Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

Hon. Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa kujitoa kuwatumikia Watanzania.

Pili, naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Maji kwa uzalendo wake wa kusimamia vizuri Wizara ya Maji kwa uwajibikaji uliotukuka.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kufikisha maji ya Ziwa Victoria pale Ushetu ni ya msingi sana kwa sababu utaalam umedhihirisha bayana kuwa Ushetu haina chanzo mbadala baada ya jitihada za kuchimba maji chini ya ardhi kushindikana.

Mheshimiwa Spika, suluhisho pekee la kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa Ushetu ni maji ya Ziwa Victoria kutoka bomba la KASHWASA kuanzia Kahama. Kwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maji tayari imefikisha maji ya Ziwa Victoria kupitia bomba la KASHWASA katika miji ya Ngudu - Kwimba, Muhunze - Kishapu, Kagongwa, Isaka, Nzega, Igunga na sasa maji yatafika Tinde, Shelui - Singida na Miji ya Sikonge na Urambo, hakuna sababu ya msingi ya maji ya KASHWASA kufika Ushetu ambapo kata ya kwanza kufaidi maji hayo ipo kilometa 12 tu kutoka bomba la KASHWASA ikilinganishwa na kilometa nyingi zilizojengwa kwenda maeneo yaliyotajwa.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu iundwe timu maalum ya wataalam wa ndani ikijumuisha RUWASA na KASHWASA ili ifanye tathmini na uchambuzi wa kina kuhusu mradi wa kufikisha maji Ushetu na kusanifu mradi kwa ujumla. Aidha, nashauri ujenzi wa mradi huo ufanye kwa force account kama ilivyofanyika katika miradi mingine mikubwa. Pia nashauri kama hali ya kifedha haitaruhusu kutekeleza mradi wote, ujenzi ufanywe kwa awamu ukianzia na kata iliyo karibu na Kahama.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.