Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya makadirio na mapato ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Pili napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa namna alivyoitayarisha hotuba yake kwa ufasaha na umakini mkubwa sana na kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa utulivu na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo: -

Kwanza ni uvuvi; napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Samia kwa namna inavyochukua jitihada kubwa za kuendeleza uvuvi nchini. Uvuvi ni sekta muhimu sana inayowaletea maendeleo wavuvi wetu. Uvuvi pia ni muhimu sana katika kuongeza ajira za wananchi wetu. Lakini pamoja na juhudi zote hizo za Serikali bado kunahitajika hatua kadhaa ili kuimarisha uvuvi nchini. Bado wavuvi wetu wanafanya kazi hii kwa mazoea. Vifaa wanavyotumia ni vilevile vya zamani, hivyo naiomba Serikali kuwapatia wavuvi vifaa vya kisasa ili kuwa na uhakika na kazi yao. Aidha Serikali yetu iwapatie elimu ya kisasa ili kuwa na ubora wa kazi yao.

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu kilimo; napenda kuchukua fursa hii kwa kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyojitahidi kuchukua hatua za makusudi ili kuendeleza kilimo nchini. Naiomba Serikali iendelee na juhudi hizi hasa za kuendeleza kilimo nchini kwa kuendelea kuwapatia pembejeo za kilimo ili wakulima wetu wapate kulima kwa wakati na kupata mazao mengi zaidi.

Mheshimiwa Spika, tatu ni kuhusu Muungano wa Tanzania; napenda kumponeza sana Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyochukua juhudi za makusudi za kuimarisha Muungano wetu. Hivi sasa wananchi wa sehemu mbili za Jamhuri ya Muungano wanashirikiana katika nyanja nyingi za maendeleo. Aidha, miradi na misaada inayopatikana sasa inaenda katika sehemu zote mbili za nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.