Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru dakika tano ni chache lakini nitajitahidi kuweza kuchangia nitakachoweza. Kwanza kabisa napongeza maoni ya Kamati zote mbili na hasa Kamati yangu ya Bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajielekeza kuhusu kwenye mwenendo wa ukusanyaji wa mapato. Ni dhahiri kwamba kwa malengo ambayo wamejiwekea Serikali wanafikia asilimia 95 mpaka 96, kwa maana ya trilioni 24, mpaka 25. Lakini kiuhalisia kama tukiweza kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato kama tukiweza ku-exhaust rasilimali tulizonazo kama nchi tuna uwezo wa kukusanya hata zaidi ya trilioni 40 na kuwa sio tegemezi kwa washirika wa maendeleo tuna uwezo huo na nitaenda kubainisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia changamoto ambazo zimeainishwa kwenye taarifa yetu ambazo zinapelekea upotevu wa kodi. Mathalani tuna hizi mashine za EFD; ni kweli kabisa tafiti zikifanyika kwa kina, na mimi mwenyewe nina ushahidi na nimeshasema mara kadhaa kwenye kamati; wafanyabiashara wana hizi EFD machine lakini in real sense hawazitumii, at a time. Ukienda wanakwambia ni mboovu, wakati mwingine ukienda unamkuta mfanyakazi anakwambia bosi amefungia. Kwa hiyo hizi zote zinasababisha upotevu wa mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine tunaelezwa kwamba pamoja na kwamba walipa kodi ni wachache sana kwa Taifa letu tunaambiwa wako milioni nne, lakini kati ya hao milioni nne wanaolipa kodi ni milioni mbili tu. Sasa kama ni hao milioni mbili wanalipa tunafika hizi trilioni 24 mpaka 25. Tukiziba mianya yote ya upotevu wa fedha hata hiyoo trilioni 40 niliyosema ni chache sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo pia linapoteza haya mapato. Taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2021 imeonesha kabisa kwamba kuna malimbikizo makubwa sana ya madeni ya kodi ambayo hayakusanywi. Inaonesha mwaka 2019/2020 madeni ambayo yalikuwa hayajakusanywa ni trilioni 3.86 ilivyokuja 2020/2021 yakaongezeka kwa asilimia 96 na kufikia trilioni 7.54. Haya maseni kama yangekuwa yamekusanywa yangeweza kuongezeka sehemu kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna changamoto nyingi kubwa, tungekusanya haya mapato ya trilioni 7.5 mathalani yakaenda kwenye mfuko wa barabara ambao unahitaji trilioni 2.4 tu kuhakikisha wanaimarisha miundombinu ya barabara, kwa maana ya TANROADS na TARURA. Leo mvua zikinyesha hapapitiki, vijijini si mijini. Trioni 2.4 tu ukizichomoa kwenye hizo trilioni 7.5 ambazo CAG ameziainisha, hapa kama yangekusanywa kwa wakati hayo madeni ya kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio hilo tu yangeweza kujenga barabara ambazo kwenye utekelezaji wa mpango inaonyesha kuna barabara za zaidi ya miaka 10 ziko kwenye upembuzi yakinifu na uchambuzi zingine zimejengwa kilomita kadhaa na kutelekezwa. Tukiweza kufanya kwa uadilifu makusanyo haya tunaweza kujenga Taifa

Mheshimiwa Mwenyekiti. Lakini ukichukua trilioni mbili tu ukapeleka kwenye sekta ya afya ambapo kwa sera ya afya tunataka kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikikopa tu alichokisema Mheshimiwa Kakunda juzi milioni 100 inajenga zahanati nzuri tu katika trilioni 2 hizi uchukue milioni 800 tu upeleke kwenye zahanati utajengewa zahanati 8000. Zahanati 8000 unapeleka zahanati 7000 vijijini na zahanati 1,000 unapeleka kwenye mitaaunakuwa umetatua pakubwa sana kati ya vijiji 12,000 kulinganisha na ambayo tuko nayo sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua trilioni 1.2 ambayo inabaki ukapeleka kwenye vituo vya afya una uwezo wa kujenga vituo vya afya 2,400 katika kata 3,900 tulizonazo. Ukiangalia sasa hivi nii chache sana zimekamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nishati walikuja kwenye bajeti wakasema kwa bajeti ambayo tunawatengea sasa hivi itawachukua takribani miaka 18 kuweza kupeleka mradi wa REA kwenye vitongoji na vijiji; kwa bajeti ambayo ni ya trilioni sita tu iliyoko mbele. Ukichukua tu trilioni 3.14 kutoka kwenye hizi ambazo zimeachwa kukusanywa kwa muda wote huu tunaweza kupunguza kwa gap kubwa sana na wananchi wakapata umeme wa REA na wakakuza uchumi, wakazidisha usalama kwenye maeneo yetu na kuongeza kwenye Pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunashindwa kutekeleza haya? Kamati imeeleza vyema, kwamba TRA au Serikali ihakikishe inakuwa na mifumo thabiti ya kudhibiti upotevu wa mapato unaofanywa na Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine wafanyakazi tulionao wanahitajika 8,000 wako 6,000. Juzi Kamati ya Bajeti ilitembelea Uturuki. Kule TRA yao wana wafanyakazi 28,000. Leo tungekuwa na wafanyakazi toshelezi hapa tuka-invest kwenye rasilimaliwatu hawa watu ambao wana EFD hawazitumii, hawa watu wanaokwepa kulipa kodi ambao wako kwenye kanzidata wangeweza kulipa kodi, tuajiri walao tufike 8,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuajiri wa kudumu na wengine wa kimkataba, tufanye kama piloting tu. Hebu tuweke kuna watu wengi wamesoma mambo ya kodi tuwaajiri kwa mkataba wa miaka miwili au mitatu tuone mapato yatakusanyika mara ngapi. Tukifanya hivi tunapoteza mapato wakati tungewekeza kwenye rasilimaliwatu tungeweza kukusanya fedha nyingi na kupeleka kwenye maendeleo ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishauri sana Serikali, na niliombe hata Bunge lako hili liazimie, katika vipaumbele vyetu walau tuwezeshe TRA wawe na wafanyakazi wa kutosha, wawe na mifumo imara ya kuweza kugundua huu upotevu wa fedha. Pia tunaambiwa kuna wafanyabiashara wengine ambao bado hawajaunganishwa kwenye mfumo wa kidigitali wa kufanya marejesho ya kikodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishauri sana Serikali na niliombe hata Bunge lako hili liazimie katika vipaumbele vyetu walau tuwezeshe TRA wawe na wafanyakazi wa kutosha, wawe na mifumo imara ya kuweza kugundua huu upotevu wa fedha. Pia tunaambiwa kuna wafanyabiashara wengine ambao bado hawajaunganishwa kwenye mfumo wa kidigitali wa kufanya marejesho ya kikodi. Sasa kama ujamuunganisha ni definitely Mapato yanapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Watanzania ambao wanafikika huko chini maskini kabisa lakini unakuta wanabanwa wanalipa vikodi vidogo vidogo ndiyo tunaweza kufanya hivyo, wakati tuna mianya mikubwa tunaipoteza ambayo tungekusanya nakuweza kulisaidia Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye mfumuko wa bei kwa haraka sana. Ukiangalia mfumuko wa bei kwenye kapu la bidhaa linalotumika kupima mfumuko wa bei. Vyakula na vinywaji visivyo na kilevi vinauzika takribani asilimia 28.2, usafiri na wenyewe una asilimia 15 pale, nyumba, gesti na nini vina asilimia 14 hivyo ndiyo vimebeba uzito mkubwa. Ukiangalia Januari, 2022 na leo Januari, 2023 nilijaribu tu kupita kwenye masoko kuangalia. Mfano, mwaka 2022 maharage yalikuwa kilo shilingi 2,000 lakini leo ni shilingi 3,600 na kuna mengine mpaka shilingi 5,000 inategemea na category. Ukija kwenye mchele ulikuwa shilingi 1,500 mpaka shilingi 1,800 mpaka shilingi 2,000, leo ni shilingi 3,600 mpaka shilingi 4,000 inategemea pia na category. Ukija kwenye sembe ndiyo kabisa ime-shoot pakubwa sana. Ukienda kwenye ngano kilo 25 ilikuwa shilingi 27,000 leo ni shilingi 45,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maisha ni magumu sana, Watanzania purchase power yetu iko chini sana. Leo ukitembea mtaani ukakuta watu wana depression, wana afya ya akili, one of the reasons ni hii, hebu tujitahidi tuone ni jinsi gani tunaweza tukafanya tufanye standardizations ya bei hizi kwa Watanzania. Mtanzania wa kawaida hawezi aka- afford, mimi mwenyewe tu hapa at a time nikipewa bill naona hela nyingi sana, asikwambie mtu Mtanzania maskini wakule kijijini, anaumia sana sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua umenivumilia muda ni mchache, nakushukuru. (Makofi)