Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, nianze kuipongeza Serikali ya CCM kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa katika sekta ya elimu, pia nampongeza Mheshimiwa Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazozifanya kwenye sekta ya elimu.
Mheshimiwa Spika, Serikali imejenga madarasa mengi sana nchi nzima na kwa mara ya kwanza Tanzania imebadilisha historia kwa wanafunzi wote waliofaulu kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza. Ongezeko la madarasa haya imeongeza idadi ya upungufu wa walimu. Naishauri Serikali iongeze ajira za walimu ili idadi ya madarasa iendane na idadi ya walimu.
Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine ni shule za zamani kuwa na uchakavu mkubwa, naishauri Serikali pia ifanye ukarabati wa shule hizo kongwe ili ziendane na shule mpya zilizojengwa sasa hivi. Sambamba na hilo ipo changamoto ya walimu kukosa nyumba karibu na shule wanazofundishia, niendelee kuishauri Serikali ijenge nyumba za walimu kupunguza changamoto hiyo.
Mheshimiwa Spika, niongelee kuhusu mitaala yetu ya elimu, nashauri Serikali kuwa mitaala yetu iendane na mafunzo ya ufundi iwe kuanzia darasa la kwanza kumwezesha mwanafunzi anapomaliza shule awe anaajirika na awe na uwezo wa kufanya kazi na awe anaweza kujiajiri.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.