Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumshukuru Mungu wa kunipa nafasi ya kuchangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, pili nampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za miradi ya maendeleo na tatu nikupongeze wewe Mheshimiwa Kairuki na naibu Mawaziri wako wawili kwa kazi nzuri mnazofanya katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, pamoja na shukrani hizi nina maombi machache; Halmashauri ya Mbulu Dc tulipewa fedha za kujengewa hospitali za halmashauri na kwa bahati mbaya sana hatukupata mgao wa fedha shilingi milioni 500 hivyo ikapelekea kutokamilika kwa hospitali hii, ombi langu mpeleke fedha ili ile hospitali ianze kazi. Tunaomba mlete fedha kwa ajili ya kumalizia Kituo cha Afya Maretadu ambayo tulipokea shilingi milioni 200 bado shilingi milioni 300 ili kumalizia kituo hicho kianze huduma kwa wanachi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu vituo vya kimkakati vya Masieda, Getanyamba, Labay, tunaomba tupewe fedha vya kumalizia maboma hayo ambayo wananchi wameanza kujenga. Maboma ya zahanati tunaomba fedha za zahanati saba ambazo zimejengwa kwa nguvu za wanachi na pia zipo katika hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kuhusu maboma ya shule za msingi na sekondari, tunaomba fedha ili kumalizia maboma ya shule zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa TARURA tunaomba TARURA waongezewe fedha za kujenga mtandao wa barabara maana tuna madaraja ya Eshkes, Maretadu, Geterer, Endahagichan na Gidihim hivyo naomba sana tuongezewe fedha hizo ambazo zinafikia shilingi bilioni nne.

Suala la uhaba wa watumishi; hatuna mhandisi wa majengo, PMU na wahasibu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mgao wa maeneo ya utawala tunaomba ianzishwe Tarafa ya Yaeda Chini/ Masieda. Pia mgao wa kata na vijiji vya Mbulu Vijijini.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.