Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia machache juu ya hoja iliyoko mezani kwetu ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni Wizara kubwa sana, ni giant na ndiyo inayohudumia wananchi katika maeneo ya elimu, afya na huduma nyingine. Tunaweza kusema kwamba TAMISEMI kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba inatimiza malengo ya Serikali Kuu, kuhakikisha kwamba basi huduma zinazopaswa kutolewa kwa wananchi zinatolewa na kwa usahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuishukuru Wizara ya TAMISEMI sasa hivi ina timu nzuri; with special compliments kwa Naibu Waziri Mheshimiwa Dugange, ahsante sana. Mimi niko kwenye Kamati ya LAAC, umekuwa ukizunguka na sisi; na huyu mwingine mgeni naye alikuwa kusini this time. Kwa hiyo, tumekuwa naye beneti kwa kweli. Kwa hiyo, mambo nitakayoyasema hapa ninaongezea kwa sababu amekuwa part and parcel ya kazi yetu, kwa hiyo, anaielewa na nina uhakika atakuwa ameshapeleka taarifa hizi ambazo tunazikuta huko chini katika Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niungane na Mbunge wa Rorya kuhusu miradi hii isiyokamilika na imepewa pesa nyingi. Anapoongelea tuseme Hospital ya Wilaya ya Rorya, ukienda Kusini Magharibi huku, Hospitali ya Mlele, Hospitali ya Sumbawanga, Hospitali ya Mpanda, Hospitali zote hizi zimejengwa mwaka 2017/2018 mpaka leo majengo yametelekezwa, hakuna kazi inayofanyika, hakuna chochote. Yaani unaweza kuona ni kwa nini Serikali imepeleka fedha huko? Wameenda kujenga hospitali kwa ajili ya nani? Kwa hiyo, tunaomba hizo Hospitali zijengwe zikamilike na kama mnaona haziwezi kukamilika, basi toa pesa kidogo kidogo ili wajenge majengo matatu yatumike, waongeze mawili yatumike ili wananchi waweze kupewa huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongelee mambo ya usimamizi wa fedha hizi. Vipo vitengo mbalimbali. Ndani ya Wizara ya TAMISEMI, kuna kitengo cha usimamizi na ufuatiliaji ambacho kingeweza kufanya kazi kabla ya Bunge Kwenda. Ukija kuangalia ni kwamba, taarifa hizi kama sio CAG, basi ni Bunge limeenda. Kwenye Wizara hizi, hasa Wizara TAMISEMI kipo kitengo cha usimamizi na ufuatiliaji wa miradi na fedha za Serikali, lakini kitengo hiki hakipewi fedha. Tunaomba Wizara itoe fedha ili hawa watu watoke maofisini. Kwa mfano, this time tumekwenda nao, ni kama tumewanyanyua sisi. Tumesafiri nao, na wengine wamesafiri hata kwenye basi letu! (Makofi)

MBUNGE FULANI: Jamanii!

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Ee!

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo inaonesha waziwazi kwamba hawa watu wanataka kufanya kazi lakini hakuna pesa inayotolewa ili waweze kufuatilia kazi hizi ambazo zinapaswa kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kitu kinaitwa force account katika usimamizi. Force account iliundwa ili kupunguza gharama za utengenezaji miradi au uendeshaji miradi au ujenzi wake. Sasa hivi force account badala sasa ya kupunguza gharama, imeongeza gharama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama ule muongozo wa PPRA wa 2020 haujazuwia mkandarasi pale ambapo kuna negotiation Ukienda maeneo mengine hakuna mafundi na hili ndio, local fundi maana yake ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, linatumika vibaya, unaenda kwenye maeneo mengine hakuna mafundi kabisa. Local fundi ni yule mtu ambaye ana uwezo wa kujenga, kusimamia na kuhakikisha kwamba, mradi unafanikiwa. Sasa ukienda kwenye maeneo mengine ili mradi wamesema local, wanasema labda anatoka kwenye Kijiji, Hapana. Huyu local fundi anaweza kutoka katika Halmashauri nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika regulations za PPRA hakuna mahali ambapo mkandarasi amezuiliwa. Wakandarasi wanatakiwa wakubaliane na zile pesa ambazo zimetolewa ndani ya halmashauri. Kama mna milioni 500 mnaweza kumwambia tunajenga majengo matatu, unafanyaje? Yeye atajikoki yeye mwenyewe, akisema milioni
400 mpeni 400, akisema 350. Lakini ninachotaka kutahadharisha ni kwamba, mtu anapoharibu jengo kwa kutumia force account huwezi kubomoa, lakini kwa mkandarasi atawajibika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba tufikirie, sijasema force account haijafanya kazi vizuri, inafanya kazi vizuri katika maeneo mengine, lakini mahali pengine imeboronga, miradi ni mibaya na kuna crisis huku mbele zinakuja kwamba, kama hii miradi ni mibovu baada ya miaka 10 au 20 nyumba zote zinaanza kuporomoka kwa hiyo, tunakuwa tunafanya kazi bure katika kuhakikisha kwamba, tunajenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli, tukubaliane. Na ninaposema kumsifu Mheshimiwa Samia, mimi kwa mfano kama sisi tunaoitwa Covid-19 watu wanaweza kufikiri tunajikomba, hapana, hatujikombi. Na tunatahadharisha mitandao huko sisi hatujikombi hata kidogo, tunamsifu mama amefanya kazi na ana uwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko kazini na tunataka kuwaambia huko kwenye mitandao, we are women at work, tuko kazini, tunawakilisha Watanzania hatuwakilishi familia. Kwa hiyo, tunaposema ni lazima sisi kama wawakilishi wa nchi na tuko hapa kihalali, kama kuna mtu anatupinga tuko huko kwenye Court Room, eeh. Kwa hiyo, ni lazima tutachangia na tutasimamia miradi ya nchi na tutahakikisha tunafanya kazi inavyotakiwa, ili kuhakikisha kwamba, Watanzania wanapata huduma zinazostahili. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Women at work.

MHE. CONCHSTER L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, yes, we are women at work na tunakwenda na mama. Na alituambia wanawake mpo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mpo, alituambia tukiwa kule ametuita wanawake kwamba, asipofanya kazi vizuri hakuna mwanamke atachaguliwa katika nchi hii. Kwa hiyo, lazima tuunge kazi yake mkono kwa sababu tunaiona, hatuungi tu holelaholela, tunaunga uwezo wa mtu hata kama ni mwanaume na kama anauwezo tutamuunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine nije kwenye TEHAMA. Sasa hivi kuna TEHAMA inatumika katika kukusanya mapato, katika matumizi. Na ninachotaka kuwatahadharisha ni kwamba, ni lazima twende na dunia inavyokwenda, lakini uko wizi mkubwa sana ambao unafanyika kutokana na TEHAMA. Nashauri Serikali na kama mmeanza huu Mfumo wa TAUSI, kama mlivyosema, lazima kuweko na kitengo cha kudhibiti wataalamu ambao wanaweza kudhibiti. Kwa hiyo, tunaposomesha watoto wetu tuwasomeshe hata TEHAMA upande wa mambo ya cybercrimes na nini, ili kuwepo na Kitengo cha Cybercrime katika halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoamini, halmashauri haiwezi ikaiba au kufanya miamala iliyoeleweka kama kule TAMISEMI hamuelewi kwa sababu, TAMISEMI ndio inayo- control kila kitu. Kwa hiyo, hili jambo Mheshimiwa Waziri uende ulione kwamba, je, inakuwaje Halmashauri wana- trespass, wanaiba. Labda wanaharibu miamala huku wanachanganyachanganya miamala, huyu wa TAMISEMI amekaa wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na yeye anakuwepo kwa hiyo, na kwenyewe huko muangalie kusudi muweze kusawazisha. Muda ni mfupi…

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshikiwa Conchester muda wako umeisha.

MHE. CONCHESTER L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nashukuru. Inatosha kwa leo. (Makofi)