Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru sana kupata nafasi ya kuweza kuchangia na mimi nataka moja kwa moja nijielekeze katika Jimbo langu la Jang’ombe maana nisije nikaja nikageuka Ngariba wa Kilwa kama msemo wa Kiswahili unavyosema. Maana Ngariba wa Kilwa aliwatahiri wenzake wote halafu yeye akajisahau, sasa mimi naanza na Jang’ombe ambapo naanza Ziwani Polisi.

Mheshimiwa Spika, pale Ziwani Polisi tuna Kituo cha Afya kile kituo cha afya, sasa hivi tumefungua maternity lakini tulipata shida moja hapa Mheshimiwa Waziri nisikilize vizuri. Tulipata shida moja ambulance ikawa hakuna lakini kuna ahadi ya mtu wa juu yako ameahidi hii ambulance. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri utakaposimama hapa useme kwamba utanifikishia hizi salamu. Pia kukashindikana generator katika maternity ile kwa sababu sheria ni lazima kwamba uwe na hiyo automatic generator, Mbunge na mwakilishi wa Jimbo hilo la Jang’ombe tumesema hivi asilimia 50 ya generator hiyo bei yake tutatoa sisi, Mheshimiwa Waziri uje unijibu kama utatuambia kwamba na wewe asilimia 50 utatuletea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Ziwani polisi kuna Bwalo lile banda la Brass Band lile pale linavuja watu ndiyo wanapofanya mikutano pale, kwa hiyo tulipokwenda kuwatembelea safari hii tulikuta kidogo hakuko vizuri Mbunge na Mwakilishi tutatoa asilimia 50 Mheshimiwa Waziri njoo uniambie na wewe utatoa ngapi ili tuweze kufanya vitu hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Masheha wangu wamenituma nitoe shukrani kwa Jeshi la Polisi, nitoe shukrani kwa jambo moja kwamba tumepelekewa Wakaguzi Wasaidizi ndiyo Maaskari Shehia, pale sasa hivi uhalifu mambo ya udhalilishaji na mambo ya madawa ya kulevya yataondoka kwa haraka kwa sababu tunafahamu Assistant Inspectors wanakuwa na maamuzi. Kwa kuwa wana maamuzi kwa maana hiyo kila kitu kitafanyika kwa haraka, kwa hiyo tunalipongeza sana Jeshi la Polisi kupitia Mkuu wake Kamanda Sirro wamefanya vizuri sana katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtemewa mate na wengi hulowa, wengi wamezungumzia masuala ya Magereza hasa msongamano. Ninazungumzia msongamano huo katika upande mmoja, kwamba tuna wageni tunawapokea tunawaweka, tunawalisha wanamaliza vifungo vyao hatuwatoi, namshukuru ndugu yangu Jumanne Sagini Naibu Waziri, tulilifuatilia hili ili liishe lakini halijamalizika kwa sababu linahusiana na Magereza, linahusiana na Uhamiaji linahusiana na Wizara ya Mambo ya Nje, wako wafungwa kutoka Ethiopia washamaliza vifungo, hawa haina haja ya kubakia hapa tukawahudumia ilitakiwa waondoke. Hili ninalisema kwa sababu mimi mwenyewe ni Mjelajela nimeacha kule nina cheo cha superintendent, sijajitangaza tu huko zamani lakini na mimi mngeniita mstaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hili nalisema kwa sababu mimi mwenyewe ni mjela jela nimeacha kule nina cheo cha super intendent, kwa hiyo sijajitangaza tu huko zamani, lakini na mimi mngeniita mstaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hili tunalielewa vizuri, huo msongamano huko unaosemwa, wengine hakuna hata haja ya kubakia ndani ya Magereza, kwa hiyo hili tunaomba lipatiwe ufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine maslahi kwa askari wa Polisi. Kilitokea kisa hapa kimoja cha yule kijana Hamza na tuliwaona askari wetu walivyokuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu. Kwa hiyo hii posho ya mazingira magumu Mama atakapotikisha hiki kichupa cha tumbaku, tunaomba awaangalie hawa askari wetu, kwa sababu pale raia wote waliingia mitini, lakini wote tumeona ile video, askari anavyomwinda mhalifu amejitolea, kwa maana hiyo, angeweza kupigwa yeye au akapiga yeye kama alivyopiga. Sasa askari wetu hawa wanafanya kazi katika mazingira magumu, kwa hiyo tunawaombea waongezewe posho ya mazingira magumu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)