Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na nitachangia fungu 65, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majukumu ya msingi ya kuanzisha Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu. Miongoni mwa majukumu ya msingi ilikuwa ni kuandaa, kuratibu na kusimamia sera kanuni sheria na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanayohusiana na masuala ya maendeleo ya vijana, kazi ajira, watu wenye ulemavu na hifadhi ya jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu randama na document zote zinazohusiana na Ofisi hii upande wa maendeleo ya vijana wamezungumzia shughuli ambazo zinaitwa shughuli za maendeleo ya vijana ni pamoja na wiki ya vijana kitaifa, pamoja na kumbukumbu ya Baba wa Taifa lakini na Mbio za Mwenge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haitoshi kwa sababu ukiangalia Integrated Labour Force Survey Review ya mwaka 2021 utaona vijana ni asilimia 57 ya labour force ya nchi yetu. Haitoshi kuzungumza vijana kwa nusu paragraph kwa kutaja hizi ndio shughuli zao ambazo zinaitwa shughuli za maendeleo ya vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo changamoto nyingi hatuwezi kuacha kuzungumza tatizo la ajira lakini siyo kwa ujumla wake ni tatizo la ajira kwa vijana kwa sababu ndio labour force, lakini pia tatizo la ajira kwa vijana wasomi hatuwezi kuacha kuzungumza hilo. Ukiangalia rate za graduate unemployment zinakua kila mwaka na tunatengeneza bomu bila kulielezea tunalitatua vipi, hatuwezi kuzungumza jumla jumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninasikitika sana kwa sababu hawa wanaozungumza hapa ambao ndio wanaoshiriki kwenye wiki ya vijana kitaifa, wanaoshiriki katika mbio za mwenge, na wanaoshiriki katika maonesho na kujitolea na midahalo ndio Ofisi ya Waziri Mkuu inazungumza kwamba ndio shughuli za vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya sana hata hicho kimfuko cha vijana kidogo ambacho kimetengewa bilioni moja. Ilitengwa bilioni moja mwaka 2022/2023 na haijapelekwa mpaka sasa hivi imepelekwa ziro haijapelekwa hata senti moja lakini hata mwaka wa fedha uliopita ambao ndio tuna malizia sasa hivi hata the previous year bado walipelekewa milioni 200 na wakaambiwa hawana vigezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Ofisi ya Waziri Mkuu ina programu za kuwajengea uwezo vijana, uanagenzi na vitalu nyumba vinaus na wana - graduate kwa qualifications za Ofisi za Waziri. Hata hawa ambao mmewa-train wenyewe hawana vigezo kiasi kwamba hamuwapi hizo pesa. Vijana hawatuelewi kwa sababu hawatuelewi tukisema wamekosa vigezo kwa sababu wana qualify kwa qualifications ambazo tumeziweka sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hizi ambazo mmezungumza lakini kuna changamoto nyingine. Kwa mfano vijana hawana jukwaa la kukutana ambako wanazungumza mambo yao, lakini pia vijana hawana sera ambayo inaendana na mabadiliko ya sasa hivi. Mabadiliko ya sayansi na teknolojia, masuala mbalimbali ambayo yanaendelea kwa sababu sera yetu ya vijana ni ya mwaka 2007 ambayo ina miaka 16 na iko outdated.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiingiza hii taarifa kwenye tablet yako, ukiingiza taarifa zote zinazosomwa ukaandika sera ya maendeleo ya vijana uka-enter hautapata information yoyote. Huwezi kuzungumza maendeleo ya vijana usizungumze sera yao ambayo ni outdated, haiwezekani. Kwa sababu sera ndiyo inatoa muongozo na inatoa utaratibu wa namna ambavyo masuala ya vijana updated kutokana na sayansi na teknolojia na mambo yanavyoendelea, kwa sababu inawezekana nyie mnazungumza lugha nyingine na vijana wanazungumza lugha nyingine, kwa sababu hamzungumzi lugha moja sera haipo updated. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa uchache sana naomba nizungumze kuhusiana na jukwaa la vijana kukutania. Mwaka 2015 Bunge hili lilitunga Sheria namba 12 ilioitwa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa ambayo mpaka leo ni miaka nane tangu tumetunga sheria. Tumetumia rasilimali za Serikali kutunga sheria ambayo haijawahi kutekelezwa tuna kigugumizi, lakini mpaka leo imepitia mwaka moja na miezi tisa tangu Mheshimiwa Rais atoe maelezo ya mwisho alivyokutana na vijana Mkoa wa Mwanza, Mwezi wa Sita 2021. Akaiambia Wizara inayohusika na masuala ya vijana waangalie nini kinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama hiyo haitoshi, naomba nisome Sera ya Vijana ya Mwaka 1996, kwa kunukuu naomba ninukuu. Sera inaelezea sura ya 4, Ibara ndogo 4 (1)
(8) inaelezea kwamba kuwe na mtandao wa kupeana na kubadilishana habari kuhusu shughuli za maendeleo ya vijana, hiyo ni Sera ya Vijana ya Mwaka 1996. Sera ya Maendeleo ya Vijana Mwaka 2007 inatamka katika tamko la sera inasema Serikali itasimamia zoezi la kuundwa kwa baraza la vijana la Taifa na kutengeneza kanuni za usimamizi wa shughuli za baraza. Hiyo ni sera ya vijana, lakini African Youth Charter 2007 Ibara ya 11 inasema nchi wanachama watapaswa kuhakikisha ushiriki wa vijana katika Bunge na vyombo vingine vya maamuzi ipasavyo kama sheria inavyoelekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuratibu uanzishwaji au uimarishwaji wa majukwaa kwa ajili ya vijana kushiriki kufanya maamuzi ngazi ya chini kitaifa, kikanda na katika ngazi mbalimbali za kimataifa za kiutawala, lakini Katiba inayopendekezwa hii sio muhimu kwa sababu haijapitishwa; lakini pia Katiba inayopendekezwa well enough vijana walitoa mapendekezo kwamba jambo la vijana au baraza la vijana liingie kwenye katiba ya mapendekezo na yenyewe ilisema Serikali itaanzisha Baraza la Vijana la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tamko la Mheshimiwa Waziri Mkuu mwaka 2016 wakati anasoma Bajeti ya Serikali mwaka 2016/2017 alisema katika hotuba yake “ili kuimarisha dhana ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za maendeleo, Bunge la Kumi lilitunga sheria namba 12 ya Baraza la Vijana la Taifa ya Mwaka 2015, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba sasa kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo zimekamilika. Hivyo katika mwaka 2016/2017 Serikali itaendelea kuratibu uanzishwaji wa Baraza la Vijana la Taifa na kuhimiza ushiriki na ni uanzishaji na uimarishaji wa SACCOS za vijana katika halmashauri zote ili vijana waweze kushiri katika shughuli za maendeleo”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo yote kuna kigugumizi gani kwenye Serikali kuhusiana na baraza, tunaenda kwenye mikutano ya nje ya nchi, nchi za wenzetu vijana wanaowakilisha vyombo vya vijana kwenye nchi zao wanakaa. Sisi kila mwaka tunasema tupo kwenye mchakato, tupo kwenye mchakato mpaka leo tupo kwenye mchakato, walikuwa vijana kipindi hiko wameshazeeka bado hatupati. Ninajua kuna vitu ambavyo vinasabaisha kwa nini hatuleti baraza, lakini ukisoma Sheria ya Vijana ina solution kwamba chombo kitakuwa cha kisiasa? Kuna utaratibu wa kinidhamu kwamba chombo kitakuwa hakina pesa? Sheria inasema vijana wataweza kupata ruzuku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiufupi ninatamani kujua nini kinaendelea kuhusiana na Sera ya Vijana ya Taifa, Sera ya Maendeleo ya Vijana lakini pia Baraza la Vijana la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nimalizie, Mwenge wa Uhuru; kwanza ni miongoni mwa champions wa hicho kwa uzalendo na kwa ukubwa wa Mwenge wa Uhuru. Nilikuwa miongoni mwa watu waliotoa maoni kwamba mwenge uingie katika urithi wa utamaduni wa dunia usioshikika; na tunaendelea ku-champion mwenye uingie pale na tunaheshimu mno, lakini Mwenge wa Uhuru was a political instrument design to propagates brotherhood and self-reliance brotherhood philosophy. Ulikuwa ni nyezo ya kisiasa kupropagandisha falsafa ya ujamaa na kujitegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumzia Diplomasia ya Uchumi na tumesema nchi imefunguka bado tunakimbiza mwenge tena very unfortunately. Nakuomba nisome barua ambayo inatoka kwa Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara. “Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Mchango katika kufanikisha Shughuli za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023”. Nitasoma para ya pili, “kwa barua hii napenda kukujulisha kuwa unapaswa kuhamisha walimu katika shule yako kufahamu falsafa ya Mwenge wa Uhuru ili kushiriki na kuchangia fedha za kufanikisha shughuli ya Mwenge wa Uhuru 2023 kwa mchanganuo wa shilingi 50,000 kwa wakuu wa shule na 5,000 kwa waalimu wa kawaida”, sasa mwenge? Look at this! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaenda vizuri, nchi imefunguka Mama anafanya mambo makubwa wasaidizi wake wapo ambao wanamsaidia, what is this? Hii inawashushia credit, mbona sisi hatujawahi kuchangishwa hapa Bungeni hata 100 kuchangia mwenge, sijawahi kuona barua kwa sababu na sisi tuletewe Mwenge wa Uhuru, Waheshimiwa Wabunge kupitia Bunge lako changieni milioni kumi kumi tukakimbize mwenge. Mimi nafikiri sasa kama ni msingi…

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, … ni kitu cha msingi the you don’t have to do this, why are you doing this?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nusrat kuna taarifa. Mheshimiwa Naibu Waziri.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi hii. Pamoja na mchango mzuri wa Mheshimiwa Mbunge, naomba kumpa taarifa kwamba katika suala la Mwenge wa Uhuru, kwanza ni tunu ya Kitaifa ambayo mwenge ukizungumzia suala la mwenge ni falsafa. Usione kama kile chombo, falsafa inayobeba ni kuhusiana na Utanzania wetu, Utaifa wetu, uzalendo wetu, mafunzo kwa ajili ya vijana lakini zaidi ya hapo ni chombo ambacho kinapita nchi nzima kuangazia na kumulika kwa sasa kuangalia value for money katika miradi ya maendeleo ambayo fedha nyingi zinaenda kwa ajili ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini zaidi ya hapo masuala ya uadilifu yanaangaziwa na mwenge. Sasa ukisema kuhusiana na suala la michango, michango ni hiari ni uzalendo wa watu hakuna utaratibu wala kanuni zinazoelekeza watu wachangishwe fedha kupitia mwenge wa uhuru. Kwa hiyo, kama aliandika huyo Mkurugenzi ni kwa utashi wake lakini sio kwa utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria na utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini zaidi ya hapo nipende pia kutoa taarifa kuna eneo amelieleza mchango ni mzuri, lakini si vyema sana ikienda tofauti huko nje, kwamba katika fedha alizosema za vijana ile bilioni moja katika mwaka huo wa fedha tulitoa bilioni 1.8 ambayo imekwenda na sasa tayari Wizara ya Fedha imeji-commit kwamba tutapata fedha hizo awamu ya pili ya mwaka ule wa fedha kutoa ile bilioni 1 kwa ajili ya vijana hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuhusu masuala ya vijana kwa ujumla, hata bilioni tisa nyingine zilitolewa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ukuzaji ujuzi kwa ajili ya vijana. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, yupo makini na vijana wake, anajua wakati gani anawapa fedha na wakati gani anatengeneza utaratibu wa kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana sisi ni kipaumbele katika Taifa hili na Mama amesema ukichezea vijana wake basi utaweza kumuona kwenye sura zote. Mheshimiwa Rais anawaangalia vijana, nikuhakikishie Mheshimiwa Hanje hata wewe ni mmoja wa vijana ambao Mheshimiwa Rais anakuangalia kwa jicho kama kiongozi mzuri wa baadaye. Tuendeleze uzalendo wetu, tutunze Tunu zetu za Taifa na tujisimamie katika kuhakikisha kwamba Tanzania yetu tunabaki kuwa salama, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nusrat unaikubali taarifa.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, barua imeandikwa unapaswa kuchangia na kama ni uzalendo tunatakiwa tuanze sisi kwa sababu mimi mwenyewe ni mzalendo. Tuanze humu tuchange milioni 20, milioni Hamsini Hamsini. Mwenge unaenda kumwaga gongo. Kuna Kamati ya Bunge inaenda kukagua miradi, tuna CAG anakagua miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)