Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwanza kwa kunipa hii nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwapongeze kwanza Wenyeviti wa Kamati na Wajumbe wote wa Kamati hizi mbili Comrade Dkt. Joseph Kizito Mhagama pamoja na Dada yangu Najma Giga, wao wametuongoza vizuri sana katika Kamati ya Katiba na Sheria ikishughulikia masuala ya Muungano na Wajumbe wao wa Kamati wote wamefanya kazi kubwa na Dkt. Jasson Rweikiza, mzee wangu wa siku nyingi na mkubwa wangu, pamoja na Naibu wake Makamu Mwenyekiti Ndugu yangu Kilumbe Ng’enda kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika upande wa Kamati ya Sheria Ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikiri wazi katika Bunge lako nikifahamu kwamba Kamati hizi sasa zote kwa mujibu wa utaratibu wetu wa kanuni zetu za Bunge inawezekana Kamati hizi wengine Wajumbe wakabadilika, lakini naomba nikiri wazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kamati hizi zimetupatia ushirikiano mkubwa sana uliopitiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano lazima rekodi ziwekwe sawa, katika upande wa Kamati ya Katiba na Sheria ambayo imekuwa ikitusimamia sisi katika kipindi chote, walikutana tukiwa na hoja takribani kati ya hoja 25 za Muungano tulikuwa na hoja 18, Kamati hii mpaka sasa imesimamia takribani hoja 15 zimekamilika. (Makofi)

Kwa hiyo, nikiwa Waziri niwashukuru sana katika hoja 18 wamekamilisha hoja 15, niwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa kazi kubwa na maelekezo yao waliyotupatia. Binafsi naomba nikiri wazi Kamati hii imetupa ushirikiano wa kutosha, na mapendekezo yote yaliyotolewa sisi wajibu wetu ni kwamba tutaendelea kuyafanyia kazi kwa sababu hayo ndiyo yaliyotusaidia tumeweza kufika hapa vizuri kwa kazi kubwa waliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa upande wa Kamati ya Sheria Ndogo, nimshukuru sana Comrade Dkt. Rweikiza na timu yake wametufanyia kazi kubwa sana kutusaidia kuturekebisha katika maeneo mbalimbali na hata pale mwanzo tulikuwa na changamoto, Kamati ilibainisha katika mambo ya Kanuni ya Environmental Expert suala zima la ukataji wa rufaa. Nishukuru maelekezo yao yalitusaidia sana, mnamo tarehe 22 Julai, 2022 GN Namba 500 ilitangazwa kuwa Environmental Expert sasa ukikata rufaa ndani ya siku 14 rufaa inatoka na ndani ya siku saba aliyekata rufaa anapata majibu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo katika ajenda ya mifuko ya plastic walitupa maelekezo na naomba nikiri wazi kwamba maelekezo yale Ofisi yetu imeyafanyia kazi na hii hoja alizungumza Mheshimiwa Kilumbe Ng’enda hapa muda si mrefu katika kuchangia; ni kwamba tumekwisharekebisha kanuni kwa mujibu wa melekezo ya Kamati, na kanuni hizo muda wowote huenda mpaka Ijumaa hii zitakuwa gazetted, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amekwishakamilisha wajibu wake, jambo liko vizuri. Kwa hiyo, niishukuru sana Kamati kwa Kazi kubwa iliyofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru Bunge lako kwa hii kazi imetusaidia sana. Ahsante sana naunga mkono hoja za Kamati zote mbili. (Makofi)