Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, na naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mungu lakini pia nichukue fursa hii kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa ambayo anaifanya. Singida Mjini tumepata miradi mingi na sasa tumepata hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kumshukuru Mheshimiwa Rais naomba nirejee maneno ya mwana mama aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Magreth Fursher, aliwahi kusema, naomba ninukuu; “In politics if you want something said ask a man, if you want something done ask a woman”
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa tafsiri isiyo rasmi ukitaka taarifa ya maneno muulize mwanaume lakini ukitaka tafsiri ya vitendo muulize mwanamke. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, akina mama wameumbwa kuwa watu watulivu wenye huruma lakini wanafanya kazi yao kwa vitendo sana, salamu hizi zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma vizuri document ya TAMISEMI wamejielekeza wanatekeleza kwamba majukumu yao kupitia hati idhini presidential instrument; na mimi naenda kwenye kipengele cha kwanza cha ugatuaji, wanasimamia sera ya ugatuaji, kwa maana ya D by D. Sera ya ugatuaji ilikuwa inazungumzia tuna gatua mamla kutoka Serikali Kuu kwenda Serikali za mitaa hatugatui kutoka Serikali kuu kwenda Wizara ya TAMISEMI. Kwenye sera ya ugatuaji imejielekeza hasa kwenye elimu kazi kubwa ambayo wanatakiwa wafanye kwenye eneo hili la local government ni kusimamia shule na si elimu; suala la elimu linabaki kwenye Wizara ya Elimu; na kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 imempa mamlaka Kamishina wa Elimu kusimamia elimu. Hata hivyo, nikiangalia hii document sijaona kama tunafuata Sheria ya Elimu sijaona kama tunafata Sera ya Elimu ya mwaka 2014.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hayo? Sasa hivi inakuja miongozo na mikataba mbalimbali, sasa hivi kuna mkataba mmoja unaitwa KPI, Key Performance Indicator viashiria vya ufaulu. Mkataba huu umekuwa kero kwa walimu na watumishi. Kuanzia Afisa Elimu wa Mkoa, Wilaya mpaka mwalimu wa kawaida amesainishwa huu Mkataba, na mkataba huu asipoutekeleza unasema zitachukuliwa hatua kali dhidi yake. Sasa walimu wameacha kufanya kazi sasa hivi wanandaa mpango mkakati wa kutekeleza makataba, hili jambo sio sawa. Nataka niombe Wizara ya TAMISEMI, kama tunataka kuboresha elimu tuanze na mwalimu, na kama tunataka kuwe na viasharia vya ufaulu, kiashiria namba moja ni mwalimu wala si kitu kingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwakumbushe, tulikuwa na BRN hapa ika-fail, tumekuja na Open Performance Review Appraisal (OPRAS) ika-fail, tukaja hapa na kalenda ya ufundishaji ilikaa within six months ika-fail. Sasa leo tunakuja na KPI. Kwa nini tunazunguka? Na hapa nataka nirejee maneno ya mwana taaluma Sign Harris alisema; “The whole purpose of education is to turn mirrors into windows.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa tafsiri nyepesi sana, madhumuni makuu ya elimu ni kugeuza kioo kuwa dirisha. Ana maanisha nini; elimu itusaidie kubadilisha mtazamo wetu wa kibinafsi tuwaangalie na wengine ambao wako kwenye mazingira magumu katika utekelezaji wa jambo hili. Sasa walimu tunapowaandalia kwa mikataba hii badala ya kuangalia mazingira yao; walimu leo wanahitaji comfort tu, wanahitaji faraja wanatakiwa walipwe mishahara yao, walipwe stahiki zao; sasa tunawapelekea mikataba ya kuwachelewesha kufanya kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana, na bado matamshi mengine yanaendelea, tunataka kufuta TAHOSA tunataka kufuta sijui umoja wa Afisa Elimu sijui wa wakuu wa Shule. Hizi forum kazi yake kubwa ni mkono mrefu kumfikia mwalimu, sasa Serikali inataka kuukata huo mkono? kwa kweli si sawa. Nimeanza na hili niwaombe wenzangu wa TAMISEMI na ninajua Dkt. Msonde ananisikiliza kwa makini sana jambo hili lifike mwisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niangalie eneo lingine la Kilimo. Leo Wizara ya Kilimo imekuja na BBT, Building Better Tanzania. Mradi huu unakwenda kila mkoa na sisi juzi kwenye ALAT Mkoa Mkuu wangu wa Mkoa alikuja na mkakati mzuri sana; kwamba walau kila kaya ambayo wanalima wawe na nusu heka ya kulima alizeti jambo. Sasa, changamoto ninayoiona hap ani kwamba, ni nani anakwenda kutekeleza jambo hili?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaye afisa ugani; lakini huyu afisa ugani mwajiri wake ni Mkurugenzi, Mkurugenzi jukumu lake ni kusimamia mapato. Afisa Ugani kapewa pikipiki kutoka Wizara ya Kilimo lakini huku chini ameenda kukabidhiwa poss ya kukusanyia mapato, ndicho kipa umbele cha Mkurugenzi. Hatuwezi kufikia malengo kwenye Wizara yetu ya Kilimo. Nataka niombe Serikali hawa maafisa ugani tuwakabidhi Wizara ya Kilimo ili waweze kurudi huku kusimamia Kilimo chetu. Tukiendelea na mpango huu maana yake hakuna mradi wowote ambao tutautekeleza ili kuwasaidia Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo lingine la Afya, wamezungumza vizuri sana. Nataka nizungumzie maeneo mawili moja ni CHF iliyoboreshwa. Watanzania hapa tunapozungumzia CHF iliyoboreshwa maana yake tunazungumzia ukusanyaji wa maduhuli, hatuzungumzii huduma ambayo wanaipata. CHF iliyoboreshwa watu hawapati huduma stahiki kwa sababu anatakiwa ahudumiwe ndani ya hospitali ya Serikali, nje hawawezi kupata huduma; na humu ndani hawawezi kufanya hivi. Wenzetu wa NHIF wamefanya kazi nzuri, wana miongozo, wana sheria na wanafuatilia kuanzia ndani na nje kwa maana ya Serikalini na kwenye private sector watu wanapata huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe ushauri kwa nini hawa CHF tusiwa-link na NHIF ili kutoa huduma kwa pamoja badala ya sasa kuwa na organ mbili tofauti? Kwamba hawa wanatoa huku hawa wanatoa huku, lakini wote wanamhudumia Mtanzania mmoja. Ni vema tukatengeneza jambo hili likawa jambo moja watu wapate huduma kwa pamoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti,mwisho , naomba nimalizie kwa kuiomba Serikali, kazi kubwa ambayo wanatakiwa wafanye Wizara ya TAMISEMI ni utawala, monitoring and evaluation na coordination. Suala la usimamizi wa miradi wawaachie Wizara za Kisekta, wawaachie Wizara ya Kilimo, Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya. Watakapotunga sera na sheria zao na miradi yao waende wakaitekeleze wenyewe huku chini. Kazi ya TAMISEMI ibaki kufanya tathmini ya utekelezaji wa hiyo. Mfano mmoja mwepesi sana, Wizara ya Utumishi na Ofisi ya Rais lakini wanafanya kazi yao vizuri, sasa na hawa ni Ofisi ya Rais wafanye kazi hiyo hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tulizungumza hapa mwaka 2017/2018 juu ya Idara ya Maji; na nilishauri Idara ya maji hii iende kwenye mamlaka za maji. Leo tunaona RUWASA wanavyofanya vizuri. Miradi inatekelezwa vizuri mno kwa sababu wanajitegemea; na huku pia tufanye utaratibu huo watu waweze kujitegemea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaombe wenzangu wa TAMISEMI, Jimbo la Singida Mjini tunayo Hospitali ya Wilaya, hatuna watumishi na hatuna vifaa tiba, naomba viletwe. Lakini kata moja ambayo imebaki ni kata ya Kisaki, kata ambayo mimi na wananchi wangu tumefanya kazi kubwa ya ujenzi sasa tunahitaji fedha kwa ajili ya kukamilisha na tunahitaji watumishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.