Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya ufinyu wa muda niombe kuleta mchango wangu kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, niIpongeze Serikali kwa ajira ambazo imetoa kwa kipindi cha miaka miwili, lakini nitoe ushauri kwenye ajira kama ifuatavyo: -

Kwanza imefika wakati sasa tujikite na kwenye ajira za kada ya uchumi, maafisa mipango, na kadhalika, hawa wamesahaulika.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2020 Menejimenti ya Utumishi ya Umma walitoa kibali cha kuajiri wahandisi kuwa walimu wa shule za ufundi kama Ifunda, Moshi Technical na kadhalika. Vijana hawa 60 miundo ya ualimu hasa Tume ya Walimu haiwatambui hivyo hawana barua za ajira, hawawezi kuthibitishwa kazini. Niombe suala hili litafutiwe ufumbuzi.