Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya katika kuhakikisha Taifa hili linapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazohusiana na masuala ya afya. Pia nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Afya na timu yake yote kwa kazi nzuri wanayofanya.
Mheshimiwa Spika, magonjwa yasiyoambukiza yanashika kasi kwa ongezeko na hata idadi ya vifo. Kwa Tanzania magonjwa ya moyo yakiongoza na pili ni magonjwa ya saratani.
Mheshimiwa Spika, ongezeko la ugonjwa wa saratani kwa sasa ni zaidi ya wagonjwa wapya 40,000 kwa mwaka na kusababisha vifo takribani 30,000 kwa mwaka huku tukiwa na wagonjwa zaidi ya 73,000 ambao wapo kwenye matibabu.
Mheshimiwa Spika, wahanga wakubwa wa ugonjwa wa saratani ni wanawake, na kundi hili la wanawake wanaopata ugonjwa huu wa saratani hasa ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti wanakumbana na changamoto nyingi sana katika jamii mfano kuathirika kisaikolojia, kuathirika kiuchumi, mahitaji ya kijamii na kimwili na mapokeo kwenye jamii.
Mheshimiwa Spika, changamoto hizi na nyingine nyingi zimekuwa miongoni mwa wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu kukata tamaa na hata kutozingatia matibabu ya kitaalam ambapo wapo ambao wameishia kujaribu tiba asili, imani za kishirikina na maombi pekee.
Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali ni kuhakikisha inaongeza nguvu katika kuhakikisha kunakuwa na nguvu kubwa katika kupambana na changamoto za wanawake wanaoathirika na magonjwa ya saratani.
Mheshimiwa Spika, vilevile Wizara ije na mpango mkakati kuhakikisha tatizo hili la saratani linapewa kipaumbele ili kujenga uelewa mpana kwa jamii kuhusu haya magonjwa ya saratani kwani huku kwenye jamii hili ni tatizo kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja.