Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, nianze kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kunipa miradi mingi ya pesa za UVIKO-19 kiasi cha shilingi bilioni mbili na zaidi.

Pia nimpongeze Waziri pamoja na timu yake yote kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani ni kazi inayoonekana na ni yenye tija na maslahi mapana ya nchi yetu.

Mhesimiwa Spika, kuna maboma mengi ya maabara yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi, lakini mpaka sasa maboma yale mengi yananyufa na mengine yanaweza kudondoka muda wowote, na hii ni hatarishi kwa wanafunzi wanaocheza maeneo hayo ya maboma. Kwa hiyo niiombe Serikali imalizie maboma haya ili nguvu za wananchi zisipotee bure na ndani ya Jimbo la Lushoto kuna maboma zaidi 25.

Mheshimiwa Spika, pia kuna upungufu wa walimu zaidi 1200 katika Halmashauri ya Lushoto, hivyo niiombe Serikali iweze kuajiri watumishi kada ya ualimu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo ndani ya Wilaya ya Lushoto ina shule za msingi 151 na sekondari zaidi ya 51 na katika shule zote hizi kuna upungufu wa madarasa zaidi ya vyumba 69. Sambamba na hayo kuna upungufu mkubwa wa nyumba za walimu. Kwa jimbo la Lushoto tuna mahitaji ya nyumba za walimu two in one zaidi ya nyumba 78, na hii imekuwa ni changamoto kubwa mno katika Jimbo la Lushoto.

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali itutengee pesa za kutosha katika bajeti hii ili tuweze kuwastiri walimu wetu hasa kwa wale wanaoishi vijijini wanaishi kwenye mazingira magumu mno.

Mheshimiwa Spika, pia walimu wapewe stahiki zao mapema pamoja na kupandishwa madaraja kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja mkono kwa asilimia mia moja.