Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hon. Yussuf Kaiza Makame

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chake Chake

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana wananchi wa Jimbo la Chakechake kwa kuniamini kuja kuwawakilisha katika nyumba hii muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba niseme maneno ya utangulizi yafuatayo. Kwa muda mfupi niliokaa katika Bunge hili, nimegundua kwamba kuna dhambi kubwa inayofanywa ndani ya nyumba hii muhimu. Dhambi kubwa ni kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jukumu kubwa la Bunge ni kusimamia, kuishauri na kuielekeza Serikali. Bahati mbaya sana ni kwamba, walioko upande wa Chama Tawala wao wamekuwa Serikali na Wapinzani ndio wamekuwa washauri na waelekezi. Hii ni sawasawa na mkubali tu; ni sawasawa na wale wanaotoka Usukumani kusema wote ni Marais kwa sababu Rais ni Msukuma. (Makofi/Vigelegele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie; historia mara zote inatufunza, hatujifunzi historia. Isiwe shida, kila tunachowaeleza mkawa ninyi ni watu wa ku-argue tu. Yako mengi tuliyo-argue, yako mengi tuliyowaeleza mka-argue, leo mmeyafanya na kwa ufanisi mkubwa. Hiyo faida mmeipata ninyi!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi tu; nilikuwa chuoni mara moja, wanafunzi wakawa wanaandamana kuhusu masuala ya mikopo. Huyu Makonda alikuwa Mwenyekiti wangu mimi nikiwa Katibu Mkuu wa TAHIRISO, wanafunzi walikuwa wakiandamana sana, tulipokwenda kuzungumza na Serikali tukawaambia shida siyo wanafunzi kuandamana, shida ni Serikali ya CCM kutowapa mikopo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba sasa nijielekeze kwenye hotuba. Nina mambo matatu tu ya kuelekeza na naomba niyaseme kwa ufupi kwa sababu dakika zangu ni tano. Moja, ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Jeshi la Polisi; na hii nita-cite zaidi Tumbatu Zanzibar; Mpendae ambapo Jeshi la Polisi limekwenda likanyang’anya vifaa, simu na baadaye wakawakanyaga wanawake katika vifua vyao na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri, wakati anapokuja kuhitimisha hotuba yake aje atuambie kabisa ni lini ataileta ripoti ya matukio yaliyotokea Zanzibar? Kwa sababu kuna matukio makubwa ambayo ni ya ulinzi, ni ya kuweka amani na usalama wa nchi yetu. Kuna ulipuaji wa bomu katika nyumba ya Kamishna Mukadam na mengine mengi. Tunaomba Waziri akija hapa atuambie, ni lini ataleta ripoti ya matukio yote yaliyotokea Zanzibar na nani waliofanya? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, utendaji kazi wa Polisi kinyume na PGO yao inavyowaelekeza. Kwa mujibu wa Police General Order, kazi ya Polisi ni kulinda raia na mali zao, lakini si vinginevyo. Sasa hivi Polisi ni watu wa kudhalilisha raia wa Tanzania, zaidi Wapinzani. Kuna vitu vimetokea; kuna matukio kadhaa yametokea; kuuawa kwa Diwani wa Muleba, Mkoani Bukoba, kuuawa kwa Alphonce Mawazo, mtuletee ripoti na mtuletee taarifa; lakini pia kuteswa na kuwekwa watu zaidi ya saa 24 ndani ya Polisi bila kupelekwa Mahakamani, mtuambie mnatumia sheria gani? Kwa mujibu wa PGO yenu inaonesha kabisa kwamba Polisi anatakiwa kuweka…
MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, siungi mkono hoja.