Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

Hon. Dr. Joseph Kizito Mhagama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Madaba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja hii muhimu sana kwa maslahi ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, kati ya mwezi Januari, 2021 mpaka Mei, 2022 mafuta ya aina ya petroli yamepanda kwa asilimia 92; ni asilimia kubwa sana; toka shilingi 1,695 mpaka shilingi 3,200 na kitu huo ni mzigo mkubwa sana kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini katika miezi hii miwili kati ya Aprili na Mei mafuta yamepanda kwa asilimia 21. Kwa hiyo, ukiangalia katika ujumla wake gharama ya maisha kwa Watanzania imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 92 kati ya mwaka jana na sasa na gharama ya maisha kwa Watanzania kati ya mwezi Aprili na Mei imeongezeka kwa asilimia 21. Wananchi wa Madaba kwa sehemu kubwa wanasaga nafaka kwa kutumia dizeli, maisha yao yameongezeka sana gharama, lakini Watanzania wengi vijijini wanatumia diseli kwenye kilimo.

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Joseph Mhagama kuna taarifa kutoka kwa Mbunge wa Kinondoni.

T A A R I F A

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, nataka kuongeza kwenye hoja yake na nimpe taarifa kwamba gari yangu mimi nilikuwa nikijaza kwa shilingi 250,000 full tank, jana nimelipa shilingi 350,000 na hivyo aweze kuona uzito wa kupanda kwa bei hizi. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Joseph Mhagama, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante naipokea taarifa muhimu sana kwa kujenga na kunogesha hoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja yangu ni ushauri, kwa sababu maelezo mazuri yametolewa na athari za kupanda kwa bei ya mafuta kwa Watanzania zimeelezwa. Mafuta ndiyo usalama wa Taifa letu, mafuta ndio uchumi wa nchi yetu na mafuta ndio ustawi wa jamii ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika mazingira ambayo tunaendana na tunasema ni market economy, uchumi huria unapojiendesha intervention ya Serikali ni muhimu sana kwa sababu huwezi kuliacha soko huria liende kiholela. Soko huria siyo soko holela; kwa hiyo intervention ya Serikali kwenye masuala ya fiscal policy na kwenye masuala ya momentary policy ni lazima yafanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na katika mazingira hayo kwa vile umenipa dakika tano tu naomba nitoe ushauri mahsusi. Tunazo tozo ambazo ukizijumlisha, mimi ningeongea mbili tu. Kuna fuel levy na kuna excise duty kwa pamoja zinachangia shilingi 792. Hapo Mheshimiwa Waziri au Serikali iangalie namna gani tutatoka. Tunajua umuhimu wa tozo zinazohusu ujenzi wa barabara vinakwenda kwa ajili ya ujenzi wa barabara vijijini. Tunajua umuhimu wa tozo zinazotumika kujenga miradi ya maji hizo zibaki kwa sababu tunaenda kuleta maendeleo kwa wananchi. Lakini zipo tozo zingine ambazo tuweza kupunguza government expenditures tukaenda kuboresha maisha ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba tuangalie zile ambazo hazina madhara ya moja kwa moja kwenye miradi ya wananchi vijijini na badala yake tushughulike na expenditures zingine ambazo tunaziweka kwenye on hold kwa muda mrefu. Ahsante sana. (Makofi)