Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa sababu ya muda na umenipa mchache sana naomba niongee kwa kifupi sana.
Kwanza nashukuru kwa kupata nafasi na mimi niweze kuchangia huku na nitachangia upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 57 ya nguvu kazi ya Taifa kwa mujibu wa Integrated Labour Force Survey ya mwaka 2021 ni vijana, lakini asilimia kumi tu kati ya vijana laki nane plus wanaoingia kwenye soko la ajira ndio wanaopata ajira rasmi. Lakini pia sekta binafsi inaajiri asilimia 64.9 ya vijana wote wanaoingia kwenye soko la ajira ambao ndio nguvu kazi ya Taifa, lakini pia findings za Inter-Universal Council of East Africa inasema asilimia 61 ya vijana wanaoingia kwenye soko la ajira, they are not fit for the job, yaani they are not cooked well natumia lugha hiyo, lakini wao wanasema asilimia 61 ya vijana wa Tanzania walifanya kwa East Africa yote inaonekana hawana uwezo wa kuajirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetaja hizi takwimu kwa haraka haraka na nimezijumuisha, nataka tu tuone namna ambavyo vijana ndio msingi tunapozungumza suala la ajira. Vijana ndio centre yaani ndio msingi na ndio mhimili mkuu kwenye sekta ya ajira kwa sababu ndi nguvu kazi ya Taifa. Lakini kwa takwimu hizi tunaona kwamba sekta binafsi ndio inaajiri kwa kiwango kikubwa sana kuliko public sector. Kwa hiyo, maana yake michakato na miundombinu yote tunayoitengeneza kwa ajili ya kuhakikisha tunaijengea uwezo sekta binafsi ili iendelee kuajiri, iendelee kufanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Kamati inasema kwamba kuna fedha asilimia 79 ambazo ziko kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana zimebakishwa huko kwa sababu vijana hawana vigezo na hiyo ndio tunategemea wachukue fedha hizo waende sekta binafsi wakajiajiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wakitusikia kwenye taarifa tunasema kuna fedha asilimia 79 zimebaki na ni milioni 200 tu ndio zimepelekwa kati ya bilioni moja ambayo ilitengwa hawatuelewi kwa sababu kuna MAKISATU, vijana wanafanya ubunifu mkubwa wanatakiwa wawezeshwe halafu tunasema kuna pesa zimebaki kwa sababu hawana vigezo, hawatuelewi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitaje kwa kifupi sana na kwa sababu ya muda vigezo ambavyo tunavipeleka kwenye soko la ajira. Kigezo cha kwanza ambacho kipo kwenye soko la ajira ili kijana aajirike Tanzania anahitaji kuwa na uzoefu miaka miwili hadi 15; kigezo cha pili anatakiwa awe na elimu degree, PhD, Masters, certificate na diploma kwa uchache sana; lakini cha tatu anatakiwa awe na soft skills, lakini taarifa ya Kamati inatuambia kwamba Serikali imeweka mkakati wa kuwajengea uwezo wa hivi vigezo hawa wahitimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi shida yangu iko kwa nini Serikali itengeneze mkakati wa kuwajengea uwezo wakati tuna mfumo wa elimu ambao kila kijana ni lazima apite kwenye nchi hii? Ni kwa nini hizi soft skills, hizi soft skills ninajua ndio uwezo wa kutatua migogoro, uwezo wa kuchangamana kazini, uwezo wa ubunifu, uwezo wa kuhimili mikiki mikiki, hizo ndio soft skills, confidence, self esteem ndio hizo life skills, kwa nini zisiwe integrated kwenye mfumo wa elimu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana niliwahi kuzungumza kwa nini tusilifanye life skills liwe somo ili wasome mwanzo mwisho? Hivi takwimu zinazotuambia kwamba asilimia 61 ya wahitimu wa vyuo vikuu hawana uwezo kwa ajili ya kazi mpaka wakapate skills nyingine, kwa sababu unafikiri watafanya nini wanaposema tunakwenda kuwajengea uwezo ili waajirike? Ni kwenda kuwaambia hivi vitu, sasa hatuwezi kuwa tunazungumza vitu hivi kila siku. Kwa sababu hii taarifa ni kama wamei-copy na kui-paste, Sera ya Vijana hatuna mpaka leo tunazungumza sera za 1996 na sera ya mwaka 2007 leo miaka 16.
MWENYEKITI: Haya ahsante sana Mheshimiwa Nusrat, ahsante sana.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.