail biology, waka-fail chemistry itakuaje? Tutawakosa wana sayansi, tunawakosa wanateknolojia ambao tunawahitaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika,Je, hawa wanafunzi ambao wamesoma kwenye hizi shule ambazo zina walimu watatu mpaka watano badala ya kuwa na walimu kumi na tano mpaka ishirini, kwa hiyo wamesomeshwa nusu nusu maisha yao yatakuaje? Huyu mtoto anapomaliza kidato cha nne utakuta wamemuandika kwamba aliyeshinda ameandika pass na aliyeshindwa ameandika fail. Huyu ambaye hakuwa na walimu ni kweli ame-fail?
Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali na wale wa Baraza la Mitihani waongeze category ya tatu, kuwe kuna pass, fail na huyu hakufundishwa; maana huyu unam-label kwamba ameshindwa miaka yake yote lakini kumbe wewe hukuweza kumpatia walimu wa kumfundisha. Kwa hiyo pamoja na kazi nzuri ambayo inafanywa ya ujenzi wa miundombinu katika afya na elimu nilikuwa na pendekeza yafuatayo: -
Mheshimiwa Spika, kwa sasa tungesimamisha kidogo mambo ya ujenzi. Najua kwamba bado tunacho kibarua cha kujenga majengo mengine kwenye afya na elimu kwa kuwa hayajatosha, lakini ili kusudi tusi-compromise ubora, tusimamishe kidogo ujenzi; tutumie hizo fedha ili Serikali itoe vibali, tuajiri watumishi kwenye afya na elimu.
Mheshimiwa Spika, najua Serikali haiwezi kuajiri walimu wote na watumishi wote wanaokosekana kwa kuwa tunao wengi waliosoma wako mitaani. Wengine tunawakuta mpaka kwenye maduka ya wahindi wanafanya kazi ili mradi wanapata kitu chochote cha kujikimu. Tuwaajiri hawa wote kwenye basis ya kujitolea. Wakiambiwa waende kujitolea wakakubali Serikali iwalipe posho kidogo kidogo; na pale itakapo tokea ajira basi hao wapate kipaumbele cha kwanza kuweza kupata hizo ajira; na tutakuwa tumeziba lile ombwe la kukosa watumishi na kukosa kutoa elimu bora au afya iliyo bora.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Sekunde thelathini malizia.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, vituo vyetu vya afya havina maji. Tumetembelea miradi mingine tumekuta kwamba wanavuna maji ya mvua. Unakuta kwenye maeneo yetu tunayo mvua lakini tunashindwa kuvuna maji lakini tunashindwa kuya-treat. Maeneo ya hospitali unakuta kuna nurse anaamka asubuhi anakwenda kwanza kuchota maji akafanye usafi halafu ndipo arudi kuja kuwahudumia watu. Maji yenyewe yanatoka kwenye visima vifupi, kwa hiyo sio safi na salama.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa napendekeza kwa Serikali, sasa hivi kila mradi wa zahanati na vituo vya afya vitakavyojengwa component mojawapo ni lazima iwe na mfumo wa maji safi na salama. Tuvune maji tutengeneze ma tank tutumie ultraviolet water disinfection tuweze ku disinfect hayo maji.
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja za Kamati zote mbili. Ahsante sana.