Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Aloyce Andrew Kwezi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. ALOYCE A. KWEZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nichukue nafasi hii na mimi kuwa miongoni mwa wachangiaji wako wa leo.

Kwanza niseme kabisa bajeti hii naiunga mkono, mbili niwapongeze sana Waziri na Naibu Waziri pamoja na Mtendaji Mkuu na timu yake yote kwa kazi nzuri ambayo wanafanya katika Utumishi wetu wa Umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina mambo ambayo ninapenda kuyazungumzia lakini nisipogusa maslahi ya watumishi katika Jimbo la Kaliua na nchi nzima nitakuwa sijatenda haki kwa wananchi, nitakuwa sijatenda haki kwa watumishi wa Umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo Wilaya, zipo Halmashauri, zipo RAS, zipo Wizara, mpaka sasa bado zinadai malimbikizo. Kwa hiyo, naomba ndugu zangu hawa wahakikishe kwanza malimbikizo ya mishahara yanalipwa kwa wakati, mbili wahakikishe yale madeni yote wanayodaiwa kwa mfano Kaliua kuna madeni mpaka sasa watumishi bado wanadai, madai ya uhamisho, madai ya likizo, madai ya matibabu Milioni karibu 170, wawape wale watumishi wanafanya kazi nzuri sana ya kuijenga Kaliua.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la msingi ambalo ningependa kulichangia kwanza niombe Wizara hii, ninapata kigugumizi ninapokuwa kwenyeJimbo langu. TAKUKURU
hawana Ofisi ya Wilaya, TAKUKURU wamepanga kwenye nyumba za watumishi, hivi huyu mtumishi anapo - misbehave TAKUKURU anamchukuliaje hatua wakati yeye ni mpangaji wake? Badala yake utamchukulia hatua leo, keshokutwa na yeye anakupandishia kodi unakuwa unahama hama. Kwa hiyo, ninakuomba Mheshimiwa Wakili Msomi, tena mko wawili wote hapo watani zangu. Niwaombe sana kwenye bajeti hii tafadhali sana Kaliua tunahitaji Ofisi ya TAKUKURU.

Mheshimiwa Naibu Spika, TAKUKURU wa Kaliua wakiongozwa na Ndugu Abdallah kazi wanafanya nzuri sana. Kwa hiyo, kama wanafanya kazi kwenye mazingira magumu hebu tupeni ofisi ili wafanye kazi kwa uzalendo wao kuokoa fedha za umma na mambo mengine mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda pia kushauri kwenye suala la wastaafu, wastaafu wetu jamani maisha asilimia 90 ya watumishi wa umma walioajiriwa yanaishia kazini. Unaingia kazini una miaka 18 pengine mpaka miaka 60 hii ni asilimia 90 ya maisha yake, sasa wanapostaafu nini kinatokea? Nje ya usumbufu wa mafao yao yote, usumbufu mkubwa wanaokuja kuupata mimi nasema ni kwenye pension, sijaona utumishi wamekaa chini wanasema, umestaafu ile pension wanakupa mshahara wako wa mwisho. Hivi kwa maisha yanavyozidi kubadilika mtu umestaafu ukabahatika kuishi miaka mia moja na, kama wazazi wangu wako Kaliua pale wana miaka mpaka mia moja, bado ile ile hela waliostaafu nayo ya pension haiongezeki.

Mheshimiwa Naibu Spika, challenge ya maisha haya tunakwenda hivi mpaka lini? Kwa hiyo, ni lazima tuangalie hawa wastaafu wetu angalau kwenye kile cheo alichostaafu nacho si kuna watumishi wanaendelea nacho? Kwa mfano, Wakurugenzi wana SSE kwa hiyo wale ambao wana hiyo na walistaafu kwenye level ile basi tutegemee watakapobadilika wa sasa na wale wastaafu pension zao ziweze kubadilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la msingi jingine niliseme la team work, naomba mje mjifunze Kaliua. Kwa kweli kuna teamwork nzuri sana kuanzia Mkuu wangu wa Wilaya Rashid Chuachua, yuko vizuri. Niko Jimboni lakini kule akizunguka atamsema Mama Samia miradi mizuri sana, atamsema Mbunge Kwezi miradi mizuri sana, atawasema Madiwani tena wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu nataka niwaambie hawa viongozi nimefurahishwa sana na Utumishi kitendo mlichokifanya juzi cha induction course kwa Wakuu wa Wilaya, wafundisheni kwa sababu mtu anatoka sehemu hajui majukumu ya Mkuu wa Wilaya, hajui majukumu hata ya wale anaofanya nao kazi ana-share vipi, team work inakuwaje hapo? kwenye Sheria Namba 8 ya 2002, Kanuni za Septemba 2003 mmeongelea Kifungu cha 65 teamwork. Sasa Public Servant maeneo mengi unakuta wengine wanafeli kwa sababu utakuta Mkuu wa Wilaya fulani amekuwa kibaraka wa mgombea fulani, Mkurugenzi fulani anafeli sehemu fulani, sasa haya yanatuangusha, lakini mkishawaeleza kama mlivyowaelimisha juzi kwa kweli kile kitendo kinaendelea kutuimarisha. Nilitaka niwathibitishie Utawala Bora pale tupo vizuri, tunahitaji tu kwenye TAKUKURU mtupatie hiyo ofisi, tunahitaji na gari ya TAKUKURU ili wakina Abdallah na team yake waendele kufanya kazi vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ambalo ningeweza kulisema Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana hivi karibuni ya kuhakikisha mishahara inaongezeka. Mishahara imeongezeka kwenye mazingira ambayo vitu vingine vyote kulikuwa na mfumuko wa bei, watumishi hawajaona impact kubwa. Nataka niwashauri, mwaka huu mpaka sasa tunaongea ni mwezi Aprili hakuna promotion iliyofanyika mwaka huu. Sasa tunamaliza mwaka bajeti ilishatengwa kwamba ile mishahara yao ya promotion ilitengwa kuanzia Tarehe 01 Julai, sasa tunakwenda mpaka Tarehe 30 Juni, hapa katikakati imebaki miezi minne, mnapokuja kutoa mnatoa with effect kwenye Tarehe ambayo mmetoa barua zenu za promotion, bila ku-consider kwamba hii bajeti ilikuwepo toka Tarehe 01 Mwezi Julai, naomba mlizingatie hili ili watumishi wa umma waneemeke na maslahi mbalimbali ya kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nichangie pia kwenye eneo moja kubwa sana la allocation ya human resource na maadili, hapa ndiko kuna shida. Hivi vetting mnazifanyaje ndugu zangu? Yaani unafanya vetting leo mtumishi anateuliwa kesho, mambo hayakwenda vizuri, mwezi mmoja mnatengua. Hawa ina maana hamjafanya vizuri vetting si ndiyo hivyo? Sasa mimi nilitaka nishauri kwamba chunguzeni kwa kiasi cha kutosha na mtoe majibu kwa wakati. Mnaziumiza Halmashauri na vetting hizo, kuna Idara mtu anakaimu na kukaimu na kukaimu kibaya zaidi hamuwaambii kwa wakati kwamba huyu hafai, unakuja kukuta alishakaimu hata miaka miwili, miaka mitatu halafu unamletea mtu mwingine, matokeo yake kunakuwa na conflict of interest. Mtu alishajenga matumaini, alijenga na mambo mbalimbali haya hatuyafanyi, niwaombe sana Mawakili Wasomi zingatieni hizo sheria kwa kuhakikisha wananchi wetu wananufaika vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuwataja hawa wanaokaimu mimi nataka niongelee crisis kwenye suala la ajira. Ajira tumefanya vizuri na jana tumeshauri vizuri kweli, lakini hizi ajira mimi nataka muangalie na kwenye private sector. Private sector kuna miradi mikubwa inaendelea, pale Kaliua kumeanza mradi wa kukarabati ile reli ya kutoka Kaliua kwenda Mpanda na sasa kuna lot ya Tabora - Kaliua mpaka Kigoma. Watu ambao wanakuja mimi nilitegemea wananchi wa Kaliua, wananchi wa Urambo wananchi wa Ulyankhulu mule ambako mradi unapita, sasa wananchokifanya sasa hivi wanahama na watumishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watumishi ametoka nao hapo Makutupora watani zangu Wagogo wame-enjoy wamenufaika tena tumewafundisha ujanja Wanyamwezi wakifika kule wanahama nao sasa wanaleta rundo kule. Wale Wanyamwezi wangu wanabaki benchi maana yake nini? Hivyo, katika kwenye hii miradi mfuatilie siwaambii huu ni utani, hata sasa hivi mkitaka m - prove nendeni pale kwa sababu wamesimika pale Zugimlole kuna stesheni pale, utakuta wamehama na watu zaidi ya 20 nikawa nauliza hawa? Eti hawa ni mafundi. Mafundi 30 halafu fundi mwenyewe kazi yake ni kubeba tofali wananchi wa Kinyamwezi kule hawana nguvu hizo? Wafipa hawana nguvu hizo? Waha hawana nguvu hizo? Siyo kweli. Kwa hiyo nataka niwaambie haya tukiyafanya tutajenga heshima ya Mama vizuri sana, tutaondoa malalamiko ambayo hayana tija vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sahani hii nilitaka niwashauri kitu kingine kuhusu uboreshaji wa miundo hii. Miundo inakaa kwa muda mrefu sana, mabadiliko yanaenda na sayansi na teknolojia, ninyi bado mnashangaa huku, shida ni nini kwanza? Kwa nini hamjiimarishi? Kibaya zaidi hapa kwenye uimarishaji wa Ikama nilitaka niseme hapa, Halmashauri kule tunawaomba kwamba mwaka huu Kaliua tunataka tuajiri watu 205 tukileta huku ninyi mnakuja kutupa chukua watu 15 hivi kweli tatizo litaisha. Ninachowaambia kwa mfano, mimi Kata zote za Jimbo la Kaliua hakuna Afisa Maendeleo ya Jamii kwenye Kata. Hayo maendeleo wananchi wanahamasihwaje? wamelima tumbaku vizuri sana, wangetegemea Afisa Maendeleo wa Jamii atapita kuwaelimisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwaambia jamani Kata zetu ziko 13 zinahitaji hiki na hiki, bado mnatakiwa mchukue ushauri wangu. Baada ya kuyasema haya siwezi kuzuia bajeti yao hawa, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)