Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara ya TAMISEMI.

Pamoja na kupongeza kazi nzuri ya TARURA, naomba iongezewe fedha shilingi milioni 250 ili kukamilisha barabara muhimu ya Mahakama yenye kilometa 1.5. Hadi sasa zimetengwa shilingi milioni 500. Tafadhari sana tusaidiwe barabara hizo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kupongeza Serikali kwa ajira mpya za walimu, tunaomba kipaumbele wapewe walimu waliojitolea.

Mheshimiwa Spika, natanguliza shukrani.