Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja zilizoko mezani. Nawapongeza Wenyeviti wote, nawapongeza pia Waheshimiwa Mawaziri wanao husika na Kamati zote kwa kazi nzuri wanazofanya.
Mheshimiwa Spika, mimi nitajikita kwenye upande wa walimu. Wenzangu wameongea umuhimu wa kuangalia walimu kwa sababu tumeangalia wanafunzi wanavyo-fail na wanavyofaulu. Pia tuangalie na walimu wanaotoa huduma, jinsi gani tunaweza kuboresha huduma kwa walimu ili wafanye kazi vizuri. Kwa takwimu nilizonazo sasa hivi walimu wote wa sekondari na msingi wapo 258,291 lakini sisi wote bado tunaomba Serikali iongeze. Sasa ndio unaangalia jinsi gani ambavyo walimu wengi kama walivyo wanaweza kupata huduma bora.
Mheshimiwa Spika, na hili Serikali ililiona ndio maana ikaanzisha TAC sasa mimi leo naomba nijikite kwenye TAC kwa dakika zilizobaki. Je, Serikali ilipounda TAC ilihakikisha kwamba sheria iliyounda TAC inatekelezwa kama ilivyoundwa? Kwa mfano, ningekuwa na muda ningesoma functions, yaani kazi za tume ambazo ziko 12; lakini nitasoma mbili tu kwa sababu ya muda. Mojawapo inasema hivi to appoint, promote and discipline teachers, maintain and administer the teachers’ service. Wamewapa majukumu; hii TAC kumuangalia mwalimu la kwanza wamesema kum appoint, ku promote hii kazi inafanywa?
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi nataka kusema hivi, sisi kama Kamati tulishaiomba TAMISEMI iangalie suala hili.
Mheshimiwa Spika,na mimi leo kwa kuwa ninaunga mkono taarifa nzima ya TAMISEMI naomba na mimi nitoe mapendekezo yafuatayo kuhusu hasa TAC. Kwanza kabisa ni kusema hivi Serikali iipe nafasi Sheria ya TAC ifanye kazi iliyokusudiwa. Mpaka sasa hivi kazi zilizokusudiwa hazifanyiki.
Pili, TAC ijengewe uwezo wa kifedha na rasilimali watu ili itekeleze majukumu yake ipasavyo. Tatu, Taasisi ambazo hazihusiki ziache kufanya kazi ya TAC kwa mfano Teachers Profession Board haina haja ya kuwepo, hiyo kazi yote ingefanywa na TAC. Serikali ilete muswada wa kufuta Teachers Profession Board ili majukumu yake yafanywe na TAC. Halafu pia TAC iwe na register ya walimu wote nchini ili mwalimu yeyote anayeingia darasani katika shule zote nchini awe na license ya kufundishia kutoka TAC.
Mheshimiwa Spika, pendekezo lingine, watumishi wote wanaohudumia Walimu wapelekwe TAC. Ukiangalia shughuli nyingi zinazofanywa za Walimu, wale watendaji au watumishi wako nje ya TAC. Hata hivyo ukiangalia sheria ilivyo, wako wengine ambao wanapaswa kurudi wafanyie kazi ndani ya TAC kwa sababu TAC ndio chombo ambacho kilipewa wajibu wa kuhudimia Walimu ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, labda niulizie swali moja tu, hivi kazi zinazofanywa na TAC, TAC inapaswa iwe chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia au iendelee kukaa chini ya TAMISEMI? Kwa sababu ukiangalia kwa mfano kazi yake namba (g) inasema, supervise teachers in service training programs. Halafu (h) inasema, conduct research and evaluation on matters relating to teachers service and advice the Minister accordingly. Kwa hiyo nafikiria pengine hii pia waiangalie, kule iliko TAC ibaki kule kule.
Mheshimiwa Spika, jambo la muhimu ningependa kumalizia, kuna haja tuiombe Serikali ya kuiangalia Sheria iliyoiunda TAC na kuhakikisha kwamba inafanya kazi ipasavyo ili iwahudumie hawa Walimu wengi ambao tunaomba waongezwe, wapate nafasi ya kufanya kazi bila kufikiria kwamba sijapanda daraja, sijarekebishiwa mishahara yangu.
Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, kama ingekuwa TAC ni binadamu sasa hivi angekwenda mahakamani kuishitaki Serikali kwamba sijatendewa haki kama nilivyopaswa kuwa. Mwisho naiomba TARURA iongezewe hela tunahitaji sana fedha. Ahsante sana. (Makofi)