Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya tabianchi ni tatizo na athari zake zinaongezeka kila mwaka. Nchi zilizoendelea, zimechangia kwa kiasi kikubwa kwenye ongezeko la hewa ukaa angani, ambayo imesababisha upandaji wa joto duniani. Kwa mujibu wa makubaliano kwenye mikutano ya kimataifa, nchi hizo zilitakiwa kusaidia nchi zinazoendelea na masikini kwa kutoa utaalamu, teknolojia na fedha za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi. Je Tanzania tumenufaikaje na Climate Change Green Funds?

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ina miti mingi na hasa maeneo yenye mvua nyingi kama mkoa wa Kagera, miti inayosadia kunyonya hewa ya ukaa angani. Je, kama nchi na kama mkoa tumenufaikaje na Carbon Credit?

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya mvua nyingi sizizotabirika, Mto Kanoni katika Manispaa ya Bukoba hufurika kila mwaka na kusababisha uharibifu wa mali, nyumba, mifugo na hata kusababisha vifo vya watu na mifugo. Serikali iliahidi tangu Januari, 2023 kuanza kuongeza kina na kujenga kuta wenye kingo za Mto Kanoni. Ni lini fedha hizo zitaletwa ili kuondoa adha ya mafuriko ya kila mwaka?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile maeneo ya Custom, Kafuti, Nyamkazi zinafurika sababu kina cha Ziwa Victoria huongezeka. Wakazi wa maaeneo haya wamekuwa wahanga wa mafuriko, wanafilisika kwa sababu ya vitu vyao na nyumba zao kuharibika kila mwaka sababu ya mafuriko. Kwa nini kusijengwe kuta kando kando ya ziwa kuwanusuru hawa wananchi?

Mheshimiwa Naibu Spika, Idara ya Mazingira katika Halmashauri zetu hazipewi kipaumbele ili wakabiliane na athari ya mabadiliko ya tabianchi, inabidi wapewe bajeti ya kutosha. Wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Napendekeza bajeti za Idara za Mazingira kwenye Halmashauri zetu, pia na bajeti ya Wizara hii iongezwe, sababu wana majukumu makubwa na mahitaji yanaongezeka sababu ya mabadiliko ya tabia nchi. Inabidi kama nchi tulione hili tatizo la mabadiliko ya tabianchi, tulipe umuhimu unaotosha, tulipe bajeti inayoridhisha na wakati wa kufanya hivyo ni sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.