Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Kilolo kuna mwekezaji anaitwa Udzungwa Corridor ambaye anawekeza katika kupanda miti ya asili kwa ajili ya uvunaji wa hewa ya ukaa. Shida iliyopo ni ukiukwaji wa taratibu za umiliki ardhi na uwazi katika uwekezaji huo. Naiomba Wizara ije na majibu je, inamfahamu mwekezaji huyu? Kuna haja ya Wizara kushirikiana na Halmashauri kuona ni jinsi gani mwekezaji huyu ataheshimu mikataba yake na wananchi na kuacha kununua maeneo ya wananchi wanayoyatumia kwa shughuli za kilimo. Mwekezaji huyu amenunua hadi eneo la ujenzi wa shule ya sekondari.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili; Kilolo ina misitu mingi ya asili kuna haja ya Wizara kutoa support kwa Halmashauri ili kuanza uwekezaji.