Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, sina budi kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wake wote. Nashukuru mama hakufanya kosa kwa kumchagua Waziri Masauni katika nafasi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kuzungumizia fire hydrants. Unajua hata kipindi kile nilizungumza kuhusu fire hydrant, kwa sababu zimamoto na uokozi huwa tunawalaumu kwamba wanakwenda na maji yanakuwa madogo, maji yanakwisha wakati wa kuzima moto, lakini wanapokuwa na fire hydrants watakuwa wanajua mimi nakwenda kufanya kazi yangu pale na nikiimaliza maji yamekwisha sehemu fulani mimi naweza kupata maji nikamaliza majukumu yangu. lakini hali halisi haipo hivyo, kwanza kwenye fire hydrants zote mamlaka anayemiliki ni Mamlaka ya Maji siyo Zimamoto. Sasa kwa vyovyote kitu ambacho hakipo kwenye mamlaka yako kwa kukitegemea inakuwa ni shida.

Mheshimiwa Spika, naomba Mamlaka ya Maji ikazifanyia ukarabati na ikazitafuta fire hydrants popote zilipo wakaweza kushirikiana na Zimamoto ili wawakabidhi Zimamoto kwani wao ndiyo watendaji wa shughuli ya kuzima moto. Wao wenyewe watazishughulikia na zitakuwa chini ya mamlaka yao na watajua mipaka yao wanafanya kazi nazo vipi, lakini zikibaki kwenye Mamlaka ya Maji wao kule hawana habari nazo, hawazijali, ina maana tutapiga kelele siku zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kuzungumzia na Bodi ya Parole. Bodi ya Parole kweli ni nzuri inafanya kazi na mikoa. Katika mwaka 2021/2022 walipewa shilingi 134,000,000 wakafanyia kazi lakini ni ndogo. Katika mwaka huo 2022/2023 wamepewa shilingi 324,000,000 pia ni ndogo kwa kufanyia kazi, maana yake ina-combine mikoa yote waliyokuwa nayo.

Mheshimiwa Spika, la msingi ni elimu. Parole hawajatoa elimu kwa jamii. Kwa sababu, wale wafungwa wa Parole, baadaye wanapokuwa wametumikia kule na Bodi ikakaa ikasema sasa hivi hawa watu tayari wamejitathmini, wako vizuri, wame-behave kule ndani tuwatoe, tatizo linalotokea hapo, lazima wakaulize kwenye mitaa walipokuwa, kwenye familia au kwenye jamii na ile jamii ikifuatwa haikubali. Isipokubali, haki za binadamu ziko wapi hapo? Kwa sababu mtu ameshaonekana tayari anastahiki, aweze kutoka na pia ni kuwapunguzia Magereza kuwa na msongamano wa watu Magerezani wakati tayari wale watu muda wao kwa mujibu wa Parole umemalizika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba Bodi ya Parole kutoa elimu kwa jamii na isitoshe kama Sheria ina upungufu ndani yake na watuletee hapa tuje tuirekebishe, lakini hawa wafungwa waweze kupata amani.

Mheshimiwa Spika, niseme kidogo kuhusu wimbi la wahamiaji haramu. Wahamiaji haramu kwa kweli ni matatizo, wanapita kila mikoa kwa njia za panya kuingia, inawezekana wakapita njia, inawezekana wakaja wakahamia. Ni tatizo kwa sababu, tunapowaona tunawakamata tunawapeleka Mahakamani, wanakwenda Magereza. Tunampa mzigo Magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivi sasa anao wahamiaji haramu kama 5,679 katika hao, wako mafungu matatu; wako bado wanaotumikia vifungo, wako ambao ni mahabusu na wako ambao tayari wameshamaliza vifungo vyao, lakini hawatoki. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)