Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nami nianze kwanza kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais, Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya kwenye majimbo yetu, na pia kwa kukubali na kuridhia kuinua sekta ya Wizara hii ya Kilimo kwa kuiongezea fedha. Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana Mawaziri, watendaji wote, hasa Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji, ndugu yangu Raymond Mndolwa kwa namna ambavyo amejikita kuhakikisha angalau skimu mbalimbali ambazo zilikuwa ni mapendekezo ya Bunge zinaweza kufanyiwa kazi na zinatengewa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukurani hizi kipekee nichukue nafasi hii kukushukuru sana Mheshimiwa Waziri, nimeona kwenye bajeti ya mwaka huu, zipo schemes za wilayani kwangu Wilaya ya Rorya, kwa muda mrefu tumekuwa tukiziombea ziingie kwenye mpango mkakati na umeezingiza. Ikiwemo scheme ya Rabong nichukue nafasi kukushukuru, ikiwemo Chereche, Ryangubo, Rwang’enyi pamoja na scheme ya Mto Mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani hizi Mheshimiwa Waziri, yapo mambo ambayo ningetamani nishauri kwa maana ya Mkoa wetu wa Mara. Mheshimiwa Waziri, utakubaliana na mimi pamoja na kwamba Mkoa huu ndio Mkoa anaotoka Muasisi wa Taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na kwamba mkoa huu ndio anaotoka Muasisi aliyekuwa anaAsisi sekta na Wizara unayoiongoza ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia utakubaliana na mimi kwamba Mkoa wa Mara ukiuzungumzia kwa sasa ni mkoa ambao hauna zao la kimkakati, hauna zao la kibiashara na ni mkoa ambao hata mazao yanayolimwa ya chakula haya- sustain. Ni mazao ambayo yanalimwa kwa ajili ya chakula cha kujilisha wenyewe na sio mazao yanayokwenda kwenye sekta kwa maana ya kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, nimekuwa nikishauri hapa ndani ya Bunge, sio kwamba tunapungukiwa baadhi ya mambo yanayoweza kutufanya na sisi tukawa na mazao ya kimkakati na mazao ya kibiashara kama ilivyo mikoa mingine. Nadhani ni uamuzi wa Wizara na intervention ya Serikali a very serious interventions ambayo inaweza ikatusaidia sisi kama mkoa kutupa direction ya namna njema ya kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Mara utakubaliana na mimi Mheshimiwa Waziri, tuna zaidi ya hekta milioni mbili lakini tunazalisha hekta laki mbili mpaka laki tatu peke yake. Mazao tunayolima mengi yao ni mahindi na tukilima yale mazao ni mazao ya chakula peke yake. Hatulimi mazao kwa ajili ya kufanya kwa maana ya kujiinua kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia utakubaliana na mimi ni mkoa ambao tuna irrigation scheme zaidi ya 42, lakini zinazofanya kazi hazifiki hata 10 peke yake. Ni mkoa ambao umezungukwa na ziwa, kwa mfano wilayani kwangu asilimia 77 nimezungukwa na ziwa lakini hakuna mazao yanayolimwa ambayo unaweza ukasema haya ni mazao ya kibiashara ya kumkomboa mwananchi kwa ujumla wake na yakatangaza ule mkoa kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Mheshimiwa Waziri, katika ziara hizi unazozunguka, kwanza upe Mkoa wa Mara kipaumbele, tengeneza a very serious intervention ya kuja kwenye Mkoa wa Mara na kutengeneza ushauri kuona namna unavyoweza kukaa na wadau wa sekta ya kilimo na wananchi wanaofanya shughuli za kilimo ili kuinua mazao ya kibiashara ili leo tunaposimama sisi kama mkoa tuwe tuna zao la kibiashara tunalotambua kama mkoa, kuwe kuna zao la kimkakati lakini pia utengeneze strategies nzuri ya kuona namna unavyoweza kuwakwamua wakulima hawa wanaolima mazao madogo madogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niombe sana Mheshimiwa Waziri, hili ulione kwa jicho pana sana. Kwa sababu ukanda ule sisi Mkoa wa Mara ndio maana unaona hakuna tunachoweza kusimama. Siwezi kuzungumzia mbolea, siwezi kuzungumzia pembejeo na wakati hata kilimo kinachofanywa bado ni kidogo sana. Tunafanya small scale agriculture ambayo tungeweza kufanya large scale ili wananchi waweze kunufaika. Sasa nikuombe kwa kuwa umeanza kuzunguka maeneo mengi na haujafika Mkoa wa Mara, nikuombe uje in a very serious ili tukae tuweze kuona namna ambavyo tunaweza Kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba unafanya haya nikuombe Mheshimiwa Waziri, la kwanza kwenye zile scheme 46 pamoja na kwamba naona zimetengwa fedha lakini bado hazizidi scheme 10, nenda uone namna ambavyo zile scheme zote arobaini na kitu unavyoweza kuzipa fedha ziweze ku-produce ili wananchi waanze kulima kilimo cha biashara. Naona sasa scheme zinatumika kulima kilimo cha chakula peke yake. Pia, haya unayaweza naona maeneo mengine umekuwa ukifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, uone namna ya kutengeneza mahusianao mazuri ya private sector ili ziweze kuwekeza kwenye mazao ambayo yanweza yakai–boost kutenegeneza mazao ya kimkakati na mazao ya kibiashara na hili unaliweza kama ambavyo umekuwa ukifanya mikoa mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, utengeneze Mkoa wa Mara kuwe kuna soko rasmi la kuuza bidhaa. Leo sisi tunauza bidhaa zetu kwenye magulio na haya masoko ya kawaida. Hatuna soko rasmi ambalo wananchi wanauza bidhaa ambalo lita–motivate wananchi kuzalisha zaidi wakijua kuna mahali pa kuuza. Leo wakizal;isha inabidi wavuke waende Kenya kutafuta soko ambalo linaweza likawanufaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani sisi kama mkoa ungeweza kutengeneza namna nzuri ya kutengeneza soko zuri moja wapo katika ukanda ule. Kwa bahati nzuri ukanda wote wa ziwa hakuna soko kubwa ambalo linauza mazao ya chakula kwa ujumla wake. Ona namna mkoa ule kwa sababu uko mpakani uweze kutusaidia tuweze kupata masoko mazuri ya kuuza bidhaa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la nne, utakapokuwa umekuja ona namna ambayo tupate ghala la chakula ambalo litawafanya wakulima badala ya kuuza bei ya chini mazao yao wanapolima, waweze kuhifadhi wakisubiri bei nzuri ili na wao waendelee kutengeneza motivation. Pia, ninaamini kwa kufanya hivi utaweza kuwa motivate wakulima wengi pamoja na vijana ambao kimsingi wameamua kujiajiri kwenye sekta ya kilimo lakini hawana uwezo na hawana soko la uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Mheshimiwa Waziri in a very serious kama nilivyosema, lazima utakaposimama hapa…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JAFARI W. CHEGE:… leo utuambie katika ukanda ule ni zao gani la kibiashara ambalo umeweza kuainisha na zao la kimkakati kwenye mkoa mziama wa mara. Tunayo mazao tunayolima ambayo yanakubali ardhi ya upande ule, Kahawa inakubali, tumbaku inakubali, mkonge unakubali. Pamba imekuwa ikilimwa kwa muda mrefu na wewe ni shahidi, lakini haya mazao haya yamekufa kwenye Mkoa wa Mara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani tukianza kuzungumza Mkoa wa Mara, hakuna zao tunalosimama nalo kama Mkoa. Sasa hatuwezi kwenda kwa style hii. Kama nilivyosema ni mkoa anaotoka muasisi ningetamani unavyosimama na wewe Mheshimiwa Waziri, ujivunie Wizara unayoiongoza muasisi wa sekta uya kilimo ni Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, sisi tungeona Mkoa wa Mara, unatunyenyuaje kwenye sekta ya kilimo, kwenye maeneo yote na sio hivi tunavyozalisha kwenye mazao ya chakula peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazalisha mahindi tani laki mbili mpaka laki tatu kwa mwaka na wakati mahitaji ni zaidi ya tani 600,000 mpaka 700,000. Kwa hiyo, hata hiyo nusu yenyewe hatufiki hata hilo zao moja lenyewe hatuwezi kufika. Kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwa Waziri,...

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. JAFARI W. CHEGE:…utakapokuja kusimama jioni hapa uweke mpango mkakati wa namna utakavyokuwa kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, nakushukuru sana naunga mkono hoja.