Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio na Mapato ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa sana na kuiweka nchi yetu katika hali ya usalama amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza mheshimiwa waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimae kuiwakilisha hotuba hii katika bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa sana Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kuhusu barabara; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyochukua jitihada kubwa za kuweka kipaumbele juu ya ujenzi wa barabara zetu. Barabara ni miongoni mwa vichochezi vya maendeleo katika nchi. Barabara zinapokuwa katika hali nzuri itaweza kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wananchi wetu wakulima.

Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba kwanza TARURA ioengezewe fedha ili iweze kutekeleza malengo yake.

Pili, Serikali itilie mkazo barabara zifike vijijini ili kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kupeleka sehemu husika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu afya; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyochukua jitihada kubwa za kujenga zahanati katika maeneo yetu yote katika nchi yetu. Hili ni jambo zuri sana katika nchi. Hivi sasa karibu kila mkoa kuna zahanati za kisasa kabisa ambazo zinaleta matumaini kiafya.

Ushauri wangu katika jambo hili ni kwanza Serikali ihakikishe inaendeleza kupeleka vifaa tiba vya kisasa katika zahanati na hospitali hizo.

Pili bado masafa kati ya zahanati moja na nyingine ni makubwa sana kiasi ambacho bado inawapa shida wananchi kufuata huduma za afya hasa vijijini. Hivyo ni vyema Serikali ikaliangalia suala hili ili kuwawezesha wananchi hasa wa vijijini kufuata huduma hii ya afya katika masafa mafupi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.