Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kuchangia kwa njia ya maandishi kwenye bajeti hii muhimu ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kutoa ushauri muhimu sana hasa juu ya mgawanyo wa fedha za miradi zinazoletwa katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais juu ya fedha nyingi zilizoletwa kwenye jimbo langu la Kwela na hivi karibuni tumepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na shule kwa shule za misingi. Kwenye Jimbo langu nakiri Halmashauri yangu kupokea fedha kwa ajili ya shule mbili zenye mikondo miwili ambapo Shule ya Motowisa A tumepokea shilingi 538,500,000 na Shule ya Tuwi iliyopo Ilemba B imeletewa shilingi 538,500,000.

Mheshimiwa Spika, pia fedha kwa ajili ya madarasa na vyoo kwenye Shule ya Laela B shilingi 75,000,000, Shule ya Kisa Kata ya Milepa shilingi 75,000,000, Shule ya Nankanga shilingi 100,000,000, Shule ya Kaoze shilingi 69,100,000, Shule ya Kinambo Kata ya Milepa shilingi 75,000,000 hivyo kufanya jumla kuu kuwa shilingi 1,497,100,000. Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kupokea fedha hizi naomba kuleta kwako Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI mapendekezo ya mgawanyo wa madarasa kwa awamu zijazo kwani Jimbo la Kwela ni kubwa sana lina kata 27 na kila kata wamejitahidi sana wamejenga maboma ya zaidi ya miaka mitano. Ushauri wangu kwamba kwa wakati mwingine Serikali ione kuna haja ya kufanya mgao walau kila mahali waweze kupata kidogo kwani shida na uhaba upo kila mahali ndani ya Jimbo la Kwela.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano maeneo ambayo mmepeleka fedha za BOOST ndio hayo hayo yalipata fedha za SEQUIP kwenye sekondari. Hii inapelekea maeneo mengine kuona kama wametengwa. Pamoja kwamba mnaweza kuwa mnatumia takwimu, lakini suala la kuleta usawa ni muhimu sana kwani kila eneo wanataka kupata walau fedha kidogo toka Serikali Kuu.

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumuomba Mheshimiwa Waziri wakati mwingine wanapotaka kupeleka fedha za miradi huko majimboni watushirikishe ili tuweze kushauriana, tofauti na sasa hivi wanaleta fedha ambayo badala ya kutuleta pamoja inasababisha mipasuko ya kimaeneo hasa kwa majimbo yetu kama Jimbo la Kwela ambalo jiografia yake ni ngumu sana. Kwa mfano awamu hii ya BOOST mapendekezo yetu hayakuzingatiwa na Wizara kabisa badala yake wametumia takwimu zao walizonazo Wizarani. Kwa mfano mapendekezo yetu ya mradi ya BOOST yaligusa kila eneo kwa kuzingatia uhitaji wa maeneo kama nilivyoaanisha kwenye jedwali hapa chini.

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mapendekezo ya bajeti ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa fedha za Programu ya Elimu ya Lipa kwa Matokeo (EP4R/BOOST) kwa mwaka 2022/2023.

JEDWALI

Mheshimiwa Spika, naomba sana Wizara ingalie namna ya kugusa maeneo yote kama nilivyoainisha ili kila eneo au kila kata wapate walau madarasa mawili au matatu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na ahsante sana.