Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

Hon. Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili kuweza kuchangia hoja hii ya msingi zaidi iliyopo mbele yetu. Awali ya yote niseme naunga mkono hoja, lakini la pili nashukuru jitihada ambazo tayari zimeshachukuliwa na Serikali katika kuweza kuangalia jinsi ya kuweza kutatua tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, kwenye uchumi kuna tools maalum ambazo huwa zinatumika kwenye kuweza ku-regulate uchumi wa nchi. Kuna kitu kinaitwa monetary policy na kuna kitu kinaitwa fiscal policy sasa kwa interest ya muda mimi nilikuwa naomba niizungumzie hii fiscal policy kwa kifupi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Waziri Mheshimiwa January Makamba mdogo wangu big up na hii inanikumbusha sana kauli ya Mzee Kikwete anaposema kwamba big brain lazima tuweze kuzipa nafasi yake.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na wazo la tozo ile la kusema Sh.100 tunaipunguza ili kuweza kuangalia hali kidogo ya mafuta itakavyokuwa, lakini for some reasons the situation was very ballistic, kwa hiyo kukawa na interpretation tofauti. Sasa hapa kwenye fiscal policy ndio sehemu ambayo sasa Serikali inapaswa ipafanyie kazi ya msingi. Wabunge wenzangu wamezungumzia suala hapa la kwenda kukopa, lakini naomba nitoe ushauri kwa Serikali naishauri Serikali isiende kukopa kwa ajili ya kutatua tatizo hili, no. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachoomba kuwashauri Serikali ni kwamba, tozo zilizopo katika mafuta zipo takribani 23 tozo moja tu la Sh.100 ambayo ilikuwa imetolewa, najua kilikuwa kina athari na sisi bajeti yetu ni cash budget system kwamba tunakusanya halafu tunatumia na hizi tozo tayari tumeshaziweka katika mahesabu yetu kwamba tunakwenda kuzitumia. Sasa ushauri wangu kwa Serikali ni lazima tuangalie vyanzo vipya vya mapato. Nilitoa mfano hapa mwaka jana kwamba twendeni tukaangalie jinsi gani ya kuweza kuwa na kitu kinaitwa TVA License viewers wa TV wako wengi sana na ni chanzo cha mapato kinachojitegemea.

Mheshimiwa Spika, leo mama anakwenda kukopa fedha kwa ajili ya kuweza kuleta mambo ya maendeleo ndani ya nchi, tumeona mambo ya madarasa, tumeona vituo vya afya na hili vilevile tumwombe Mheshimiwa Rais kwenda kukopa? Nasema tu kwa Wabunge wenzangu, mawazo yangu ni kwamba tuangalie vyanzo vipya vya mapato. Hapa ndipo sasa Wizara ya Fedha inapaswa iangalie nini cha kuweza kufanya, ndio maana tuna kitu tunaita Wizara ya Fedha na Mipango. Hizi brain kubwa kubwa za late kina Profesa Ngowi ziko wapi. Huu ndio wakati muafaka sasa wa kuangalia kipi kinaweza kufanyika kwenye fiscal policy, pale ambapo kuna gap ya fedha tunazozitoa kwenye tozo… (Makofi)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Mpembenwe kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Matiko.

T A A R I F A

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, nataka nimpe taarifa tu mzungumzaji kwamba, hapa tunaongelea jambo la dharura kuweza ku-rescue hii situation ya mafuta, anapendekeza vyema anasema kwamba, tuangalie vyanzo vipya vya mapato ambavyo itategemea mpaka tunamaliza Bunge la Bajeti. Sasa hiyo inakuwa haina udharura wowote ule, ukipendekeza chanzo kipya cha mapato sasa hivi lazima kije hapa Bungeni tukiidhinishe na kitakuja kupitishwa kwenye Sheria ya Fedha ambayo tunaitengeneza mwaka huu. Kwa hiyo, ni jambo la dharura tunaomba ujielekeze vyema. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Twaha Mpembenwe.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, uchumi ninaouzungumza hapa ni uchumi wa hali ya juu sana, too advanced to be understood by ordinary individual. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumza kutoa tozo maana yake ni nini Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango sasa ni wakati muafaka wa kuweza kuangalia kama tuliweza kusema kwamba tumetoa Sh.100 tukawa na deficit ya shilingi bilioni 30 tunajaribu kuangalia where are we going to get that money from? Tunapoweza kujua kwamba wapi tunakwenda kuipata hiyo fedha, ndio pale tunakuja na tafsiri sasa fiscal policy inakwenda kufanya kazi na kwa tafsiri hii hii maana yake ni nini, tusiwe tunakwenda kwenda tu katika kukopa kopa, tunakwenda kukopa ndio sawa, kuna mambo ya kwenda kufanyika kwa ajili ya kukopa, lakini kuna technics za kiuchumi ambazo inabidi sasa ziweze kufanyika na the brain inayoweza kutumika ni Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, nimezungumza hapa suala vile vile la mambo ya monetary policy, hili ni suala ambalo linajitegemea tofauti, lakini Waheshimiwa Wabunge wenzangu sidhani kama tumeweza kuligusa kwa undani zaidi... (Makofi)

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Mpembenwe kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Agnes Mathew Marwa.

T A A R I F A

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, napenda kumpa taarifa mzungumzaji kwamba ni kweli suala la kukopa kwa sasa hivi kwa suala hili la dharura kwanza kukopa ni process, lakini pia ni kuhamisha tatizo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambao mzigo huo huo utarudi kwa wananchi. Ijapokuwa kukopa ni suala zuri, lakini sasa kwa sababu hili ni suala la dharura basi tuangalie jinsi tu ya kuondoa hizo tozo chefuchefu ambazo zitasaidia kwa sasa hivi kwa suala la dharura. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Agnes nadhani Mheshimiwa Mpembenwe alisema yeye haungi mkono hilo eneo la mkopo. Sasa ni kwamba unampa taarifa au unamuunga mkono kwenye hoja yake kwamba yeye hakubaliani na hoja ya kwamba nchi ikope?

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, namuunga mkono.

SPIKA: Mheshimiwa Twaha Mpembenwe.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, ndio maana huyu ni kada mzuri wa Chama cha Mapinduzi, napokea taarifa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninachotaka kusema tu ni kwamba Serikali sasa, Wizara ya Fedha na Mipango ni wakati muafaka sasa wakae kitako na kuweza kuangalia vyanzo vipi tunakwenda kuvitumia ili kuweza ku-rescue situation. Kwa tafsiri hiyo hiyo maana yake ni nini? Narudia kusema kwamba Mheshimiwa January wazo lake lilikuwa zuri sana, lakini hakuweza kueleweka, it was too advanced, probably the procedures hazikuwa za kufuatwa the way it should be lakini at the end of the day twendeni tukaondoe hizi tozo zilizopo. Tozo
23 katika suala zima la mafuta this is absolutely ridiculous. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naona kengele imegonga, naunga mkono hoja, lakini tusiende kukopa Wizara ya Fedha wakae kitako. (Makofi)