Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Taifa letu kwa kutuletea maendeleo ambapo sasa nchi yetu inapiga hatua haraka kutokana na kazi nzuri, tunampongeza sana.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Buyungu ni miongoni mwa majimbo ambayo tumepewa fedha nyingi. Tunashukuru na kupongeza sana.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii pamoja na mambo mengine tunaomba kupewa fedha kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa stendi ya mabasi ya mjini Kakonko unaondelea; fedha kwa ajili nyumba za walimu na madaktari; fedha za ujenzi wa barabara kilometa tatu alizoahidi Rais Magufuli na zitengwe fedha za dharula kwa ajili ya TARURA.